client
JF-Expert Member
- Dec 13, 2015
- 671
- 884
Mnamo mwaka 1959, Fidel Castro aliondoka mjini Santiago de Cuba kwa msafara mrefu wa magari kuelekea Havana. Karibu miaka 60 baadae, mabaki yake yamebebwa kupitia njia ile ile, kwa kurudi nyuma.
Hiba ambayo itaendelea kubaki ya kiongozi huyo ni kama ile ya Daudi na Goliati wa kwenye biblia. Alikuwa kijana, mwanamapinduzi mwenye ndevu nyingi kutoka katika kisiwa kidogo ambaye alipambana na ukubwa wa ubepari na nguvu ya Marekani.
Hilo ni suala la ndotoni. Lakini si ndoto ya kila mtu. Na, kwa kweli, sio kila mtu anaweza kukubali kwamba Fidel alikuwa ni Daudi au Goliathi.
Picha ya utawala wa Castro kuwa kama Daudi ilianza kuonekana wakati wa uvamizi wa Wacuba waishio nje ya nchi hiyo wakifadhiliwa na Marekani mwaka 1961 katika kile kilichokuja kujulikana kama Bay of Pigs. Picha hii ilionekana tena na tena wakati Fidel alipokuwa akirusha mawe na maneno dhidi ya jirani yake, taifa kubwa la Marekani huku akiungwa mkono na mshirika wake wa karibu Urusi na baadae Venezuela.
Na ni picha ambayo baadhi ya Wacuba – wale ambao walivutiwa na mvuto pamoja na uwezo wake wa kuzungumza ambao aliutumia kuonyesha kwamba kuteseka kwa sasa ni muhimu kama kianzio cha kupata maisha bora baadae – waliyaamini, angalau kwa muda huo. Hilo lilikuwa zaidi kwa wale ambao walifaidika na maendeleo ya awali ya mapinduzi na walioishi katika Cuba ya maendeleo ya raia.
Wacuba waliopigana dhidi ya udikteta wa Fulgencia Batista katika miaka ya 1950 na walihatarisha maisha yao katika vita hiyo, waliendelea kutetea mapinduzi hayo. Waliishi katika furaha wakati dikteta huyo alipoangushwa na waliendelea kumfuata Fidel.
Kwa wale wengi waliofaidika kutoka kwenye upanuzi wa elimu na huduma za afya ya umma, Castro aliendelea kuwa mtu anayeheshimika. Na maendeleo haya hayawezi kusahaulika, kwa sababu yalikuwa ni matunda ya kujitoa ambako Wacuba walikuwa wakifanya kila siku.
Wacuba wengi ambao walikuwa hawajui kusoma wala kuandika hapo awali waliweza kujifunza kusoma katika kampeni iliyofanyika baada ya mapinduzi. Wacuba masikini zaidi katika maeneo ya vijijini, na wale waliokuwa na historia ya kufanya kazi mijini, hadhi yao ilipanda ghafla kutokana na sasa kujua kusoma.
Lakini kwa Wacuba wengi, yule Daudi wa zamani aligeuka na kuwa Goliathi mwenye sura ya kutisha. Wakati Castro akipeleka shutuma za matatizo ya kiuchumi ya nchi yake kwa Marekani badala ya kufanyia kazi matatizo hayo kwa kutumia sera zake mwenewe, baadhi ya Wacuba wakaanza kuondoka katika nchi hiyo na kwenda kutafuta maisha mapya nchini Marekani. Miongoni mwa sera zake zilizoshindwa ni lile jaribio la Castro kuwataka raia wote wa nchi yake kuingia katika mashamba ya miwa na kuanza kukata. Alitaka wote, wakiwemo madaktari na wakulima bila kujali kazi ya mtu, kwenda vijijini kukata miwa kwa lengo la kufikia mavuno ya tani milioni 10 za miwa, na wakati huo huo akisisitiza kwamba heshima ya Cuba ilikuwa hatarini. Suala hilo lilishindikana kufikia lengo lake, na kuwaacha Wacuba wakiwa wamechoka na kufedheheka.
Ni wazi kwa watu wengi wa Cuba ambao leo wanaishi nchini Marekani – na wengine wengi ambao wamesambaa katika maeneo mbalimbali duniani, hasa nchini Hispania, Amerika Kusini, na Canada – Fidel hakuwa Daudi. Lakini hili pia lilikuwa wazi kwa Wacuba wengi waliokuwa nchini humo na kuanzisha vuguvugu la chini kwa chini ambao walikuwa wakihatarisha maisha yao kila siku katika mapambano ya siri kujaribu kurudisha demokrasia huko Cuba, hata chini ya ukandamizaji wa serikali.
Vuguvugu hilo lilikuwa miongoni mwa vijana katikati ya miaka ya 1980, wakiwemo wale waliokwenda kusoma nchini Urusi na mataifa mengine ya Ulaya Mashariki, baada ya kuona ukomunisti kwa karibu na majaribio yao kwenye glasnost na perestroika ili kufanya marekebisho ya ukoministi kwa kuanzia ndani.
Leo, vuguvugu hilo linahusisha makundi kama Movimiento Cristiano Liberacion na lile linalofahamika zaidi la Damas de Blanco, kina mama ambao wanatembea kila Jumapili kwenye mitaa ya Havana, wakiwa wamevaa nguo nyeupe, na kubeba ua, wakiomba kuachiwa kwa waume zao, watoto, au kaka zao, ambao walifungwa kutokana na kutordhishwa na uwepo wa chama kimoja, jamii ya kiimla, na Patriotic Union of Cuba.
Mwishowe, Wacuba ndiyo walioumia kutokana na maendeleo yale ya awali chini ya utawala wa Castro. Mishahara yao midogo ikazidi kushuka, na kuwafanya raia wengi wa nchi hiyo, wakiwemo wataalamu wa masuala mbalimbali kuingia kwenye umaskini wa kutupwa. Hata wale waliopata elimu nzuri walibaki katika hali mbaya kiasi kwamba hata chakula tu ilikuwa ni shida, hata pale wanapojaribu kutumia njia zisizo halali kuweza kujikwamua kimaisha.
Wacuba waliulipa utawala wa Castro kwa kunyimwa uhuru, ambao uliwafanya kushindwa kupata maendeleo kiuchumi. Familia ziligawanyika baada ya kukosekana kwa maendeleo ya kiuchumi na uhuru, kitu kilichowalazimu wengi wao kuikimbia nchi yao.
Hiba ya Castro baada ya kifo chake itakuwa ni nini? Nini kitabadilika? Kwa muda mrefu, Cuba imekuwa kama mchezo wa taratibu sana wa chess ambao kete zake zinagoma kutembea kwa haraka. Sasa wakati ambapo mfalme ameondoka, kete nyingine zina nafasi ya kuweza kusogea pia. Ni mambo gani watayafanya, tunasubiri kuona.