Ferry - Kigamboni: Weka hapa Kero, Ushauri na malalamiko yako

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
Zamani enzi zetu tukisoma pale ferru tulivuka kwa shilingi 20 tu kutumia mitumbwi.

Serikali ikaleta MV Magogoni na baadae Mv Kazi na mv Kigamboni.

Hivi vivuko Kigamboni kina injini 4 lakini mara nyingi wanawasha mbili tu na kufanya kutumie dakika 20 ndani ya maji.

Kero:
wameleta mfumo wa kadi, ili kuzuia wizi unaofanywa na baadhi ya watumishi lakini kila siku sistim ipo chini na wanasababisha jam issiyo na ulazima.

Wamama wauza samaki:_ Hawa wakipanda tu pantoni, wanakimbilia mbele na kuweka ndoo njiani na kukaa, ukimwambia akupishe, una tusi, hawa wamama wengi ni mashankupe?

Hawa wamama ni kero sana na wanaogopeka maana matusi yapo kwenye koromeo! Unaweza fikiri pantoni imejaa kumbe wamama wamekaa na ndoo zao njiani.
Samahanini sana.

Wauza machungwa: hawa wanapaki basikeli ndani ya pantoni na kuzuia abiria kuingia kwa urahisi.

Wauza karanga na pipi: Hawa wamefanya kivuko chao, wanazuia njia saa ya kupanda na wanasukuma watu ilimradi tu wauze, ni wabishi na hatujui wana kibali gani cha kushinda siku nzima kwenye kivuko.

OMBA-omba: ebwana eeh hawa ndugu zangu wanatoka mkoa fulani upo katikati ya nchi,wanashinda kwenye ferry na lounge, wao muda wote wanafunua makovu yao, sehemu zenye vidonda ili watu waone, hii ni kero.

Magari binafsi: Mtu kishapaki gari ndani ya pantoni hazimi injini, joto kali, moshi yeye anakula AC wengine huku wanaumia mapafu na joto, JKT mgambo wapo tu na ma simu yao sijui wanafanya kazi gani!

Wanafunzi IFM/MAGOGONI./CBE/DIT: wanafunzi wengi wa hivi vyuo wanaishi hosteli za kimaskini kigamboni na badhi wanaishi na wanaume zao.

Bodaboda wakati wa kutoka kigamboni, : Yani unakuta bodaboda zimezuia njia nzima, raia inabidi apite njia ya mwendokasi na kuna watu kadhaa washagongwa kwa sababu hiyo.
Wauzza samaki nao wameziba njia, yaani kwa ujumla WAZIRI PEKEE WA HIYO WIZARA ALIKUWA MAGUFULI, wengine hawajui hata wanachofanya hapo.


1.jpg
2.jpg
3.jpg
 
Nini kifanyike
Itengwe panton moja wapo,yenye kusafirisha abiria tuu,na nyingine iwe ya vyombo vya Moto pamoja na baiskeli.
 
Mkuu hivi Speed ya MV Kigamboni na MV Magogoni ili ina speed ndogo, labda umekosea mkuu Mv Magogoni ni mwendo wa bibi harusi
 
Back
Top Bottom