Ujasiriamali wakati wa usiku Kigamboni Ferry ni kero

Mapico

JF-Expert Member
Apr 17, 2019
281
1,000
Habari zenu wakuu poleni na majukumu ya kila siku.

Imepita kama miezi 3 hapo nyuma tangu hii hali nianze kuiona aisee ukiwa unashuka na pantoni pale ferry kuanzia kituo cha juu kukata tiketi utakutana na watu wamefunga njia wanauza madafu na bidhaaa ndogo ndogo hamna shida kwa vile riziki ndiyo inatafutwa popote

Kimbembe ukifika stendi kipande cha barabara ya kutoka na kuingia.

Magari ya kibada toangoma hawa wafanyabiashara wasipodhibitiwa wanasababisha kero. hakuna sehemu ya kupita sehemu ya watembea kwa miguu wameweka vibanda na meza za matunda.

Hakuna sehemu ya kupita ukipita utapita kati kati ya barabara na ni hatari kwa watembea kwa miguu wanasababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara .

Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni je hili hamlioni au ndiyo mpaka litokee la kutokea muamke

Namulika uzi teyari"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom