Fikiri kabla ya kutenda.

Fikiri kabla ya kutenda.

Senior Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2011
Posts
3,405
Reaction score
3,701
Mzee mmoja alianza hofia kuwa yawezekana mkewe kaanza matatizo ya kutosikia vizuri.Hivyo ikambidi amtafute daktari wa familia na kumsimulia mkasa mzima.
Baada ya daktari kumsikiliza yule mme vizuri, akamwambia kuwa sasa atahitaji akirudi nyumbani amfanyie jaribio moja mkewe ili majibu yake yaweze kumpa dokta mwanga wa kumsaidia kulitambua tatatizo na yule mama apone.
Daktari akamwambia, " ukirudi nyumbani simama futi 40 kutoka kwa mkeo na kwa sauti ya mazungumzo ya kawaida ongea neno ili uone kama atasikia na kama hatasikia simama karibu futi 30 ukimsogela , kama hatishoshi ongeza zaidi futi 20 mpaka atakapo kusikia"
Jioni yake mzee akiwa sebuleni na mama akiwa jikoni anaandaa chakula cha jioni, baba akiwa sebuleni akamwita mkewe na kuuliza, "Mpenzi tuna kula nini leo jioni?" lakini mke hakujibu.
Mzee akazidi kusogea futi 30 karibu akamuuliza tena, "Mpenzi tuna kula nini leo jioni?" lakini pia mke hakujibu, mzee akasogea tena futi 20 karibu na jikoni na kumuuliza tena, "Mpenzi tuna kula nini leo jioni?" mara hii mke hakujibu tena.
Basi ikambidi yule mzee amsogelee mpaka karibu yake na kumkumbatia mgongoni huku akimuuliza tena "Mpenzi tuna kula nini leo jioni?" mkewe akamjibu," mme wangu nimepika kuku" mbona nimekujibu tangu uko sebuleni ina maana hukunisikia?
Mzee yeye alidhani mkewe ndio mwenye tatizo la kutomsikia mtu akiwa mbali yake kumbe yeye mzee ndio mwenye tatizo la kutosikia mtu akiwa mbali.
Ndio ilivyo katika Maisha yetu ya kila siku, tunaweza tukafikiri kuwa wenzetu ndio wenye matatizo zaidi lakini kumbe sisi ndio wenye matatizo zaidi.
Pia ni vyema kutokuwa wepesi wa kuhukumu au kueneza jambo lolote tunaloliona kuwa ni baya bila ya kuangalia sisi tupo upande gani katika uvumi huo.
Ni rahisi kufikiri unawaharibia watu kumbe unajiharibia.
 
Mh! kweli kabisa! Nimejifunza kitu! Somo zuri ! Big up!!
 
ni sahihi kabisa. Ona boriti ndani ya jcho lako kabla ya kukiona kibanzi ndani ya jcho la mwenzako.
 
Somo zuri sana . Nimechukua point
 
safi sana somo zuri rahisi nanimeelewa!kama tungekuwa tunapost thread za namna hiyi basi MMU ingekuwa jukwaa bora sana maana siku hizi tumechoka na thread za kina papuchi na nduguye mdedego ambazo hazina mantiki yeyote zaidi ya kudhalilishana jinsia zetu
 
........
Ndio ilivyo katika Maisha yetu ya kila siku, tunaweza tukafikiri kuwa wenzetu ndio wenye matatizo zaidi lakini kumbe sisi ndio wenye matatizo zaidi.
Pia ni vyema kutokuwa wepesi wa kuhukumu au kueneza jambo lolote tunaloliona kuwa ni baya bila ya kuangalia sisi tupo upande gani katika uvumi huo.
Ni rahisi kufikiri unawaharibia watu kumbe unajiharibia.

Nimepata kitu cha tofauti kwenye hii thread. Ubarikiwe

Naomba nisindikizie hili somo na hichi kibao cha Lucky Dube,

Lucky Dube - Shut Up Lyrics
Don't close the door behind you
You might wanna go through it someday
Don't burn that bridge
You might wanna cross it someday
Your best friends today
Could be your worst enemies to morrow
Your worst enemies today
Could be your best friends tomorrow
Don't burn the bridge
Don't cross the door

Chorus
And if you can't say something good about somebody
Oh shut up
And if you can't say something about somebody
Just shut up.

Don't say those words that will hurt people
Don't do those things that will hurt people
The things you say today
Will come and haunt you tomorrow
The things you do today
Will come and haunt you tomorrow
Do unto others as you would like them do unto you

And if you can't say something good about somebody
Oh shut up
And if you can't say something good about somebody
Just shut up
 
Back
Top Bottom