Fikiria leo hii Lowassa angekuwa Rais!

Fikiria leo hii Lowassa angekuwa Rais!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,838
Kama tungemchagua Lowassa kuwa Raisi wa wa 5 wa JMTZ unafikiri mpaka sasa hivi ni nini kingekuwa kimetokea? Unafikri wagonjwa Muhimbili wangetoka sakafuni na kuhamia kitandani? Unafikiri Lowassa, Mbowe Lisu &Co. wangeacha kutumia milioni 250 na badala yake kuzipeleka Hospitali kusaidia Watanzania? Rejea Tundu Lissu kutetea milioni karibia 300 walizokuwa walipwe kama Wabunge, je angeziacha hizi za juzi kama angekuwa na madaraka?

Unafikiri Lowasa na Mbowe wangeahirisha kuuza sura Disemba 9 na badala yake kutumia hizo fedha kwa ajili ya maendeleo?
Unafikiri Lowassa na Mbowe wangefuta safari za nje ya nchi?

Mke wa Lowassa unafikiri leo hii angekuwa kimya kama mama Janeti au tayari angeshaanzisha NGO na sia ajabu sasa hivi angekuwa yuko safari ndefu ya Marekani na Ulaya kuuza wazo lake?

Mungu bado hajachoka na sisi Watanzania anatupenda na ndiyo maana ametuongoza na tukafanya maamuzi ya busara, leo hii ukiwauliza waliompigia kura Dr. Pombe Magufuli kama wana majuto yoyote ya kufanya jibu lake ni HAPANA kubwa!
 
Hakika Mungu mkubwa, angekuwa ashajimilikisha Vitalu vyote vya gesi, Mengi angepewa kimoja kwa promo yake!
eti waziri wa mambo ya ndani angekuwa msindai!
 
Kwa Lowasa hiki anachofanya Magu ni cha mtoto. Tungelishuhudia mabadiliko ya kasi tena bila kutumia magufu kama anavyofanya Magu. Halafu lazma kuwa systematic, siyo kila kukicha unatoa jambo jipya bila kufanya analysis ya lile la jana ni kwa kiasi gani umefikia au kukaribia lengo.
 
Tena walikuwa wamekwisha kugawana uwaziri na ss hvi kwao ingalikuwa ni kupongezana tu, hakika maombi ya watz Mungu aliyasikia na kutupatia kiongozi ambaye kwa sasa watz tunaanza kupata matumaini mapya na hii serikali, cha msingi ni cc kuwafichua wala rushwa ili na yy apate hamasa ya utendaji wake.
 
Kwa Lowasa hiki anachofanya Magu ni cha mtoto. Tungelishuhudia mabadiliko ya kasi tena bila kutumia magufu kama anavyofanya Magu. Halafu lazma kuwa systematic, siyo kila kukicha unatoa jambo jipya bila kufanya analysis ya lile la jana ni kwa kiasi gani umefikia au kukaribia lengo kama Magu anavyofanya.

Lowasa asingekuwa na jipya tofauti na kupongezana kwa kazi kubwa ya kuchakachua kura na kugawana wizara na mipango ya kwenda kujitambulisha nchi za nje, fisadi hana huruma, na Lowasa hakuwahi kuwa na huruma na hakuna siku atakuwa na huruma kwa watz, na ndo maana kura zake hazikutosha, ss wameanza siasa kwa kutumia kifo cha Mawazo. Watz wameshachoka na UKAWA kwa sasa, kwani wamepata Raisi bora na si bora Raisi.
 
Ww mleta acha kutibua watu SAA hiz, mafisadi mmjezana hapo Lumumba , lowasa angekuwa rais kuanzia vijinin wangeshaanza kupata huduma bora za afya, na mwakan hakuna mwanafunz angeagizwa mchango, na angeshakomoesha mgao wa umeme tungeanza kufurahia umeme wa gesi
 
Back
Top Bottom