Ficha mambo haya, kisha njoo unishukuru

Ficha mambo haya, kisha njoo unishukuru

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,171
Reaction score
79,630
Na, Robert Heriel

Ukiweza kujificha adui asikuone, nawe ukawa unamuona basi jua umemshinda adui huyo. Kujificha ni moja ya kanuni tatu bora za ushindi, kufanikiwa, kutimiza malengo, kumshinda adui.

Ikiwa wote hamuonani, na mnatafutana basi ushindi upo nusu kwa nusu, halikadhalika mkiwa mmeonana uso kwa uso, ushindi upo nusu kwa nusu.

Kitu kinachofichwa huitwa siri. Kikawaida hakuna siri ya watu wawili. Siri ni tafsiri ya ushindi. Siri ni ya mtu mmoja, halikadhalika ushindi ni wa mtu mmoja. Siri inapokuwa ya watu wawili ni kutoa upenyo wa kushindwa. Siri ndio huo ushindi, kile asichokijua adui yako ndio unapitiamo humo humo.

Siri nini?
Kwa tafsiri yangu, Siri ni ushindi wa kitu chochote kilichofichwa ili kuweka mambo sawa, kuleta amani, kuleta furaha. Endapo siri ikibumbulika mambo hayo yanavurugika.

Kwa nini kuna SIRI?
1. Kuweka mambo sawa, kuleta amani na furaha
2. Kujilinda, Siri ni Ulinzi. Mtu asiye na siri hana Ulinzi
3. Kutawala. Siri hufanya watu watawaliwe, waogope, wawe watumwa. Siri ikibumbulika watu huwa huru. Siri ndio inaleta amani duniani. Kama pasingekuwa na siri hakika pasingetawalika, amani isingelikuwepo.
4. Mafanikio. Siri ipo kwaajili ya mafanikio. Ili ufanikiwe lazima ujue siri fulani fulani.
5. Akili. Siri zipo kwa sababu ni ishara ya akili. Kutunza siri lazima mtu awe na akili. Mtu yeyote asiye na siri hana akili nzuri. Siri ni akili.

Ipo hivi.

Wenye Siri siku zote wanajitahidi kuzilinda siri zao. Wenye siri hutumia akili, nguvu na mali kuhakikisha siri zinabaki kuwa siri.

Jambo moja ninaloweza kusema hapa ni kuwa, ukiona jambo lolote linasemwa sana, linapromotiwa mno, jua jambo hilo sio kweli, jambo hilo linatumika kama kivuli kuficha mambo mengine. Na hapa nazungumzia mambo yanayohusiana na mafanikio.

Mafanikio ni Siri, mafanikio yanathamani, Mafanikio kamwe hayawezi kutangazwa, Mafanikio hufichwa kwa hali na mali. Mafanikio huwekewa vizuizi vingi ili yasifikiwe.

Nitaongea jambo moja, utanisamehe ikiwa litakugusa.

Siku hizi, kuna manabii, masharifu, mitume na maimamu ambao wamekuwa wakitangaza mafanikio kwenye media mbalimbali. Watu hao wamekuwa wakiwalaghai watu kuwa kumfuata Yesu utapata utajiri, kutumia maji ya upako, sijui keki, sijui mafuta ya upako utapata mafanikio. Huo ni uongo. Mafanikio ni siri, siri kamwe haiwezi zagaa kiasi hicho.

Labda ungejiuliza, matajiri wakubwa hapa nchini mia moja huwezi wakuta humo kwenye hayo makanisa au wakitumia hao masharifu, sijui maimamu. Hilo pekeake lingekufanya uone ni uongo.

Kuna vibao vya matangazo ya waganga wa kienyeji, sijui kutoka Sumbawanga, hale, pangani, Gambushi, Ruangwa, Kilwa, hao wote wanakuambia utafanikiwa.

Siri yoyote inayokutafuta sio siri. Mafanikio yoyote yanayokufuata hayo sio mafanikio. Siri haiwezi kukufuata, siri ni lazima uifuate wewe, mafanikio hayawezi kukufuata mafanikio lazima uyafuate wewe mwenyewe tena kwa gharama.

Kuna aina nyingi za Siri.
1. Siri za Kiroho
2. Siri za Kijeshi
3. Siri za Kiuchumi
4. Siri za familia
5. Siri za Kisiasa
6. Siri za Kijiografia
7. Siri za Nyakati
8. Siri za maingiliano

1. Siri za Kiroho
Hizi ni Siri zilizofichwa rohoni ambapo mara nyingi hudhihirshwa kwenye nafsi ya mtu ikiwa kuna ulazima. Siri za rohoni hudhihirishwa kwenye nafsi kwa njia mbili,
1.1. Ndoto
1.2. Maono
Ili siri hizi zidhihirishwe basi ni lazima mwili uwe nusu kufa. Mtu akiwa amelala basi nafsi yake huweza kuona maono kutoka rohoni, maono haya huitwa ndoto.

Kikawaida Mungu anawasiliana na kila mtu kupitia roho yake, kisha roho huwasilisha kwenye nafsi, na kama nafsi haijaharibiwa mtu huyo lazima aikumbuke ndoto aliyoiota, kisha apate maana.

Kila siku mtu lazima aote ndoto, lakini wengi wetu tunakuwa hatuna uwezo wa kuzikumbuka kutokana na nafsi zetu kuharibiwa. Siri za kiroho ndizo huleta ushindi kwenye maisha kwani ndizo zinaijua kesho, juzi na leo.

2. Siri za kijeshi
Hizi ni siri za mbinu, mikakati, mipango, bajeti, silaha, watumishi, na matukio zinazofichwa ili kulipatia jeshi ushindi. Kila jeshi lazima liwe na Siri. Ninapozungumzia Jeshi, nimejumuisha, Polisi kwa aina zake, mgambo kwa aina zake, wanajeshi kwa aina zake, majasusi kwa aina zake. Jeshi lazima liwe na uwezo wa Kusoma matukio ya namna zote na kuyakadiria, kwa maana kila tukio ni ishara ya jambo fulani liwe zuri au baya.

3. Siri za Kiuchumi.
Ni zile zilizofichwa katika mafanikio ya kiuchumi. Siri hizi zinalenga mali, pesa, vyakula, teknolojia, afya, n.k
Ili mtu afanikiwe sharti awe na siri kwenye ishu za uchumi wake. Watu wasijue kipato chako, malengo yako, wapi unataka kufanya nini.
Najua kuna walioajiriwa ambao kimsingi ni lazima watu wajue mishahara yao.
Siri haihitaji kusemwa, siri inahitaji utekelezaji. Kwa mfano kama ulikuwa unampango wa kuanzisha mradi wa Saloon ya kike, usiwaambie watu, bali unatakiwa ufanye watu waone ukiwa tayari unasaloon. Hiyo itawapa mshtuko, lakini wengi wetu tunashindwa kwa sababu, tunasema kabla ya kutenda. Hii inawapa nafasi maadui kukukwamisha.

90% ya watu waliofanikiwa ni watu wa siri sana, yaani utashangaa tuu ananyumba, utashangaa tuu anagari, utashangaa tuu ameolewa, utashangaa tuu kaenda ulaya, yaani hata hukusikia. Watu wengi walioshindwa wamekuwa na mdomo, kuaga aga kwa kila mtu. Hilo ni kosa kubwa.

4. Siri za Familia
Familia yoyote iliyoimara lazima iwe na siri. Mume anaficha siri za mke, na mke anaficha siri za mume wake. Watoto automatic wataficha siri za nyumbani. Familia yenye siri lazima ifanikiwe.

Wanaume wengi wanaficha siri zao kwa sababu wanatambua kuwa wake zao si watu wa siri. Ni wanawake wachache sana waliobarikiwa kuwa wasiri.

Utashangaa Mke anaenda kwa shoga ake kutoa siri za Mume wake, utasikia akisema; Shost tumenunua kiwanja Bunju, au kesho kutwa tunaenda kununua nyumba Tabata. Nakuhakikishia ni wachache wanaotimiza lengo lao siiri inapovuja.

Mwingine anaenda kwa sijui Mchungaji, ati anataka kuombewa kwani Wamepanga na Mume wake wanunue kiwanja, hivyo mchungaji aombe kwa Mungu. Kosa! Utaomba mpaka ukome. Mchungaji mwenyewe hana nyumba, anasubiri sadaka ndio ajenge, yeye ndio akuombee, looh! Ficha mipango yako.

Wewe ungejiuliza tuu, ni mambo mangapi umefanikiwa bila kuombewa na mchungaji au sheikh au mganga ungepata majibu. Huko kwa wachungaji, masheikh, na waganga watu wanaenda kutoa shukrani sio kuombewa. Kama hujui hao viongozi wa dini wengi wao ni mawakala wa adui.

Utakuta mwanamke anamgogoro ndani ya ndoa, badala yeye mwenyewe afunge na kuomba, ajiulize ni wapi anafeli, anaenda kufunua siri za nyumba. Nyumba nyingi zimeangukia hapo. Huwezi omba ushauri kwa kutoa siri za nyumba yako hata siku moja ukabaki salama. Ficha siri, subiri uone mwisho wake, lazima mambo yatakaa poah. Ndani ya familia kuna vipindi, kuna misimu, kuna miaka saba ya neema, na miaka saba ya mateso. Ukilijua hilo wala hutaangaika.

Usipende kuwaelezea watu mume wako au mke wako mtarajiwa, hilo ni kosa, ongea jambo hilo ishu ikiwa too late, dakika za mwisho yaani unawaalika watu kwa maandalizi ya ndoa. Sio mtu chakula hakijaiva ndio unapeta mchele alafu unakaribisha watu mezani. Kosa! Wengi hawapendi,

Utamlaumu mchumba wako bure kumbe kosa ni kidomo domo chako. Mpuuzi wewe

.5. Siri za Kisiasa
Hiz ni siri za masuala yote ya siasa, na hapa nazungumzia siri za nchi au taifa fulani. Kwa mtu binafsi sio rahisi kufanikiwa kwenye siasa ikiwa utakuwa mtu asiye na siri. Mtu anayetaka kugombea nafasi za juu akajidhihirsha mapema, hii imegharimu wengi. Kuchukua mamlaka kunahitaji siri, mpaka dakika za majeruhi jitokeze. Kama ni kutangaza nia, fanya mambo indirect yaani bila kuhusika moja kwa Moja. Tengeneza mtandao bila watu kujua dhima yako. Jifiche acha kuzagaa zagaa, hii imemgharimu, Membe, Lowasa, na sasa nafikiri Tundu Lisu atafuata mkondo huo.

Kwani adui amemjua mpinzani wake mapema, amechukua muda kumsoma madhaiifu yake. Siasa haihitaji kelele, ila kelele inaihitaji siasa. Muda ukifika piga kelele, otherwise maintain silent.

6. Siri za Kijiografia
Kuna mazingira ni favourable kukufanikisha, iwe kwa kilimo, biashara, makazi. au namna yoyote ile. Jiografia ndio kila kitu kwani tunaishi kwayo na inatuzunguka. Ukishaelewa eneo hili ni Potential acha kelele, piga kimya. Kula taratibu, hairuhusiwi kula huku ukiongea. Siri inahitaji utulivu. Piga kazi watu wakija kushtuka wewe umeshashiba, acha hiyo tafuta nyingine,

7. Siri za Maingiliano
Kila unayekutana naye kwenye maisha yako anasababu maalumu, anakupa ishara fulani, pia anaweza kukuachia athari chanya au hasi.

Ni lazima ujue siri za kwanini uliye naye sasa hivi upo naye na kwa nini si mwingine, je anania njema au anania mbaya iliyojificha. Mtu unayekutana naye anaweza akawa na nia njema ila kilicho ndani yake kisiwe na nia njema. Tunafahamu kuna dunia ya ndani na dunia ya nje, sisi tunaishi dunia ya nje kwenye macho ya nyama.

Kila unayekutana naye usimuamini, ukimuamini mtu ni rahisi kukudhuru, Kumuamini mtu ni kuweka usalama wako rehani.

Mtu anaweza kutokea maisha ili akuletee maambukizi ya UKIMWI bila ya yeye kukusudia, mwingine kukupa mimba na kutelekeza, mwingine kukuingiza katika hali ngumu ya maisha huenda ni ulevi wa madawa ya kulevya au tabia mbaya yoyote

Wengine wanakuja kwenye maisha ili kukupa magonjwa ya moyo kwa kisirani chao, wengine kukufilisi na kukuletea mikosi.

Lazima ujue siri za maingiliano yako na watu. Kila anayetaka kuwa karibu yako lazima umchunguze, apende asipende, lakini zingatia asijue kuwa unamchunguza. Hata kama ni mke wako au mume wako, chunguza, uchunguzi hauishi mpaka utakapozeeka.

Wengi wamepata madhila kutoka kwa wenzi wao, walioana wakiwa negetive lakini baadaye mmoja anakuja kuua familia, kuua ndoto za familia na watoto.

Anayekuambia mwanamke au mwanaume hachunguzwi anakudanganya, hakupendi, na anataka usalama wako uwe mashakani. Chunguza lakini uwe na moyo kwa utakayokutana nayo kwenye uchunguzi wako kwani yanaweza kukuumiza. ukigundua jambo baya usikurupuke, jipe muda kutoa maamuzi.

Adui anaweza kuwa yeyote, usimuamini yeyote, chunguza yeyote ikiwa yupo katika mzunguko wako, iwe Mke/mume, Mama, Baba,, kaka, Dada, na marafiki. Chunguza, hakikisha wasijue unawachunguza.

Kujua siri ni kuwa salama, huwezi kuwa salama ikiwa kuna mambo huyajui yanaendelea katika mzunguko wako wa maisha. Ni hatari.

Nimeandika kirefu, pengine wengine wasipendezwe na makala ndefu, ingefaa sasa niwaage, kisha Mungu akipenda nitaandika tena.

Kwa maana hakuna mwisho wa kutunga vitabu; na kusoma sana huuchosha mwili kama alivyosema Suleiman mwana wa Daudi.

Basi nami Taikon nakuambia, ziishike amri za Mungu nawe umche zikuzote, wewe na mke wako, na watoto wako, na watumishi wako, kwa maana hiyo ndio imfaavyo Mtu.

Ulikuwa nami;

Robert Heriel
 
Taikon ni neno kutoka lugha gani? Lina maana gani?
 
FICHA MAMBO HAYA, KISHA NJOO UNISHUKURU.

Na, Robert Heriel
Maandishi ya Robert Heriel kwa Lugha ya Kiswahili.
Haki zote zimehifadhiwa.

Taikon wa Fasihi
0693322300
Safi sana kiongozi, nimekuelewa
 
Kuna mambo mengine ukifanya siri, utaharibikiwa

Share na watu usaidiwe, hivyo yaan

Ni kweli kabisa,
Ila kuhusu kufanikiwa kama huna siri ujue hutafanikiwa,
Ukiona unatafuta ushauri wa namna ya kufanikiwa, ujue bado hujafuzu kufanikiwa, hivyo hata upate milioni 100 bado utaomba ushauri uzitumieje
 
Back
Top Bottom