gmosha48
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 2,399
- 1,478
Kama hujui historia,then achana na siasa.Inaonekana wengi humu kwenye jukwaa la siasa hawajui history na how imeshape the current world.
Mitazamo hii ndo inayoendelea kutudumaza siku hadi siku. Kwani mataifa mengine hayakuwa na Historia? Mbona yamefanikiwa kuendelea pamoja na hizo historia zao? Je unafahamu kwamba kwa kutumia vigezo mbalimbali vya maendeleo ( mfano pato la taifa, huduma mbali mbali za jamii- elimu an afya, nk) Tanzania haikuwa mbali sana ukilinganisha na mataifa mengi ya Asia kama Malasia, Thailand, Indonesia nk. Leo mataifa hayo yameendelea sana wakati sisi tunaendelea kushadadia majibu mepesi ya HISTORIA yetu. Kweli historia inachangia kutufanya jisnsi tulivyo, lakini hilo lina ukomo. Kinachotakiwa sasa ni sisi wenyewe kuhakikisha kwamba tunaweka mifumo itakayotuwezesha kushiriki kikamilifu katika utandawazi kwa maslahi ya Taifa. Tusifikiri kwamba kuna mzungu atakuja kufanya biashara hapa kwa lengo la kutuendeleza. Tukilemaa watafanya biashara, watachuma na kutuacha patupu( hicho ndicho kinachotokea kwenye sekta ya madini na Utalii). Tukijipanga, watafanya biashara na sisi tutavuna stahili yetu. Kama wengine wamewez, kwa nini sisi tushindwe?