FFU mlinzi wa benki NMB ajipiga risasi

Bora wewe uliyeamua kujiuwa kuliko ukatumwe kuuwa raia wasiokuwa na hatia rip afande
 
Askari polisi mlinzi wa NMB benki Dar amejipiga risasi mbili tumboni na kufa haijajulikana sababu.

kisa cha askari huyo ni hiki hapa.

Askari huyo alifikia uamuzi huo baada ya kuzungukwa/kutopewa posho yake ya sherehe ya miaka 50 ya uhuru wakati aliwajibika vyakutosha kwenye mkesha pamoja na sherehe yenyewe kapigwa sana na jua lkn posho yake akazurumiwa/hakupewa.

Cku ya tukio alipo ingia shift alipiga sim mala kazaa kuulizia posho yake bila mafanikio baadae dk tano kabla ya tukio akapigiwa sim na bos mwingine na kumwambia posho yake ashamwingizia kweny a/c yake tokea jana.

Jamaa akakurupuka fasta kwenda kwenye ATM kucheki salio alichokikuta ni siri yake bali alitoka kakunja uso na kuonekana mtu mwenye huzun na aliyekata tamaa na maisha haya alikoki bunduki na kusema sema maneno kama mtu anayelan kitu flan ndipo hapo akaamua kujimiminia risasi.

Source:tunguli la mafixadi
 
Kafa kizembe kweli si angeacha hata wosia kuwa anajiua kwa sababu Serikali haiwajali police then ce Chadema tungepata mtaji.
 
Pia ni Risk kuwapa siraha watu ambao wanalipwa kidogo serikali haiwajali ivi angeamua kufa na wengi si angeweza au magazine yake ilikuwa na hzo risasi 2.
 
Mshahara mdogo halafu kazi ngumu.Ila licha ya ugumu wa maisha yao hufanya kazi kwa kujituma sana

Afande,raha ya milele akujalie Ebwana na nuru ya rehema akuangazie.Amen!

kwa nature ya kazi yao lazima ujitume, maana ukizubaa wanaume wanakuwahi wewe kwa risasi
 
Chezeiya moyo wa ntu! Kidogo na mie nijilipue na hii gun yangu!
Afadhali wamtume kwenye maandamano manake huwa anawaelekezaga waandamanaji pa kujificha,lol
unahaki mama ya kujilipua kama kweli ingekuwa hivyo ila kwa sasa kula,kunywa kwa raha zako
 
me ndo maana nakuwa makini sana nikiwakaribia hawa mapolisisisiem,wanashida nyingi sana mioyoni mwao,so anaweza kumaliza matatizo yake na wew bila kosa lolote,hasa unapoingia kwa atm mashine anaona unadroo cash za kutosha while yeye waatoto hawjui watakula nini.RIP a afande

Kushinda zako? Acha upumbafu na ujinga! Mbona kuna polisi wengi wana maisha mazuri sana kushinda nyie mnaojifanya raia matajiri. Acha askari wetu wafanye kazi, huyo tar.yake imefika! Mungu amrehemu.
 
so sad : kumbe hyu dogo namjua ..mara ya mwisho kukutana naye walikuwa yeye na kaka yake nilirud nyumbani ...tena nakumbuka niliwapa dogo pesa ya kutumia si unajua mtu ukiwa umetoka mbele unawatoa ndugu zako kiaina ..dogo namkumbuka sana alikuwa mtu mkimya na mtulivu zaidi ya ufikiriavyo..dah rip dogo mpaka sasa hivi siamini yaani
kwanza baba yake na mama yake walishafariki kwa hiyo dogo alikuwa anaishi kwa bibi yake...mpaka sasa hivi hawajajua chanzo kwani dogo alifuta kila kitu kwenye simu
 
Back
Top Bottom