Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 228
- 249
Wakati upo darasa la kwanza ukifanya vizuri wanakuambia oooh subiri darasa la tatu ndio hesabu zinakuwa ngumu, ukifika darasa la tatu unaambiwa darasa nne kuna mtihani wa taifa kuvuka ni issue, unaingia la tano unaambiwa sasa shule ya msingi ipo darasa la sita. Unapoingia la saba unakutana na ambao wako form one wanakutisha kuwa huku huwa ni kiingereza tupu na shule ipo huku. Unapoanza kidato cha kwanza wanakuambia hapa rahisi shule ipo form Two kuna mambo ya logarithms na set na mtihani wa taifa. Inshaaallah unaingia kidato cha pili unaambiwa huku rahisi sekondari ipo form 3 na 4 hapo ndio elimu ya sekondari ilipo. Ukiingia kidato cha nne unaambiwa kuwa Kidato cha tano na sita siyo poa huku unahitaji evidence. Kama ni historia inabidi ujue hata vasco dagama wakati anatua Cape town alikuwa na usafiri wa aina gani na alitua saa ngap?. Mungu si Athuman unaingia kidato cha tano na sita, sasa hapo unakutana na watu walio chuo kikuu wanakuambia Chuo kuna bata ila huku siyo poa na hakuna tuition lazima uwe vizuri sana. Chuo unaingia na mkopo unapata ukipost picha nzuri upo chuo utawasikia muache huku kitaa ndio chuo kipo maisha magumu hatari. Baadae unamaliza chuo na maisha yanaendelea kama wao.
Mlimwengu mimi nilichokigundua binadamu anapenda kukupa ugumu hataki ufurahie maisha uliyo nayo anataka uishi kwa wasiwasi. Live now ndugu zangu. Ukila bata sasahivi watakuambia subiri uoe utapata shida. Na unapopata mke watakuambia subiri upate watoto ndio kuna shida.
Maisha ni hayahaya furahia sehemu uliopo.
#mlimwengumimi
#jichoLaMlimwengu
#liveAtMaximum