Kalamu Nzito
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 376
- 850
Wimbo wa Ferooz maarufu kama “Wema wangu umeniponza” ni wimbo unaosimulia namna dhamana ilimponza mtunzi. Ferooz anamuwekea dhamana rafiki yake ambaye alikamatwa kwa kosa la jinai. Baada ya kutolewa kwa dhamana, rafiki yake anatumia mwanya huo kutokomea kusikojulikana. Ferooz, akiwa kama mdhamini wa mtuhumiwa, anakamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha.
Kiuhalisia, kumuwekea mtu dhamana haimaanishi kwamba unabeba tuhuma au mashitaka yake. Hivyo, mdhamini hawezi kuhukumiwa kwa makosa ya mtuhumiwa/mshitakiwa pale ambapo mtuhumiwa/mshitakiwa huyo atatoroka. Mdhamini atawajibika kwa kiasi cha fedha au mali aliyotumia kuweka dhamana hiyo tu.
Licha ya kasoro hiyo, wimbo ni mzuri sana na unaishi mpaka leo kwani, unaangazia ukweli mchungu wa namna gani tunaweza kuumizwa kwa kutenda wema.