Huwa napenda kusikiliza watu wazima from time to time ili kupata picha time yao walikuwa wanafikiria nini. Juzi ilikuwa zamu ya Babu KRS One. Kwenye album yake 'I Got Next' ana track inaitwa 'A friend', dope track si uongo. Nimeiskiliza kama mara 3/4/5 hivi, nikakumbuka our very own..Fid Q ana track inaitwa 'sihitaji marafiki', kwa bahati mbaya sijawahi kuiskiliza mpaka sasa, ila nilishawahi kuona episode moja ya Mkasi Jamaa akiielezea. Knowing Fid Q, nikaingia Tzhiphop na kucheki lyrics, na kulinganisha na track ya Teacha. Nimegundua Jamaa ka-copy concept, baadhi ya mistari na maneno pia, japo kayafanyia sanaa kidogo.
'True friends are quick to sit
in the beginning of all trouble, and when your bankroll doubles/ - Teacha
Vs
Kupata washkaji ukiwa na pesa ni rahisi, Kuwapata na hauna kitu ujue umefanikiwa kichizi/ -
Fid
'Cause don't nobody care about us, all they do is doubt us/
Until we blow the spot then they all wanna crowd us, and wanna shout us/
but you my man from way back' - Teacha
vs
'sihitaji urafiki na usupastaa / ukihit ndo unang'aa..
upishwe useat kwenye bar,upewe beat na Jr../
kitu ambacho haikuwa rahisi kipindi fid ni underground' - Fid
'/I'm not a yes man and none of my friends are yes men
or women/' - Teacha
Vs
'sikia fidq anamsifia fareed ni bandidu sio Yes man/'- Fid
'Whether at the bar with superstars'- Teacha
Vs
'sihitaji urafiki na usupastaa / ukihit ndo unang'aa..
upishwe useat kwenye bar,' - Fid
Kuna lines kadhaa pia za Rappers wengine humo ndani, mojawapo ni ya Biggie Smallz
'Girls used to diss me, now they write letters coz they miss me'
Vs
'Siku hizi mademu wanaoni-miss ni walioni-diss'
Fid Q, Fraud Q or Fake Q??
Teacha Huyu hapa, msikilize mwenyewe halafu linganisha na ngoma ya Fid hapa chini.
Niliamini mapene hayatoshi..na niki-hustle siyakosi/
Sababu.. sipo kwenye loss na life simple huwa hai-cost/
Kwahivyo nikaenda Dar na treni... of thoughts../
Sikwenda kuzubaa au kushangaa nikusaka chapaa boss/
Sikutaka kuivaa mikosi..nilitaKa kuivaa mikoti/
Sikuwa na passport..password.. pin..lakini ni crack codes/
Walionisapoti wote siwaoni kwa line/
Wakini-approach ili nifungue pochi ya noti tu-shine..hatuko fine/
Je mimi ni kaka mubaya...? kaka aso haya../
KAKA..? huniitaga NAKAAYA/
Mama C huniita brother bila shaka.. Mozaya/
Niko sick & tired of being sick & tired/
Na huu ni mwaka wa ndui/ Sitaki upele urudi tena.. mnachotaka sikijui/
Nashukuru hamtopata mbawa ikiwa mtaupata huo uchui/
Mnautaka uadui? mnayempaka ni mtata.. makaka hamkui?
Mmeendekeza hila.. legeza hasira za harakati/
Mie nita-ball.... hata kwa mpira wa makaratasi/
Unaweza ukahisi mie napita tu.. kwakusahau mie nina-hustle/
Nimezaliwa Afrika.. ugumu wa maisha umenifunza ku-struggle/
Ukiwa idle.. unamu-attract shaytwan (SHETANI)/
Kichwani nina MSAHAFU na BIBLE.. life ni zaidi ya ku-have fun/
Kwani.. Kila kicheche anajiona ni mzima/
Na njia pekee ya kuepuka ngoma ni kugoma kupima/
Ikiwa maujuzi haya hayakugusi.. itanilazimu nikuelewe/
Sometimes hata kamusi.. huimiss tafsiri yenyewe/
Nalindwa na dua za mama.. tangu baba simjui/
Namfanya adui mwenye njama aache drama na akue/
Ili ajijue kabla hajakwama huko mrama asitue/
Ajikwamue kwenye lawama.. yenye maana yamchukue/
Kisha anaiombee mimi ili nifaidike kwa hizi mbio/
Siamini kwenye umasikini hivyo sihofii mafanikio/
Ndiyo.. mie ni LEO kwahiyo sifikirii kushindwa/
Zingatia kauli hiyo hausikii inaashiria ubingwa?/
Mie ni mbishi.. muulize Nikki - hatopinga/
Na hata kama ningekua mbuzi ningelala chaka la simba..