Fikra: Wazungu na Tanzania!

Usipofanya wanavyotaka hao wazungu, wanakuondoa madarakani ama kuidhoofisha serikali yako.Mfano Gaddafi,Mugabe,lumumba,Nkrumah etc.Interest zao ni first.Hatujapata uhuru kamili.Nani alaumiwe?

Mushi!

Nafasi ya waafrika wachache wanaowasaidia wazungu hao iko wapi? Na viongozi legelege ambao hawajui nchi yao inaenda wapi ni tatizo la wazungu?

Tuendelee kujadili.

Sisi wenyewe ndio tatizo la msingi,ni kweli kwamba wazungu wangependa kuendelea kututawala lakini kama sisi hatujawapa nafasi inakuwa agenda zao kutimia

Kama sisi tukisimama imara nao watakosa namna ya kupenyeza unyonyaji wao

Kumbukeni baada ya uhuru tulichukua kila kitu tukaanza kuendesha wenyewe,shule bandari,mashamba na njia nyingine za kiuchumi.Na tulifanya vizuri kwa mda mrefu mpaka baadaye tulipoyumba kwa sababu zilizofahamika

Kwa kufuata historia hii naweza kukubaliana na school of thought namba 3

Mushi!

Nafasi ya waafrika wachache wanaowasaidia wazungu hao iko wapi? Na viongozi legelege ambao hawajui nchi yao inaenda wapi ni tatizo la wazungu?

Tuendelee kujadili.
Msando,hii isue ni very complex.Na ndiyo maana ninaamini kuwa wakulaumiwa ni both viongozi na wale wa nje wenye nia ya kutunyonya in any means neccessary.
Sisi huwa na tatizo moja kubwa,ambalo ni ku concentrate pale tulipoangukia badala ya pale tulipojikwaa.Misingi tuliyojiwekea toka mwanzo tulipopata uhuru ndiyo imetufikisha hapa tulipo.
Ndiyo ni kweli kwamba tatizo ni viongozi wetu.Hata hivyo bado ni kweli kwamba ni lazima wawasikilize hao "Bwana wakubwa"Wako under control,ni kama wanawafanyia kazi hao wazungu na si wananchi waliowachagua.Chaguzi zimekuwa kama viini macho.Kwani silaha za kujilinda dhidi ya wananchi hata kama wakitetea maslahi ya wazungu ie wawekezaji si wanapewa na wazungu hao hao?
Labda sijaelewa,if so nieleweshe.
Ninavyoelewa mimi ni kwamba nchi inapokwenda,lazima hao wawekezaji,wafadhili nk wawe na say.Mabadiliko yote tuliyoyafanya kwa shinikizo la world bank na IMF kuanzia mwalimu alipo ng'atuka sisi kama wananchi tulikuwa na say?Si mzungu alituamulia?Na mwalimu kwa kujua kuwa power yake ina limit pale inapokuja kwenye maamuzi ya hao wazungu,aliamuwa kuachia ngazi badala ya kula matapishi yake.Ni wazi bado hatujapata uhuru wa kweli.Hi mikataba wanayoingia hawa chief mangungos wetu ambayo tunaipigia kelele unadhani wanaijali?Unadhani kina Geita gold mining wanajali kuwa kuna poisonous materials inayowa athiri wananchi wakati wa operations zao?Bado wana nguvu zadi na bado wao ndiyo wanatutawala.Viongozi wetu ni manyapara tu ambao wanatumia fursa kujinufaisha.
Tuendelee na mjadala.

Nakubaliana na wewe asilimia 100. Siku zote wajinga wanatafuta scapegoat. Hitler alisingizia Jews, sisi tunasingizia wazungu. Mzungu ndio anakulazimisha ununue gari la waziri kwa mil 300? mzungu ndio anakufanya ujenge shule za kata zisizo na walimu? mzungu ndio amemgeuza rais wenu kuwa vasco da gama?
Kuna wazungu wanaipenda tanzania kwa moyo wao wote na kuna wanyonyaji, just like the case with our leaders...mfano; Slaa na lowassa, Mbowe na kikwete, huku tusimsahau mkapa....

Ndg,

Hakuna mzungu anayependa Tanzania kwa moyo wake wote!
Kwa tabia za wazungu, wao hupenda vitu vyenye manufaa au faida kwao, hivyo kupenda kwao Tanzania labda ni kutokana na wanachokipata.
Hata hivyo, mtu yeyote mwenye akili nzuri, mara nyingi atapenda kitu chenye faida kwake, hii ni hali ya asili na hata wanyama wanayo!U
Urafiki wa wazungu na Tanzania ni wa kimaslahi zaidi na si vinginevyo.
Nimefanya kazi na wazungu kwa zaidi ya 95% ya muda wangu baada ya kugraduate, kwa kiasi kikubwa najua wanavyofanya lobbying kwa watumishi wa uma na viongozi na wakati mwingine unaweza hata kutamani nguvu itumike kuwaondoa watumishi na viongozi hao kwenye nafasi zao na pia kuwafukuza wazungu hao hapa nchini.
Watanzania tunatakiwa tuwatumie wazungu kwa faida yetu na siyo wao watutumie kwa faida yao.
Tatizo kubwa ni mtazamo,mwenendo na matendo hasi katika kutekeleza majukumu yanayohusiana na uwepo wa wazungu au wageni wengine hapa Tz.
Hata hivyo, ni muhimu tujue kwamba Tanzania yetu tutaijenga wenyewe, yeyote yule mwenye mawazo kwamba Tanzania itajengwa na wazungu au wageni wengine ni adui na msaliti wa watanzania na hafai katika karne hii.Huyo alitakiwa awepo enzi ya utumwa!!!

Msando,hii isue ni very complex.Na ndiyo maana ninaamini kuwa wakulaumiwa ni both viongozi na wale wa nje wenye nia ya kutunyonya in any means neccessary.

Sisi huwa na tatizo moja kubwa,ambalo ni ku concentrate pale tulipoangukia badala ya pale tulipojikwaa.Misingi tuliyojiwekea toka mwanzo tulipopata uhuru ndiyo imetufikisha hapa tulipo.

Ndiyo ni kweli kwamba tatizo ni viongozi wetu.Hata hivyo bado ni kweli kwamba ni lazima wawasikilize hao "Bwana wakubwa"Wako under control,ni kama wanawafanyia kazi hao wazungu na si wananchi waliowachagua.Chaguzi zimekuwa kama viini macho.Kwani silaha za kujilinda dhidi ya wananchi hata kama wakitetea maslahi ya wazungu ie wawekezaji si wanapewa na wazungu hao hao?

Labda sijaelewa,if so nieleweshe.

Ninavyoelewa mimi ni kwamba nchi inapokwenda,lazima hao wawekezaji,wafadhili nk wawe na say.Mabadiliko yote tuliyoyafanya kwa shinikizo la world bank na IMF kuanzia mwalimu alipo ng'atuka sisi kama wananchi tulikuwa na say?Si mzungu alituamulia?Na mwalimu kwa kujua kuwa power yake ina limit pale inapokuja kwenye maamuzi ya hao wazungu,aliamuwa kuachia ngazi badala ya kula matapishi yake.Ni wazi bado hatujapata uhuru wa kweli.Hi mikataba wanayoingia hawa chief mangungos wetu ambayo tunaipigia kelele unadhani wanaijali?Unadhani kina Geita gold mining wanajali kuwa kuna poisonous materials inayowa athiri wananchi wakati wa operations zao?Bado wana nguvu zadi na bado wao ndiyo wanatutawala.Viongozi wetu ni manyapara tu ambao wanatumia fursa kujinufaisha.

Tuendelee na mjadala.

Mushi! Ni siku nyingine tena ndani ya nchi yetu tunayoipenda kwa moyo wote. Nakubaliana na wewe kwamba kuna mashinikizo kutoka kwa wazungu. Misaada yao inaakuja na masharti, mengine mazuri mengine mabaya. Lakini, hapo hapo linaibuka tatizo lingine, misaada hiyo tunaitumia vibaya!! Pamoja na masharti magumu bado wachache wanashindwa kuipangilia misaada hiyo.

Hatujui tutaendelea kusaidiwa mpaka lini. Hatujui kwanini tunahitaji kusaidiwa! Miaka hamsini sasa bado tunahitaji kusaidiwa! Huu ni uzuzu wetu!

Kuna msemo naupenda, kuna watu wanafaanikiwa sio kwa sababu ni wajanja ila kwa sababu wengine ni wajinga! So its about the latter's stupidity and foolishness the former succeeds!

Hatujaweka mkazo wa kutosha katika elimu, bado elimu yetu ni ya kusuasua! Hatuna priority tena! Eti kilimo kwanza! Kilimo cha jembe la mkono na kutegemea mvua??

Lazima tuchukue hatua haraka. Mimi na wewe.

Kwa hiyo waarabu na wahind na wachina poa? Tatizo ni viongozi wetu wala si wazungu

Kama hujui historia,then achana na siasa.Inaonekana wengi humu kwenye jukwaa la siasa hawajui history na how imeshape the current world.

nakuunga mkono kabisa hata mimi naona wengine humu hawajui wanachokichangia ila kwa ushauri tu kabla ya kuchangia mambo kama haya lazima uwe una ufahamu mkubwa wa mambo yalivyokuwa yalivyo na hata kuweza kusema yanaelekea wapi anayesem mzungu ni mzuri au rafiki lazima ana matatizo makubwa ya kiuchanganuzi wa mambo tena anatia huruma ila swala la udhaifu wa kiuongozi na kutojiamini kwa viongozi na kutokuwa wabunifu these are other things to discuss.lakini wazungu wabaya sana hawa na popote walipo hawako bure hili tutambue jamani ndio maana hata viongozi wetu wa hapo nyuma kama nyerere alisema tuishi nao kwa akili mno watu hawa.

Mushi! Ni siku nyingine tena ndani ya nchi yetu tunayoipenda kwa moyo wote. Nakubaliana na wewe kwamba kuna mashinikizo kutoka kwa wazungu. Misaada yao inaakuja na masharti, mengine mazuri mengine mabaya. Lakini, hapo hapo linaibuka tatizo lingine, misaada hiyo tunaitumia vibaya!! Pamoja na masharti magumu bado wachache wanashindwa kuipangilia misaada hiyo.

Hatujui tutaendelea kusaidiwa mpaka lini. Hatujui kwanini tunahitaji kusaidiwa! Miaka hamsini sasa bado tunahitaji kusaidiwa! Huu ni uzuzu wetu!

Kuna msemo naupenda, kuna watu wanafaanikiwa sio kwa sababu ni wajanja ila kwa sababu wengine ni wajinga! So its about the latter's stupidity and foolishness the former succeeds!

Hatujaweka mkazo wa kutosha katika elimu, bado elimu yetu ni ya kusuasua! Hatuna priority tena! Eti kilimo kwanza! Kilimo cha jembe la mkono na kutegemea mvua??

Lazima tuchukue hatua haraka. Mimi na wewe.
Msando,

Kama taifa hatuna mipango wala priorirties.Hatuna malengo kabisa.Kwanza tungejiuliza tuko wapi na tunataka kwenda wapi.Ni wazi kuwa hatuna long term strategies na matokeo yake ndiyo haya.

Kwa mfano swali dogo tu ambalo tungetakiwa kujiuliza ni je misaada hiyo ni ya kazi gani?Tunaipokea ili iweje?For how long?and then whats next?Je in a long run tuanataka tuachane nayo na kujitegemea wenyewe?Hapo ndo kwenye shida.Hatuna mipango ya muda mrefu,serikali inaendeshwa kizimamoto.No body knows about tommorow.

Hayo masharti wanayokuja nayo hao wazungua pia na yenyewe ni kuhakikisha kwamba misaada hiyo haituondoi kwenye umasikini.Kwasababu nadhani unaelewa ule usemi wa adui yako mwombee njaa...

Ukweli ni kwamba hatuwezi kuondoka kutoka kwenye umasikini kama serikali kila siku inafikiria tu namna ya kuwaplease hao wazungu,kujaza matumbo yao wenyewe pamoja na hizo 10%

Kama tungekuwa na priorities zetu kwamba sasa tuufute umasikini,maradhi na ujinga once and for all,then tungekuwa na masterplan ya where to start,how and why.Ndiyo maana unasikia kuna viongozi wengine wanasema kilimo kwanza,wengine elimu kwanza.However wamebakia hapo na kubishana tu bila kuchukua hatua.Haijalishi kama tutaconcentrate na lilpi first.Lakini all in all,tunahitaji tuwe na pahala pa kuanzia kwenye mission yetu ya kuutokomeza umasikini uliokithiri,maradhi na ujinga.

Ukitaka kujuwa prorities zetu si kitu,then angalia issue ya neti za mbu zinazotengenezwa na mmarekani kwa kigezo cha msaada na uwekezaji.Bush alifunguwa huko Arusha.Sasa rais wetu kweli anafikiri kumaliza malaria ni kuzalisha neti?Really?Marekani walikuwa na tatizo la malaria lakini hawakulimaliza kwa utengenezaji wa neti.Walipambana na mazingirana sasa wameutokomeza.Sasa sisi kutofanya hivyo bado nawalaumu wote viongozi/mangungo wetu pamoja na hao wazungu wanaotaka tuendelee kuwa tegemezi ili waendelee kutunyonya!

Kwa kifupi Msando,we got to have somewhere to begin.However kwanini tusianze na vyote hand to hand?Kama hizi pesa zote wazozifisadi wangezielekeza huko kwenye kilimo na elimu si tungekuwa tumepiga hatua?

Hata tukisema kilimo kwanza,haina maana kuwa elimu isipewe kipaumbele.Si kuna vyuo va kilimo?if so then ina maana hakuna kinachofanyika duniani chenye maendeleo bila uwepo wa elimu.Na kwa upande wa nchi yetu masikini,vyote must go together strategically.Nina amini tunahitaji ukombozi mpya.Kwa hali iliyopo kwasasa.

Uongozi wa taifa letu umekuwa ni kama usanii tu.Na ukweli ndo huo kuwa inawajali wazungu kuliko raia wake.Bila kuwa mbinafsi huwezi kuongoza taifa la Tanzania kwasababu ni mzigo mkubwa sana kama kweli una nia ya kuufuta umasikini uliokithiri,maradhi na ujinga wa kupindukia.

Acha niishie hapa kwasasa.Ntarudi.

Wakati nikiwa mdogo,kijijini kwetu ilikua akikatiza mtu mweupe awaye yote,wanakijiji hasa watoto walikua wanatoka na kushangilia wakiimba mzuuungu,mzuungu,mzuunguu..........
Nilipoendelea kukua mimi na marafiki zangu tulikua tunaona ujiko sana kama mzungu atakuongelesha na ilikua kama kuna mpiga picha karibu lazima uombe upige picha na huyo mzungu japo humjui hata kwa jina.
Sasa linapokuja hili swala la matatizo ya nchi hii mengi kuchangiwa na wazungu,ni kweli yapo na yanachangiwa na wengi wa viongozi wetu ambao wanaona ujiko kuongea na hata kupiga picha na wazungu ili mradi tuu wale wanaomzunguka wamwone kuwa yeye ni wa matawi ya juu.Viongozi wetu wengi ni malimbukeni,mtakumbuka ile story ya mzungu aliyewekwa hotelini kazi yake kusaini mikataba tuu na akaondoka na dau nono japo hakua na chochote alipoingia nchini.
Watanzania tumekua wavivu wa kufikiri na tumeazimisha akili zetu baadhi ya watu watusaidie kufikiri kwa niaba yetu.Ndo maana ukiangalia asili ya ufisadi wote ni lazima utakuta kama source sio mzungu,basi alishiriki kwa namna moja au nyingine hasa kwa mgongo wa uwekezaji.
Asikudanganye mtu watanzania tunawaogopa na kuwanyenyekea wazungu,ipo mifano ila kwa sasa sio wakati wake.

Ndg,

Hakuna mzungu anayependa Tanzania kwa moyo wake wote!
Kwa tabia za wazungu, wao hupenda vitu vyenye manufaa au faida kwao, hivyo kupenda kwao Tanzania labda ni kutokana na wanachokipata.
Hata hivyo, mtu yeyote mwenye akili nzuri, mara nyingi atapenda kitu chenye faida kwake, hii ni hali ya asili na hata wanyama wanayo!U
Urafiki wa wazungu na Tanzania ni wa kimaslahi zaidi na si vinginevyo.
Nimefanya kazi na wazungu kwa zaidi ya 95% ya muda wangu baada ya kugraduate, kwa kiasi kikubwa najua wanavyofanya lobbying kwa watumishi wa uma na viongozi na wakati mwingine unaweza hata kutamani nguvu itumike kuwaondoa watumishi na viongozi hao kwenye nafasi zao na pia kuwafukuza wazungu hao hapa nchini.
Watanzania tunatakiwa tuwatumie wazungu kwa faida yetu na siyo wao watutumie kwa faida yao.
Tatizo kubwa ni mtazamo,mwenendo na matendo hasi katika kutekeleza majukumu yanayohusiana na uwepo wa wazungu au wageni wengine hapa Tz.
Hata hivyo, ni muhimu tujue kwamba Tanzania yetu tutaijenga wenyewe, yeyote yule mwenye mawazo kwamba Tanzania itajengwa na wazungu au wageni wengine ni adui na msaliti wa watanzania na hafai katika karne hii.Huyo alitakiwa awepo enzi ya utumwa!!!

Mimi si-dispute facts zako. Inategemea unafanya kazi katika industry gani. Mimi nimesoma shule na wazungu wanaojiita watanzania. Ni watu wanaipenda Tanzania. Tumeenda kusoma nje wote na wengi wamerudi Tanzania kufanya kazi. Wengi wameenda huko maporini kabisa. Hawa ni watu wanaojiona kuwa Watanzania kwa asilimia 100. Ukimwondoa Tanzania hana pa kwenda.
Of course lazima nchi iendeshwe katika interest za wananchi na sio wazungu wawekezaji na ni wananchi wenyewe ndio wanaoweza kujenga. But be careful jinsi gani una-define mwananchi.

Msando,hii isue ni very complex.Na ndiyo maana ninaamini kuwa wakulaumiwa ni both viongozi na wale wa nje wenye nia ya kutunyonya in any means neccessary.
Sisi huwa na tatizo moja kubwa,ambalo ni ku concentrate pale tulipoangukia badala ya pale tulipojikwaa.Misingi tuliyojiwekea toka mwanzo tulipopata uhuru ndiyo imetufikisha hapa tulipo.
Ndiyo ni kweli kwamba tatizo ni viongozi wetu.Hata hivyo bado ni kweli kwamba ni lazima wawasikilize hao "Bwana wakubwa"Wako under control,ni kama wanawafanyia kazi hao wazungu na si wananchi waliowachagua.Chaguzi zimekuwa kama viini macho.Kwani silaha za kujilinda dhidi ya wananchi hata kama wakitetea maslahi ya wazungu ie wawekezaji si wanapewa na wazungu hao hao?
Labda sijaelewa,if so nieleweshe.
Ninavyoelewa mimi ni kwamba nchi inapokwenda,lazima hao wawekezaji,wafadhili nk wawe na say.Mabadiliko yote tuliyoyafanya kwa shinikizo la world bank na IMF kuanzia mwalimu alipo ng'atuka sisi kama wananchi tulikuwa na say?Si mzungu alituamulia?Na mwalimu kwa kujua kuwa power yake ina limit pale inapokuja kwenye maamuzi ya hao wazungu,aliamuwa kuachia ngazi badala ya kula matapishi yake.Ni wazi bado hatujapata uhuru wa kweli.Hi mikataba wanayoingia hawa chief mangungos wetu ambayo tunaipigia kelele unadhani wanaijali?Unadhani kina Geita gold mining wanajali kuwa kuna poisonous materials inayowa athiri wananchi wakati wa operations zao?Bado wana nguvu zadi na bado wao ndiyo wanatutawala.Viongozi wetu ni manyapara tu ambao wanatumia fursa kujinufaisha.
Tuendelee na mjadala.

Ivi China iliendelea kwa kutegemea say ya watu wa nje? Kwa nini tunashindwa kuiga model yao ya development? Tatizo ni simple, we have failed ourselves. Tukisoma hatutaki kurudi nyumbani. Waliosoma bongo wamegeuka kuwa wezi. Huwezi kuamini Chenge na Obama ni Harvard alumni. Lakini angalia utendaji wao katika nchi zao. Wachumi tunao, lakini ndio hao kina Lipumba wanaong'ng'ania urais utadhani ni mbinguni! We have failed ourselves and have no one to blame....NO ONE!

Mambo ya kudai wazungu ni wanyonyaji ni UONGO. Kila mtu ni mnyonyaji. We have to represent our interest. Kama hatuwezi kuchimba dhahabu, tufunge migodi. Shida ipo wapi? Kwani bila hiyo dhahabu leo hatuwezi kuishi? Engineers waliomaliza hapo UD wako wapi wasitengeneze mitambo na mashine za kusafisha dhahabu hapa kwetu? Kuna siku nili-argue na mnaigeria mmoja kuwa Africa was not ready for independence. Karibia tupigane. That is what i sincerely believe. Waliokuwa tayari ni wachache mno, na wengi walikuwa wajinga (ignorant) na bado wajinga. Kumbuka speech ya Nyerere...adui wa taifa ni ujinga, umaskini na maradhi. Lakini alifanya nini kuondoa huo ujinga? Kwa maoni yangu, kushindwa kuondoa ujinga ndio sababu leo tumeshindwa kupiga hatua. Na ndio maana ccm imebaki madakarani na kuua nchi yetu. Ujinga kila kona!

Tatizo la Tanzania ni ccm, na daima nitaichukia ccm.

Mkuu soma historia vyema,unadhani ilikuwa bahati mbaya kwamba chini ya mkoloni kulikuwa na wasomi wachache sana?Je hujui kuwa rasilimali zilikuwa zinabebwa na wala hakuna proccessing industry?Tunategemea misaada ya masharti yake mengi ni wao wanapanga wapi iwe allocated.Unadhani wanataka tuendelee?

Umezungumzia China?Wao wana historia tofauti sana na ya kwetu.Historia ya mwafrika ni unique.Mzungu kabla hajamvamia mchina atafiikiria mara mbili mbili.Ila kukavamia kanchi ka Afrika ni just in a wink of an eye.

Mfumo wa kikoloni bado upo pale pale.Mfano ni wazimbabwe.Nawalaumu wazungu pamoja na viongozi wetu wakoloni weusi ambao ni puppets wao.Kwa taarifa yako siwalaumu wazungu individually,but collectivelly from their leaders.Sina maana kuwa nina chuki na wazungu na kwamba sitaki waishi na wafrika side to side peacefully and with harmony.Dont get it twisted.

Waafrika waliosomeshwa kabla ya uhuru walikuwa ni wachache wale vibaraka wao ambao walitumika kuwa contain wananchi ili watawaliwe vizuri kwa kuwa walipewa tuheshima flani na maisha bora huku wakiwa brainwashed.Same thing happens nowdays,same ol shit just a different day!Na wengi wao ndo walioachiwa madaraka baada ya uhuru.Kwahiyo mwelekeo wa Afrika ukawa ni ukoloni mambo leo AKA neo colonialism.

Ndio maana viongozi ambao walienda tofauti kama Mwalimu Nyerere wali fail.Ndiyo nikakupa mfano wa masharti ya World Bank na IMF ambayo mwalimu alikuwa akiyapinga sana tu na hata ikabidi ang'atuke.Hakuna sera za kibepari ambazo mwalimu aliamini zitauondoa umasikini kutokana na hali ilivyokuwa kwenye taifa letu ie wengi wakiwa hawana elimu.Hakuna uzalishaji na mala ghafi zinakuwa shipped out of the country to be proccessed else where,na hivyo uchumi mbovu hence everthing mbovu kama elimu,socia services,miundo mbinu nk.

Mkuu issue hii inatakiwa kufikiri kwa marefu na mapana haswa.Viongozi waliojitolea unajuwa walifika wapi?Kina
Lumumba?Unajuwa nani alimwua Kwame Nkrumah na ni kwanini?Do your research.

Nimefuatilia michango ya wabunge kwa makini. Jambo moja kubwa limejitokeza, wazungu wanaonekana kuwa ni chanzo cha matatizo yetu mengi!

Wapo ambao wanaosema tuwafukuze, wengine wana wakebehi na kuwatukana. Wengine wanasema ni lazima tufanye nao kazi na hatuwezi kufanikiwa bila wao. Kuna shule mbili au tatu za mawazo;

1. Wazungu ni wakoloni na hawatufai. Wanatunyonya. Waondoke.

2. Wazungu wanatufaa na ni watu rafiki. Tusiwafukuze. Bila wao hatuwezi.

3. Wazungu ni wanyonyaji lakini wanatufaa. Tukae nao tujifunze tukiweza waondoke!

Inawezekana kuna shule nyingine za mawazo zaidi ya nilizotaja.

Suala hili linahitaji mjadala. Si CCM wala Chadema inaonekana wanachama wake wanakubaliana kuhusu hili. Utasikia waziri anasema hivi mbunge anasema vile. Waziri kivuli anasema hivi mbunge wa upinzani anasema lake.

Sifa, umaarufu, ujinga, kura, upumbavu vinaweza kuwa sababu ya mkanganyiko huo wa fikra. Ilani na sera za vyama vinasahaulika kwa urahisi pale mtu anapokuwa ameruhusiwa kuchangia. Jazba na uzalendo wa kinafiki vinakuwa ni msukumo wa kusema badala ya kuzungumza!! Na mimi nisikike wapiga kura wanisifie!

Naamini hapa JF suala hili litazungumzwa kwa upana na urefu wake. Nakaribisha michango yenu wafikiriaji wakuu!
4. Wazungu ni wakoloni hawatufai, wanatunyonya, lakini hatuwawezi bora kujiunga nao kuliko kushindana nao...

just imagine , nyerere alikuwa ana mipando mathubuti ya kulipa direction taifa na afrika kwa ujumla ila shangaa kwamba alifanikiwa kidogo sana na hatimaye alishindwa kabisa, baada ya kudai eti anataka kupumzika kumbe mambo yalishamzidi kutokana na presure za world bank na IMF.

Kiukweli wajamaaa wana mbinu fulani za kuturudisha nyuma ama kutudumaza kama ilivyosilika ya binadam yeyote yule, ila kikubwa ni kwamba sisi wenyewe hatupo organized kwa malengo mahsus ya taifa. MWISHO KABISA INAONEKANA WATU WEUSI WENGI WAO WANA LAANA YA KUTOKUWA WAZALENDO, sijui tumeipata wapi hii kitu-hapo ndo chanzo. Umeona wapi kiongozi anganganie madaraka kwa maslai yake mwenyewe na akubali et kuiuza nchi kwa kuwa puppet leader kwa kumnufaisha mzungu ,kama sio laana hii.

Ni bora kuwa kama wamarekani wenye NATION INTEREST KWANZA.

Nimefuatilia michango ya wabunge kwa makini. Jambo moja kubwa limejitokeza, wazungu wanaonekana kuwa ni chanzo cha matatizo yetu mengi!

Wapo ambao wanaosema tuwafukuze, wengine wana wakebehi na kuwatukana. Wengine wanasema ni lazima tufanye nao kazi na hatuwezi kufanikiwa bila wao. Kuna shule mbili au tatu za mawazo;

1. Wazungu ni wakoloni na hawatufai. Wanatunyonya. Waondoke.

2. Wazungu wanatufaa na ni watu rafiki. Tusiwafukuze. Bila wao hatuwezi.

3. Wazungu ni wanyonyaji lakini wanatufaa. Tukae nao tujifunze tukiweza waondoke!

Inawezekana kuna shule nyingine za mawazo zaidi ya nilizotaja.

Suala hili linahitaji mjadala. Si CCM wala Chadema inaonekana wanachama wake wanakubaliana kuhusu hili. Utasikia waziri anasema hivi mbunge anasema vile. Waziri kivuli anasema hivi mbunge wa upinzani anasema lake.

Sifa, umaarufu, ujinga, kura, upumbavu vinaweza kuwa sababu ya mkanganyiko huo wa fikra. Ilani na sera za vyama vinasahaulika kwa urahisi pale mtu anapokuwa ameruhusiwa kuchangia. Jazba na uzalendo wa kinafiki vinakuwa ni msukumo wa kusema badala ya kuzungumza!! Na mimi nisikike wapiga kura wanisifie!

Naamini hapa JF suala hili litazungumzwa kwa upana na urefu wake. Nakaribisha michango yenu wafikiriaji wakuu!

Alberto !! Alberto!!
Wewe ni mwanasheria kwa maana hiyo sii mvivu wa kusoma vitabu. tafadhali saana kwa heshima na taadhima tafuta kitabu cha "The Capitalist Nigger" by Chika Onyeani (kipo mtandaoni: Capitalist Nigger - A self published book prepared by Five Corners Press) tafadhali soma then nafikiri utakuja na mawazo tofauti kabisa.

Sioni tatizo la wazungu, wachina, wahindi, na waarabu tatizo kubwa ni mfumo wetu unaotuongoza, tukiangalia kwa upeo mdogo tunaweza kuwa MAKABURU weusi tatizo ni mfumo uliopo ndiyo hautoi haki sawa kwa watu walionacho na wasionacho, weupe na weusi. Kingine ni Inferiority ya watu wengi weusi dhidi ya weupe

Lazima tutambue hata sisi wenyewe tunadharauliana wenyewe kwa wenyewe. Wazungu hawatudharau ila viongozi wetu wanaendesha hii nchi kama dampo bila sheria. Mzungu ni mtu anapenda kuishi kwa kulenga maisha ya mbele lakini sisi tunawaza kupata hapo hapo na kushiba leo basi. Lazima watanzania tuamke tuendane na dunia ya sasa hasa watendaji wanapopewa majukumu ya kuijenga hili taifa.

Wataacha kutudharau kama tutabadilisha makazi yetu na kufuata sheria zinazomnufaisha mtu sio hizi sheria za kishikaji. Serikali ijitahidi sana kutafuta mbinu ya kuwaweka watanzania wa leo kujisomea zaidi kuelewa hii dunia inavyokwenda. Hapa ninalenga %kubwa ya watanzania hawajui kiingereza vitafutwe vitabu film muhimu wavitafsiri ili watanzania wabadilike.

Back
Top Bottom