Fiesta 2016 Dar imebumaaaaaa

Fiesta 2016 Dar imebumaaaaaa

Sambusa kavu

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2015
Posts
811
Reaction score
1,311
Awali ya yote nikiri kabisa mi ni shabiki kindakindaki na mpenzi mkubwa mno wa burudani...nikiwa kama mpenda burudani ntakuwa mnafiki endapo sitasifia tamasha la fiesta linalofanyikaga kila mwaka nchini kwetu..

Mpaka sasa kwa mwaka huu tamasha hili limeshafanyika takribani mikoa mingi na sasa ni zamu ya Daresalaam ikiwa kama hitimisho...

Ila kwa mwaka huu Fiesta 2016 tamasha la Daresalaam naona kama limeshabuma kabla hata ya iyo jumamosi haijafika...nasema tena fiesta 2016 dar limebumaaaaaaaaa kwa sababu zifuatazo:

1.Tangu tamasha hili lianzishwe,ikifika kilele chake ambacho uwa ni show ya mwisho inayofanyika Dar lazima msanii mkubwa kutoka Marekani atue bongo...mwaka huuu HAKUNA!!!!!!!!tulitegemea labda mwaka huu tumuone Jay Z,Rihanna, Drake,Beyonce,au hata Chriss Brown basi (tena alifika mpaka mombasa hapo) lakini waaaaapi!!!!!
leo hii nitoe 20K nikamuangalie Tekno kweli??? huyu jamaa hapa Tz si ameshakuja kama mara 7 hivi....kwanza tekno hana utofauti na Nuhu mziwanda... Au yule Yemi Alade kwani ana tofauti gani na Shilole????!!! Fiesta Dar bila msanii wa Marekani imebumaaaaaaaa!!!!!!

2.Japo si makosa yao ila still naamini bado lilikuwa lipo ndani ya uwezo wao...yees ni Diamond Platinumz!!!! Inawezekana ikawa ni gundu la pili kwa Fiesta mwaka huu kumkosa huyu mtu pia!!!! hapa napo Fiesta 2016 imebumaaaaaaaaa!!!!!!(niishie hapahapa maana nikiandika sana hapa ntaonekana ni member wa timu fulani)

3.Wasanii wa Tz wooote waliosajiliwa nao ni jipu lingine!!!!!!! Hili ni kosa la wasanii wenyewe maana show zao zote ni very predictable...yaaan inajulikana kabisa msanii fulani ataingia na nyimbo gani atacheza vipi,ataweka vikolombwezo vipi na atamaliza na nyimbo ipi....hii ni mbaya sana maana mashabiki tunawachoka mapema wasanii hawa...Binafsi mwaka huu nimeshashiriki kwenye fiesta ya Mwanza,Shinyanga,Kahama,Bukoba na Dodoma..and trust me...yaaan ni kama copy and paste ya performance ya wasanii wote....walichofanya Mwanza ndicho icho walichofanya Kahama,ndicho icho icho walichofanya Dodoma,na ndicho icho icho walichofanya mikoa mingine na Dar pia watafanya icho icho.....Hapa napo imebumaaaaaaaaaaaa!!!!!

N.B. tunawatakia kila la kheri katika tamasha hili na naamini watu wa Dar wataenjoy pia bila msanii wa Marekani maana mziki wao pendwa wa Kisingeli utakuwepo.!!!!!!

Wasanii wa bongo wajifunze ubunifu hasa pale wanapopata show au tour za mikoa mbali mbali ...wasikariri kufanya show ya aina moja tuuu...nilitegemea Mr Blu alieperform mwanza awe tofauti kabisa Mr Blu alie perform Dodoma,na awe tofauti kabisa na Mr blu alieperform mikoa mingine na awe tofauti pia na Mr Blu atakaeperform Dar....(ila kwa sasa wasanii wetu wa bongo sahau icho kitu,ni kilekile tuuuuu....yaaaan inafahamika kabisa akitoka kuimba Darasa ndo atapanda Mr Blu...kama kasheria vileeee)
 
Kubuma ua kutobuma ni perception yako. bado ukweli unabakia kuwa Fiesta ndio tamasha kubwa zaidi la burudani nchi hii. Hili utalitambua kwa kiwango ushiriki wa wadhamini kwa kugombea kufadhili. Upande mwingine ni watu wanao matter kujalibu kujitanabahisha na Fiesta. Nina mashaka sana usahihi wa utabiri wako. Mwisho kuna tamasha gani lenye ujasiri wa kucharge kiingilio mpaka cha Sh. 25,000 hiyo ndio value ya show.
 
Diamond kutokuwepo Fiesta sio kosa la clouds lakin, Yeye amesaini mkataba na voda kufanya show ya fiesta ambayo inadhaminiwa na Tigo ni kukiuka mkataba
Hiv ina maana CLOUDS hilo hawakuliona mapema na wangeweza hata kukaa chin na Voda kuangalia namna nzur ya kumfanya jamaa aperfom
 
Naona povu lote hili kuja mtetea diamond hahahahahhahah[/QUOTE
Umeanza upuuzi sasa hapo kuna utetezi gani wa diamond labda... Au ndo umekuja na majibu yako ya mfukoni.. halaf eti unajichekelesha. Badilika mwanaume
 
Hiv ina maana CLOUDS hilo hawakuliona mapema na wangeweza hata kukaa chin na Voda kuangalia namna nzur ya kumfanya jamaa aperfom
mmh achana na ishu za mikataba ndugu yangu halafu hapo clouds hawawez fanya chochote Diamond ndio aliyejifunga na mkataba yan sio Fiesta tu ikitokea kuna tamasha lolote la mziki sponsor ikawa ni mtandao wowote wa simu imfano zantel , smart au airtel as long as mkataba wake na voda haujaisha hawez perform
 
Inaitwa Tigo fiesta,Diamond yupo na Vodacom kimkataba hawewzi kuharibu mkataba wake kwa issue ya siku moja.
Ingekua bado ni Serengeti Fiesta angeweza kutumbuiza maana beer na simu ni bidhaa mbili tofauti
 
Kubuma ua kutobuma ni perception yako. bado ukweli unabakia kuwa Fiesta ndio tamasha kubwa zaidi la burudani nchi hii. Hili utalitambua kwa kiwango ushiriki wa wadhamini kwa kugombea kufadhili. Upande mwingine ni watu wanao matter kujalibu kujitanabahisha na Fiesta. Nina mashaka sana usahihi wa utabiri wako. Mwisho kuna tamasha gani lenye ujasiri wa kucharge kiingilio mpaka cha Sh. 25,000 hiyo ndio value ya show.
Rejea mistari yangu miwili ya mwanzo kabisa.. Usipoelewa na hapo basi tena hakuna namna
 
mmh achana na ishu za mikataba ndugu yangu halafu hapo clouds hawawez fanya chochote Diamond ndio aliyejifunga na mkataba yan sio Fiesta tu ikitokea kuna tamasha lolote la mziki sponsor ikawa ni mtandao wowote wa simu imfano zantel , smart au airtel as long as mkataba wake na voda haujaisha hawez perform
 
Naona povu lote hili kuja mtetea diamond hahahahahhahah
Hamna povu hapo na wala uyo uliemtaja sina interest nae... Ndomana nimehudhuria tamasha hili over 4regions so far.. We leta ushabiki ila CMG wenyewe wanajua ukweli kama mwaka huu kumkosa big artist imebuma au laah
 
Hiv ina maana CLOUDS hilo hawakuliona mapema na wangeweza hata kukaa chin na Voda kuangalia namna nzur ya kumfanya jamaa aperfom
Kama unaiangalia Tanzania ya wakazi million 50 kwa upeo huu, jichunguze mara mbili mbili kijana!
 
N.B. tunawatakia kila la kheri katika tamasha hili na naamini watu wa Dar wataenjoy pia bila msanii wa Marekani maana mziki wao pendwa wa Kisingeli utakuwepo.!!!!!!

Sasa imebuma vipi mkuu na unasema mziki pendwa Dar utakuwepo?
 
Sasa imebuma vipi mkuu na unasema mziki pendwa Dar utakuwepo?
Fiesta ya dar watu wengi sana uwa wanatoka mikoani kuja kumuona msanii mkubwa wa marekani... Mwaka huu sidhani kama kuna mtu atafunga safari kuja dar kumuona shilole tu wakati tayar alishamuona kipind tamasha ilo lipo mikoani... Na iyo 20k kwa usawa huu wa uncle Magu mmmmh... Nahisi imeshabumaaa
 
Kwa usawa huu nani wa kutoa elf 25 kuangalia uji.nga wa Fiesta.... 25 ni cement mifuko 2
 
Fiesta ya dar watu wengi sana uwa wanatoka mikoani kuja kumuona msanii mkubwa wa marekani... Mwaka huu sidhani kama kuna mtu atafunga safari kuja dar kumuona shilole tu wakati tayar alishamuona kipind tamasha ilo lipo mikoani... Na iyo 20k kwa usawa huu wa uncle Magu mmmmh... Nahisi imeshabumaaa

Mkuu kama ukipata nafasi ya kuziona picha za watakaoingia uwanjani utashangaa sana, mimi siyo member lakini nina uhakika watajaza kama kawaida.
 
Back
Top Bottom