Fid Q: Best Quotes from his music, his interviews & from himself

Fid Q: Best Quotes from his music, his interviews & from himself

tunajenga tabia,kisha tabia zinatujenga,
ukishindwa kujiendesha ujue mwenyewe tu ulipenda.
kama umevutiwa na asali,jiandae kumkwepa nyuki,
hauwezi mtisha kwa mawe,adui alieshika bunduki.
ni uchunguzi tu wa kisayansi ambao haukufanikiwa,
kama ng'ombe kula nyasi tuu afu anatoa maziwa.

propaganda
 
usimuamini muongo hata kama akiongea ukweli,
dhambi kutumia dini kama njia ya kutapeli.
 
mstari uliofanya nimkubali Fid Q ni huu wa kwenye Umbo namba 8 ......"kivipi nimkazie jicho wakati binti kasimama!?"

Hapa Fid alitoa mstari wenye maana tatu tofauti

1. Hapa alimaanisha kivipi nimkazie jicho yani nimkodolee tu macho wakati binti aliokuwa kwenye mwendo amekwisha simama?

2. Alimaanisha pia kumkazia jicho ni kumla tigo na nivigumu kumla jicho mtu akiwa kasimama,labda ainame.

3. Kivipi nimkazie jicho ya maana ya tatu alimaanisha kivipi ale kwa macho wakati binti kasimama ,hapa kasimama alimaanisha 'yuko bomba'


Utachukua utayopenda wewe!
 
tunajenga tabia,kisha tabia zinatujenga,
ukishindwa kujiendesha ujue mwenyewe tu ulipenda.
kama umevutiwa na asali,jiandae kumkwepa nyuki,
hauwezi mtisha kwa mawe,adui alieshika bunduki.
ni uchunguzi tu wa kisayansi ambao haukufanikiwa,
kama ng'ombe kula nyasi tuu afu anatoa maziwa.

propaganda

Hakika kabisa ukishindwa kujiendesha kweli umependa!
 
OMG Seriously ''Kala Jeremiah'' now plofiled as a long time artist !

Any way straight to the thread intention

''Unakula nao happy leo, Kesho wanamkata Mkeo''

Fid Q - Sihitaji Marafiki
 
Changanya akili ya kueleza na unachokifahamu vyema

Neno.
hapa anamaanisha unapotaka kueleza jambo flan hakikisha unalijua vzur,kisha uchanganye na akili ya kuelezea,ili unaowaelezea wakuelewe na ujumbe ufike
 
Namiliki cheupe manga na japo nna cheusi dawa

Fid,nlipotoka
Hapa anamaanisha ana demu mzungu(mweupeee),lakini pia anamiliki cheusi dawa,ambayo ni tv show inayomilikiwa na fid
 
Naulenga MWEZI najua hata nkiukosa ntajua tu juu ya NYOTA na mambo yatakua shokpa.

Cnn,fid alishirikishwa na ngwair.
Hapa anatumia fasihi kutuambia ya kua ni vizuri kua na malengo makubwa,ili hata ikitokea usipofikia hayo makubwa,automatically utapata madogo,ambayo huja kabla ya makubwa(hutakosa vyote)
 
Chipukizi fanyeni kazi ili mng'atuke mlipokwama,
Vumilieni kama nyota mtatoka juu likizama

Fid,ni hayo tu
 
Ni binadamu sijakamilika,ila kuandika rhymes sikosei/
Japo MIRUZI ni mingi lakini JIBWA sipotei.

Fid,ni hayo tu
 
Nikifa siachi skendo nauhakika ntaacha pengo,
Kwa hivi vina hata wakulima hujikuta wanameza mbegu.

Propaganda
 
Na-Flow coz kuna "F" kwenye Fid,
Ni Mwanza coz kuna "M" kwenye Mc

Fid,nlipotoka
 
Unaeza ukawa mgomvi,na una BLACK BELT ya kupigwa.

Fid,nlipotoka
Hapa anatumia fasihi kuonesha kua unaweza ukawa mgomviiii,ila ukawa umekubuhu kwenye kupigwa
 
"Simba kala mtu ni habari"/
ila "mtu kala simba" ni habari ya kusisimua.

Fid,tema knowledge.
Hapa anamaanisha kua mtu kuliwa na simba ni habari tu ya kawaida(yani sio kitu cha ajabu).
Ila simba kuliwa na mtu ni habari ya kusisimua,maana hatujazoea kuona kitu kama hcho
 
Matumizi bila akiba,fedha zitatukimbia/
usupastaa mzigo wa mwiba,ukiubeba utaumia.

Fid,august 13
 
Kwenye ukurasa wake wa Insta...dada mmoja alimwambia Fid q nakupenda hadi naumwa

Reply toka kwa Fid Q..."ugua pole dada"
 
Nimeona tofauti kubwa sana ya thread za "Timu diamond" na "Timu Ally Kiba" na hii

Fid Q Unajisoma
 
Kwenye ukurasa wake wa Insta...dada mmoja alimwambia Fid q nakupenda hadi naumwa

Reply toka kwa Fid Q..."ugua pole dada"
Duh,hyo noma
 
Back
Top Bottom