Ifikie pahala wanaume mkubali tu kwamba yote mnayoyapigania ni kwa maslahi yenu na si ya wanawake wala ya jamii acheni hizi propaganda zenu za mwaka 47 siku hizi wanawake wana akili, maana kila ukiuliza madhara ya feminism kwa wanawake wenyewe hakuna mwenye majibu yaliyonyooka utaletewa kiswahili kirefu halafu mwisho wa siku utagundua hayo madhara ni kwa wanaume, ila wanaume wanatumia self serving reverse psychology trick ili ionekane kama vile wanapigania maslahi ya wanawake na ya jamii kwa ujumla ili mradi tu wanawake wafanye yale wanaume wanayoyataka
Madhara ya feminism kwa wanawake ni kitu cha kuuliza kweli na tunaongea kila siku hapa? Ngoja nikuwekee hapa shida ipo wapi.
Feminism na feminist wameleta changamoto zifuatazo kwenye jamii yetu.
1. Ideology ya feminism imeharibu akili ya mwanamke wa kisasa wa kitanzania kuamini anatakiwa ajipambanie yeye mwenyewe na si jamii yake,si watoto wake wala wanawake wenzao. Hii tayari imeshamfanya mwanamke anayefuata u feminist kuwa chizi fresh wa jamii. Tazama hawa wa marejesho na michezo ya upatu wa kila siku mtu anatoka au kausha damu utanielewa.
2. Feminist na feminism haiungi mkono swala la familia ya baba mama na watoto,ina wafundisha wanawake kuamini kuwa maisha yao binafsi ndio kipaumbele so akipata watoto ajenge familia ya single mother households ambaye technically ni kinyume na vitabu vya dini,lakini pia inakinzana na malengo ya ustawi wajamii wa ujenzi wa taifa bora.
3. Feminism haisemi chochote juu ya vitu negative wanavyofanya wanawake wa kisasa kwenye jamii more importantly feminist hawana ajenda za kuwajenga wanawake na kuwapa mtazamo chanya wa kijamii, badala yake ukimya wake ni sapoti ya tabia zote za hovyo mfano utoaji mimba,umalaya,udangaji, ulaghai wa mahusiano, kutelekeza watoto walelewe na house girl, wizi wa pesa za wanaume,usagaji,ulevi,ulaji mbaya unaosababisha wanawake kuwa muonekano wa viboko wa katavi na kuathiri hata afya zao za uzazi na kadhalika.
4. Feminism sio ideology ya kumkomboa mwanamke sababu ukitazama maudhui yake si ya kumkomboa bali kumpa mwanamke harakati ambazo hazina msaada kwenye jinsia yake na mbaya zaidi kumtoa katika ramani ya jamii. Tazama wanawake hawaki nyumbani wanawaachia house girls wakidai wankwenda kutafuta, huko kwenye kutafuta majority wanajenga mahusiano mapya badala ya kushimu ndoa zao na kufanya kazi kama walivyodai wanataka, wakipata mapato hawataki kujenga familia zao wanataka kujitenga na kujijenga binafsi. Sasa hapo mwanamke anakombolewa vipi zaidi anazidi kufutwa kwenye jamii na kuwa kiumbe kisicho na sehemu au role maalumu kwenye jamii.
5. Feminism sio idea ya jamii yetu ya kitanzania wala kiafrika ni zao la ma'zionists ambao ndio wale wale wapo nyuma ya movement za LGBTQ, nyumba ya gender reassignment programs na left wings woke agendas mambo ya kishetani yote kwao ni okay so siwezi kushangaa kwann wanafosi hili la feminism afrika ili wawatumie wanawake kama daraja kuzisambaratisha jamii za kiafrika.
6. Feminism kwa Tanzania kupitia ideology zake imetengeneza masingle mother wengi sana. Sasa sijui kwako kama usingle mother ni mafanikio kwa mwanamke.
7. Feminism imeteka akili mabinti wengi wa miaka ya 1980 na 1990 na kuwafanya wapoteze muda wao muhimu (prime years from 16 to 26) wakichase dreams na 💰 ili wawe maboss ladies na kujikuta wakiamka kutoka katika usingizi huu wakiwa na miaka 30 kwenda juu,hawajawa maboss lady,broke, no conducive cash flow, hawana anwani,hawana ndoa,hawana familia,hawana mume wala watoto, heshima hawana zaidi ya rekodi chafu ya kubadili vitanda (midfielders wa lodge) wanajua kuta nyingi za lodge kulika kuta za kanisa. Kwa kifupi feminism imewapoteza njia.
8. Feminism ni brainwashing scheme inayolenga kutengeneza cults za Wanawake wenye trauma mbali mbali za kimaisha kujikubali na kumshirikisha shetani kama MUNGU wao kwa maana culture ya feminism haiwaruhusu kutumia muongozo wa MUNGU huyu wa Abraham. Watazame mafeminist wengi utaona wana move kama kikundi cha talebanians.
9. Feminist wengi hawajui nini maana ya kuwa mwanamke na hii ni matokeo ya hii ideology kuwapumbaza na kuwatoa kwenye reli ya uanamke. By average feminist ukimwambia kulea mtoto anasema ni utumwa,ila atapiga kijijini simu aletewe mtoto wa mwanamke mwenzake aje mjini kumpikia,kumlelea mtoto, kumfanyia usafi wa nyumba nzima,kumtuma dukani mara 100 kwa siku yote kwa mshahara wa 30,000 ambao atamkata 10,000 kwa kosa la kuunguza nyama sababu alikuwa anambeleza mtoto wake mwenyewe na kupitiwa na usingizi ila yeye akaita uzembe. Huyu ndio mkombozi wa wanawake na anajua thamani ya mwanamke au ni feminism imetengeneza vichaa wa jamii wanaokandamiza zaidi uanamke.
10. Ukiwatazama wanawake mafeminist wengi hawana furaha na hata takwimu zimeshaonyesha hilo. Kinyume na matarajio, feminism iliwaahidi wanawake liberation kwenye maisha nje ya mfumo dume but haikuwaambia kuwa liberation huja na gharama na mizigo na majukumu zaidi. Kujitegemea sio rahisi kwa mtegemezi.
Wanawake wasasa wanahangaika kama mtu aliyelala chumba chenye joto kali huku akiutafuta usingizi kwa kujipepea na gazeti.
Akijipepea usingizi unakuja, usingizi ukikolea mkono unaacha kujipepea anastushwa na joto,and the cyle continues. Maisha ya mwanamke na mwanaume ni mwanamke kulala huku mwanaume akipepea asikatishe usingizi wake hadi kukuche.
Feminism ikawa danganya na ndio maana saa hii mnaomba hela sana kwasababu you are out here on your own wanaume wamestuka hawataki kutumika kama ATM mkiwa na shida mnakuja na vichanjio kudraw hela ambazo hamkuweka.
11. Feminism ideology imewacorrupt watoto wa kike kuamini kuwa wao ndio wenye maamuzi ya mwisho ya miili yao to the point kwamba wanafanya vitendo vyenye irreversible side effects in the name of "my body my choice". Kutoa mimba, kulala na wanaume wengi kunakosababisha mangojwa makali ya STDs,kuingiliwa kinyume na maumbile kiasi kwamba inavuruga utaratibu wa kujifungua kawaida na matokeo yake wanatumia operation delivery na kulimit kiwango cha watoto mwanamke anaweza kutengeneza na mwanaume.
Madhara ni mengi, unajitoa ufahamu tu hapa