Fiesta na wasanii wenye njaa

Fiesta na wasanii wenye njaa

pinno

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2013
Posts
1,213
Reaction score
1,233
Kuna Tangazo linapiga sana wiki hii, Clauds fm, likitangaza Tamasha la Fiesta Musoma na Mwanza

Manzoni wakati nasikiliza hili tangazo la Tigo Fiesta 2018 Musoma na mwanza, niliposikia mtangazaji anasema tamasha hilo litapambwa na madj wakali, na wasanii wenye njaa

Sikujiuliza sana sababu nilijua "Njaa " ni neno mbadala kwa ari, hivyo nikagundua wanamaanisha wasanii wenye ari na kiu ya mafanikio na kiu ya kupagawisha mashabiki.

Lakini ghafla nikajikuta napitia majina Ya A list artist wa Bongo sasa hivi na ambao wametoa ngoma kali kwa mwaka huu. Nikagundua majina mengi hayapo, na ukiangalia hawa ni wasanii ambao kwa definition ya njaa kama ari, wana ari kweli.

Ndipo nika hitimisha kuwa hawa jamaa zangu wamechukua wasanii wenye NJAA Ya kabisa kabisa, yaani hii njaa hii mbaya ambayo inaweza ikamfanya simba Ale nyasi, ndo type ya wasanii walio wasajili.

Wasanii hawa wenye njaa wengi ni wale ambao wanaihitaji fiesta kuliko fiesta inavyowahitaj wao.

Sio kwamba ni wachovu, au sio wakali hapana, kuna kichwa kama Whozu, ni bonge la artist mwenye very bright future, lakini sote tunajua Whozu anaihitaj fiesta ili imsaidie kumkuzia brand yake mikoani, hivyo atakuwa tayar hata kupokea malipo kiduchu.

Fid yupo kwenye list, ni msanii ambae hana show nyingi, japo ni mkali, so bado unakuja pale pale

Rostam wameshazunguka majukwaa kadhaa nao ndo vile, wana ishi kwa mziki, wana familia ,sio watu ambao mnaweza mkabishana bei sababu ya njaa.

So ukiangali list ya Top Artist Bongo hapa, chukua data youtube, chukua data google, chukua data kokote, kwa sasa kuna majina kama Vannesa mdee, Navy kenzo,Ney wa mitego ,Aslay,Kiba Diamond na madogo zake akina Hamonize, Rayvan, Mboso na lavalava pia kuna wakongwe kama Duly sykes, Prof jize, weusi na chipukiz akina Marioo,Nandy na Maua sama . Hii ndo state of the art kwa sasa, kama nimesahu jina basi ni moja au mawili

Lakini ukiangalia hapo msajili wa Fiesta kachuja yale majina ambayo ni cheap, na ambayo yana njaa, Sio Vannesa, sio navy kenzo, Ney wa mitego sio kiba wala msanii wa wcb yeyote alie tokea had sasa kwenye Jukwaa la fiesta.

Reason ni kuwa wanapeleka wasanii wenye njaaa mikoani ili kumaximize profit

Ikifika Dar kidogo ndo watajichanga labda wazame deep into pockets watuletee akina Vanesa, kiba etc ambao watawagharimu kias ila had sasa wanatembea na wasanii wenye njaa

Imagine Ney wa mitego, Aslay, Navy Kenzo, Vanessa ,wote hawa hawana beef linalotambulika kama ilivyo kwa wasanii wa WCB, lakin nao pia hawapo? Je kigezo hapa sio njaa kweli?

Na kama jamaa basi tuseme wana beef na 80%ya A list artists, tutajiuliza kwa nini?


Kinachouma sio wao kufanya mbinu hii ili wamaximize profits

Kinachouma ni Wao kufunguka na kusema kabisa kwenye jingle kuwa Tunaleta WASANII WENYE NJAA

Huko ni kuwananga wasanii wenyewe lakini pia ni kejeli fulani kwa mashabiki

Lakini ni swali ,hivi ndivyo tunavyokuza sanaa?

Ni lini wataacha kutumia wasanii wenye njaa??
 
naona hawajakuelewa, tembeza uzi mwenyewe.
 
Wataacha endapo wasanii wenyewe wataacha kukubali hali ya kuchukuliwa kinjaanjaa
 
Wasanii wakijitambua Wataweza kujisimamia na kujielewa na wasipoenda kwenye Show na kupata pesa,.....WATAKUFA
 
nadhani hiyo A list ilishaperform ILAM tour kama mnakumbuka vizuri. kwa hyo wakija dsm labda watapanda stejini
 
Andaa tamasha lako na wewe uwaite hao A list wako...jux,weusi,rostam,nandy,aslay,fid q hawa sio A list??
 
Mondo hawawezi kumchuka wanampango wakumuua kimziki clouds wabinafsi wazindaki wanagubu kwakifuoi hawafai
 
inshort ni kwamba Waandaji wa TAMASHA wamefilisika "... ila hawawezi kusema tu
 
Huu uandishi wako wa kuweka vifunga/vifungua semi bila sababu huwa unanistaajabisha sana😀😀
wewe deal na mambo yako tu mkuu " madam sivunji sheria za JF hayo mengine haya kuhusu " Au nina kula kwenu nini !!?
 
Back
Top Bottom