Fikra: Wazungu na Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fikra: Wazungu na Tanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Aug 18, 2011.

1. M

MsandoAlberto JF-Expert Member

#1
Aug 18, 2011
Joined: Nov 2, 2010
Messages: 1,019
Likes Received: 2
Trophy Points: 0
Nimefuatilia michango ya wabunge kwa makini. Jambo moja kubwa limejitokeza, wazungu wanaonekana kuwa ni chanzo cha matatizo yetu mengi!

Wapo ambao wanaosema tuwafukuze, wengine wana wakebehi na kuwatukana. Wengine wanasema ni lazima tufanye nao kazi na hatuwezi kufanikiwa bila wao. Kuna shule mbili au tatu za mawazo;

1. Wazungu ni wakoloni na hawatufai. Wanatunyonya. Waondoke.

2. Wazungu wanatufaa na ni watu rafiki. Tusiwafukuze. Bila wao hatuwezi.

3. Wazungu ni wanyonyaji lakini wanatufaa. Tukae nao tujifunze tukiweza waondoke!

Inawezekana kuna shule nyingine za mawazo zaidi ya nilizotaja.

Suala hili linahitaji mjadala. Si CCM wala Chadema inaonekana wanachama wake wanakubaliana kuhusu hili. Utasikia waziri anasema hivi mbunge anasema vile. Waziri kivuli anasema hivi mbunge wa upinzani anasema lake.

Sifa, umaarufu, ujinga, kura, upumbavu vinaweza kuwa sababu ya mkanganyiko huo wa fikra. Ilani na sera za vyama vinasahaulika kwa urahisi pale mtu anapokuwa ameruhusiwa kuchangia. Jazba na uzalendo wa kinafiki vinakuwa ni msukumo wa kusema badala ya kuzungumza!! Na mimi nisikike wapiga kura wanisifie!

Naamini hapa JF suala hili litazungumzwa kwa upana na urefu wake. Nakaribisha michango yenu wafikiriaji wakuu!

2. Bishop Hiluka

Bishop Hiluka Verified User

#2
Aug 18, 2011
Joined: Aug 12, 2011
Messages: 4,100
Likes Received: 1,424
Trophy Points: 280
I doubt kama kweli serikali hii ni sikivu,
anyway nitarudi baadaye kuchangia
maybe this time watasikia!

3. afrodenzi

afrodenzi Platinum Member

#3
Aug 18, 2011
Joined: Nov 1, 2010
Messages: 18,135
Likes Received: 2,398
Trophy Points: 280
Wasije wakageuza nchi yetu kama
ilivyo Zimbabwe ...

4. Nyani Ngabu

Nyani Ngabu Platinum Member

#4
Aug 18, 2011
Joined: May 15, 2006
Messages: 73,651
Likes Received: 35,408
Trophy Points: 280
Wanaooanisha uzungu na matatizo yetu wao ndiyo wana matatizo. Wana matatizo ya chuki. Chuki hizo ziko kwenye misingi ya rangi ya ngozi ya mtu.

Sasa hayo ni maono mafupi na mabaya sana kwa sababu ni ya kibaguzi. Matatizo tuliyonayo hayana uhusiano wa moja kwa moja na rangi ya ngozi ya mtu. Matatizo yetu mengi na kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na uongozi mbovu usiowajibika na usiojua kuwajibisha.

Sishangai kwa nini baadhi ya watu wawalaumu wazungu. Hii ni njia ya kuepa lawama na kuepa uwajibikaji ambayo imetumika sehemu nyingi duniani. Ni rahisi sana kwa mtu kumnyooshea mtu mwingine kidole cha tuhuma za ubaguzi kuliko kujiangalia mwenyewe na kuwajibika.

Tatizo la Tanzania siyo wazungu. Tatizo la Tanzania ni uongozi mbovu usio na sera bora, ubunifu, na usiofuata utawala wa sheria.

5. jmushi1

jmushi1 JF-Expert Member

#5
Aug 18, 2011
Joined: Nov 2, 2007
Messages: 17,552
Likes Received: 1,896
Trophy Points: 280
Nakubaliana kuhusu lack of leadership,however kama huna insight ya the other side of the coin,then just chill out usome maoni ya wengine.Si lazima uchangie evrything.

6. Nyani Ngabu

Nyani Ngabu Platinum Member

#6
Aug 18, 2011
Joined: May 15, 2006
Messages: 73,651
Likes Received: 35,408
Trophy Points: 280
And what is that other side of the coin Mr. Meku?

7. Chapakazi

Chapakazi JF-Expert Member

#7
Aug 18, 2011
Joined: Apr 19, 2009
Messages: 2,881
Likes Received: 8
Trophy Points: 135
Nakubaliana na wewe asilimia 100. Siku zote wajinga wanatafuta scapegoat. Hitler alisingizia Jews, sisi tunasingizia wazungu. Mzungu ndio anakulazimisha ununue gari la waziri kwa mil 300? mzungu ndio anakufanya ujenge shule za kata zisizo na walimu? mzungu ndio amemgeuza rais wenu kuwa vasco da gama?
Kuna wazungu wanaipenda tanzania kwa moyo wao wote na kuna wanyonyaji, just like the case with our leaders...mfano; Slaa na lowassa, Mbowe na kikwete, huku tusimsahau mkapa....

8. makwimoge

makwimoge JF-Expert Member

#8
Aug 18, 2011
Joined: Apr 14, 2011
Messages: 294
Likes Received: 1
Trophy Points: 35
Uzungu au uarabu sio tatizio,tatizo ni akili mbovu za serikari legelege

9. M

MsandoAlberto JF-Expert Member

#9
Aug 18, 2011
Joined: Nov 2, 2010
Messages: 1,019
Likes Received: 2
Trophy Points: 0

Tutafanya majumuisho kwa pamoja. Tuendelee kusikilizana!

10. Chapakazi

Chapakazi JF-Expert Member

#10
Aug 18, 2011
Joined: Apr 19, 2009
Messages: 2,881
Likes Received: 8
Trophy Points: 135
nani kafanya majumuisho? mie nimetoa opinion yangu....

11. jmushi1

jmushi1 JF-Expert Member

#11
Aug 18, 2011
Joined: Nov 2, 2007
Messages: 17,552
Likes Received: 1,896
Trophy Points: 280
The other side is the one you dont have any insight on.Soma taratibu.Ama nyie ndo wale wa kata?

12. M

MsandoAlberto JF-Expert Member

#12
Aug 18, 2011
Joined: Nov 2, 2010
Messages: 1,019
Likes Received: 2
Trophy Points: 0

Chapakazi, nisamehe kwa kuandika statement. Nilichomaanisha ni kwamba baada ya kusikiliza wengine tutafanya majumuisho ya pamoja. Sikumaanisha kwamba umejumuisha ndugu yangu! My apologies!

13. Nyani Ngabu

Nyani Ngabu Platinum Member

#13
Aug 18, 2011
Joined: May 15, 2006
Messages: 73,651
Likes Received: 35,408
Trophy Points: 280
Wacha dharau Meku. Wee unadhani tuko kwenye kilabu cha mbege hapa? Eboooo!!! Haya jibu swali langu.

14. jmushi1

jmushi1 JF-Expert Member

#14
Aug 18, 2011
Joined: Nov 2, 2007
Messages: 17,552
Likes Received: 1,896
Trophy Points: 280
Ntaachaje kudharau makamasi?Swali gani?

15. Shine

Shine JF-Expert Member

#15
Aug 18, 2011
Joined: Feb 5, 2011
Messages: 11,514
Likes Received: 16
Trophy Points: 0

Kweli kabisa mkuu hapo umenena

16. Shine

Shine JF-Expert Member

#16
Aug 18, 2011
Joined: Feb 5, 2011
Messages: 11,514
Likes Received: 16
Trophy Points: 0
Sote tunaishi kwakutegemeana mzungu amtegemea mwafika na mwafrika amtegemea mzungu japo inatofautiana digree

17. jmushi1

jmushi1 JF-Expert Member

#17
Aug 18, 2011
Joined: Nov 2, 2007
Messages: 17,552
Likes Received: 1,896
Trophy Points: 280
Kama hujui historia,then achana na siasa.Inaonekana wengi humu kwenye jukwaa la siasa hawajui history na how imeshape the current world.

18. F

FJM JF-Expert Member

#18
Aug 18, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 8,088
Likes Received: 90
Trophy Points: 145
Ni nadra sana mtu akaja nyumbani kwako akawatwanga makonde mkeo, na watoto unless anajau kuwa akifanya hivyo hakuna chochote kitatokea! Hii dhana ya kuunganisha unyonyaji na RANGI ya ngozi is the wrong way to go. Sidhani kama hawa wazungu ni wavamizi kwa maana ya watu kwenda mahali bila kufuata taratibu husika. wanapataje visa? wanapoingia airport au kwenye mipaka mingine wanasema wanaenda wapi? Wanajuajue kwa mfano Merereni au Bulyanhulu kuna madini?

Tatizo kubwa ninaloona hapa ni ile dhana kwamba tunaweza ku-import solutions kwa matatizo yetu! Tukikubali kuwa sisi ndio wenye solution & anything else ni kuboresha juhudi zetu katika kukabiliana na matatizo yetu basi hata hawa 'wazungu' watapokelewa hivyo - 'supplement'.Kwa mfano, Mpanda wanawaalika wazungu kulima, hivi wananchi wa mpanda wakipewa hizo zana (matrekta, machine etc) na kukawa na 'technical support toka kwa hao wazungu (kama wanampanda wanahitaji technical support) watashindwa kulima hizo ekari? Ni kwa nini wakimbilie kumleta mzungu kabla ya kuwawezesha wanampanda?

Kwa mtazamo wangu watanzania (hasa walio kwenye maamuzi) ndio tatizo, wazungu ni mgongo wa walafi!

19. Nyani Ngabu

Nyani Ngabu Platinum Member

#19
Aug 18, 2011
Joined: May 15, 2006
Messages: 73,651
Likes Received: 35,408
Trophy Points: 280
Mpaka sasa hujaongea hoja yoyote ya maana zaidi ya ku dismiss tu.

20. jmushi1

jmushi1 JF-Expert Member

#20
Aug 18, 2011
Joined: Nov 2, 2007
Messages: 17,552
Likes Received: 1,896
Trophy Points: 280
Usipofanya wanavyotaka hao wazungu, wanakuondoa madarakani ama kuidhoofisha serikali yako.Mfano Gaddafi,Mugabe,lumumba,Nkrumah etc.Interest zao ni first.Hatujapata uhuru kamili.Nani alaumiwe?

Loading...