"Feminism" inavyopotea njia Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Feminism" inavyopotea njia Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiranga, Apr 2, 2009.

 1. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  1. Naibu Waziri anajionyesha alivyo mtupu kwa kuanzisha "gender war" isiyo lazima pahali ambapo angeweza kutumia nafasi hii kushughulikia maswala muhimu ya wanawake.

  2.Anajionyesha kwamba hawezi kutumia logic.Kwamba hakuna ufisadi unaohusisha wanawake katika mfumo ambao hauna viongozi wanawake hakuonyeshi kwamba wanawake hawana ufisadi, kunaonyesha kuwa hakuna mafisadi wengi wanawake kwa sababu hakuna wanawake wengi katika sehemu nyeti ambazo ufisadi unaweza kustawi.

  3.Hajauangalia ufisadi katika upana sahihi, wanawake wanahusishwa sana katika ufisadi na kuanzia ufisadi ngono mpaka ufisadi wa IPTL.

  Naibu Waziri sio tu anajionyesha yeye asivyo makini, bali pia, kwa kusema maneno haya jukwaani, anauonyesha mfumo mzima uliomlea usivyo makini.

  Naibu Waziri: Watenda ufisadi ni wanaume tu

  2009-04-02 11:51:34
  Na Muhibu Said


  Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Lucy Nkya, amesema wanawake wamethibitika kutokujihusisha na ufisadi kwani katika kundi kubwa la watu wanaotuhumiwa kwa vitendo hivyo nchini kwa sasa limejaa wanaume, kwa hali hiyo ili kuvikomesha ni vema kuwachagua wanawake zaidi katika nafasi za uongozi.

  Dk. Nkya alisema hayo alipokuwa akifungua warsha kuhusu ``Nafasi ya mwanamke na jinsia katika kuimarisha siasa na demokrasia,`` iliyoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), jijini Dar es Salaam jana.

  ``Katika haya masuala ya ufisadi yanayoendelea, nadhani mtakuwa mmeona kwamba hakuna mwanamke anayetajwa kuhusika. Hii inaonyesha kwamba namna nyingine ya kupambana na ufisadi ni kuchagua viongozi wengi zaidi wanawake katika nafasi za kisiasa,`` alisema Dk. Nkya.

  Alisema baadhi ya mila na desturi zimekuwa zikikinzana na jitihada za kuleta usawa wa jinsia, hali ambayo imewafanya wanawake kuendelea kuelemewa na majukumu na mzigo mkubwa wa kazi, hata pale ambapo mabadiliko madogo tu ya kiteknolojia yangewapunguzia uzito huo.

  Aliishukuru TCD kwa kutambua umuhimu wa kuwashirikisha wadau mbalimbali katika mijadala inayolenga kutoa elimu, hamasa, ikiwa ni pamoja na kuendeleza na kuimarisha jitihada zinazolenga kufikia lengo la asilimia 50 kwa 50 katika ngazi za uongozi na maamuzi katika siasa na utendaji.

  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akiwasilisha mada katika warasha hiyo, aliwataka wadau kujadili nafasi ya wanawake kwa mapana wakati wanapotafuta Katiba mpya ya nchi.

  Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Gharib Bilal, ambaye alikiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika warsha hiyo, alisisitiza mapendekezo ya CCM ya kutaka kila wilaya iwe na majimbo mawili ya uchaguzi ili kutoa fursa kwa wanawake wengi zaidi kuingia bungeni na kufikia idadi ya 50 kwa 50 iliyomo kwenye azimio la Umoja wa Afrika (AU).

  Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama (CCM), alisema suala la usawa wa kijinsia, ni haki ya binadamu na si upendeleo kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

  Hata hivyo, Mbunge Viti Maalum, Halima Mdee (Chadema), alisema haina mantiki kuwa na wanawake wengi katika vyombo vya maamuzi, kama vile Bunge, huku mchango wao ukiwa ni mdogo katika chombo hicho.

  Ingawa Dk. Nkya hakutaja ufisadi alioulenga, miongioni mwa kashfa za ufisadi zinazovuma nchini kwa sasa ni pamoja na wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jumla ya watu 21 wakiwa wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi huo.

  Jumla ya Sh bilioni 133 zilichotwa EPA kifisadi na makampuni 22 yakiwa yamesajiliwa kijanjajanga. Miongoni mwa walioshitakiwa kwa tuhuma hizo ni wanaume 18 na wanawake watatu.

  Kesi nyingine ambayo inahusu ufisadi ni ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development Corporation (LLC) ambayo mmiliki wake mwanaume, Naeem Gire, amefikishwa mahakamani.

  Pia kuna kashfa ya Kamapuni ya Kagoda ASgriculture inayodaiwa kuchota Sh bilioni 40 za EPA, hata hivyo hakuna aliyeshitakiwa kwa sakata hili. Kashfa nyingine ni ya kamapuni ya kukagua tahamani ya uchimbaji madini ya Alex Stewart ambayo mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona wameshitakiwa kwayo, wakituhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka.

  Pia katika Alex Stewart aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Grey Mgonja, naye ameunganishwa katika kesi hiyo.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Apr 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Maria Kejo......
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Anna Mkapa.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Apr 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Mange Kimambi
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Mary Ndosi.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Apr 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Mke wa Hassy Kitine (alitumia sijui $63,000 huko Canada)
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Zakia Meghgi alitetea ufisadi wa EPA,Sophia Simba wa UWT je?
   
 8. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Huyo mama ndiyo anajifunza siasa. Halafu amechagua siasa za ulaghai wa waziwazi.
  Amewadhalilisha wanawake, tena si kidogo.
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  Apr 3, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Duh Mkuu sura yako inafanana na yule Mwanasheria wa IMMA..... una bifu?
   
 10. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kweli wamepotea kabisa. kwanza mafisadi wanawake wapo wengi sana tu, ni kwamba tu hawajapewa huo ugavana wa benki kuu, uwaziri mkuu, uwaziri wa nishati, nk. Wengine kwenye ufesti ledi tu walipigiza vibaya kama akina siti mwinyi na anna mkapa. Na juu ya yote, ufisadi mwingi unaofanywa na wanaume una wanawake behind the scenes ambao ndio wanaofaidi hayo mahela kama wake, mahawara nk, wanatumia hayo mahela ya kifisadi kufanyia shopping za kufamtu.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,553
  Likes Received: 18,238
  Trophy Points: 280
  Naomba tutofautishe feminisim na activist. Mama Lucy Nkya ni 'aids activist' wala sio feminist. wapo ma 'gender activst' ambao siyo feminist.
  ili kuwa fare, tenganisha feminist ni nani na anapinia nini, gender activist ni nani na aids activist ili upate jibu.
  ni ukweli usiofichika, wanawake wako more coutious kwenye vitendo vya uvunjaji sheria.
  wanawake mara nyingi zaidi ni makini kuliko wanaume kwenye issue nyingi.
  hata used car, ukisema 'driven by a lady', it fetches better deal kuliko gari inayoendeshwa na mwanaume.
  Jambo moja ni wazi, japo ni wanaume ndio wanaofanya ufisadi, wanaume wanafanya usisadi huo ili kuwafurahisha wanawake. God made man, man made money, money made man mad for women'.
   
 12. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli hata mimi nilishituka nilipoona heading ya hii thread, kwa ufahamu wangu Feminism hapa nchini imeendelea kuwepo tena kuimarika sasa than ever, na maneno ya mwanasiasa mmoja Lucy Nkya hayawezi kuwa ni kipimo cha feminism kupoteza muelekeo.
   
 13. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Bila kumsahau Matlida Burhani aliyemwandama Mhe. Zitto kwamba kasema uongo kuhusu Uozo katika mgodi wa Buzwagi. Ili tujiridhishe na Kauri ya Mhe. Dr.NKya, tufanye utafiti kwa wafungwa wanawake, ni wangapi wamefungwa kwa kutafuna hela za serikali? wapo tunaowafahamu. Ufisadi si wa wanaume pekee na akina mama tena ndio wanao -pressurize-wanaume wao kwa mahitaji yao ya kibinafsi. Mfano Mke wa Rais wa zamani wa zambia Chiluba ambaye kafungwa kwa sababu kama hizo
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Kama Naibu Waziri wa ya wanawake anaweza kusema hivi, naibu waziri anayeshauriwa na wataalam wa mambo ya wanawake, huwezi kusema huyu ni mtu mmoja.

  Huwezi kukataa kwamba feminism inakuwa misguided.Feminism is such a broad term kiasi kwamba ukikataa kwamba huyu mama si kiongozi wa feminism unajionyesha kuwa either huelewi feminism ni nini, au una emotional attachment na mambo haya kiasi cha kukataa ukweli.

  Kitendo cha mtu mjinga mjinga kama huyu kupewa nafasi kubwa kama hii katika serikali tayari kina derail feminism.

   
  Last edited: Apr 3, 2009
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Kama vile kauli potofu za rais zisizoweza kuwa kipimo cha serikali kupoteza muelekeo.
   
 16. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  samahani mkuu naona tumekukosea sana, umeanza kutu attack personality, lakini lengo lilikuwa ni jema tu, kusema mtu mmoja kapotoka ni sawa na doctrine yote imepotoka si sawa. Kwa mfano rahisi muumini mmoja wa dini ya kikristo akizini hauwezi kusema kama dini yote ya kikristo imeharibika au imepotoka si sawa. Kwa maana nyingine hata kama Lucy Nkya amekosa muelekeo si sawa hata kidogo kusema Feminism imekosa muelekeo hata kama yeye ni Feminist damu.
  Narudia samahani sana labda ni ujinga wangu wa kutofautisha belief(feminism) na mtu (feminist) ndio uliokukwaza.
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Nimeongelea kuhusu central position ya naibu Waziri kama kiongozi wa mambo ya wanawake.

  nimeongelea position yake, na maana ya hiyo position kwa ujumla, hususan kutoka katika point of view ya ushauri anaoupata wizarani, huyu mama anatoa official stand za serikali ya Tanzania, naibu waziri anaisemea serikali, anawashauri wasomi, anapata mawasiliano yanayotakiwa.Huyu ndiye mmoja wa viongozi wetu wakubwa katika maswala ya wanawake.Huwezi kum dismiss huyu kama "mtu mmoja tu", huyu anawakilisha wizara ati, hakwenda pale kama mama Nkya, kaenda kama Naibu Waziri.

  Isitoshe, siajsikia mtu mwingine yeyote katika feminism movement aki i denounce kauli hii kama divisive, which means hata watu wa TAMWA na TGNP nao wameona sawa tu.

  Sasa unataka kusema feminism imeji disassociate na hii kauli? Mtu akisema feminism inakuwa derailed atakuwa amekosea?

  Kauli-Mtu!
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Halafu inaonekana huyu Dk Nkya michemsho na inconsistencies ndiyo kazi yake, ona hapa chini alikuwa anaongelea kuhuhu mambo ya chuki katika jamii, with dictatorial leaders like these...

  Makala -Dk. Nkya, umeteleza kuhusu HakiElimu

  Dk. Nkya, umeteleza kuhusu HakiElimu
  Salehe Mohamed


  MOJA ya maadui watatu aliowapiga vita hayati Mwalimu Julius Nyerere katika nchi hii ni ujinga. Alifanya jitihada kuboresha elimu, ikiwamo kutoa elimu bure na kuanzisha kisomo cha watu wazima.

  Aliamini kuwa taifa lenye wajinga kamwe haliwezi kuendelea; lingelikuwa tegemezi na kuwa na watu wasio na fikra za kimaendeleo.

  Hii ikiwa pia ni kwa ajili ya kudumisha demokrasia.

  Wiki iliyopita, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Lucy Nkya, alitoa kauli ya vitisho dhidi ya Taasisi ya HakiElimu, kutokana na matangazo ya kuikosoa zaidi serikali. Alidai kwamba, matangazo hayo yanajenga chuki kati ya jamii na serikali.

  Alikwenda mbali zaidi kwa kusema serikali imechoshwa na matangazo yanayotolewa na taasisi hiyo na kwamba ipo siku serikali itatoa meno yake na kuiuma taasisi hiyo ambayo katika Awamu ya Tatu chini ya utawala wa Rais Benjamin Mkapa, iliwahi kufungiwa kwa madai kama hayo.

  Katika tishio lake hilo Dk. Nkya alisema HakiElimu inatakiwa kuwafundisha vijana na wanafunzi namna utawala bora unavyotakiwa kuwa, si kuwajengea misingi ya kuichukia serikali yao kwa vitendo vya kifisadi.

  Alitolea mfano matagazo ya kwenye televisheni yanayowaonyesha wanafunzi wakifanya hesabu baada ya taifa kupokwa sh bilioni 133 kwenye akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) kwa kuwauliza hizo zingetosha kufanya mambo gani.

  Kimsingi nadhani Dk. Nkya, anaelekea kulewa madaraka na anafikiri Watanzania wa leo ni wale wa miaka mitano iliyopita, ambao wakiambiwa kitu huamini bila kuhoji au wanaona mambo yanakwenda kombo na wao wanakaa kimya.

  Amesahau kwamba zama hizi ni utandawazi na demokrasia inapanuka zaidi na kila kibaya kinachofanywa na viongozi au watendaji wa serikali huanikwa na watu wenye nia njema na nchi hii ili waliofanya vibaya warekebishe makosa yao.

  Ni utawala bora upi ambao Dk. Nkya anataka HakiElimu iwafundishe vijana na wanafunzi ambao kila kukicha husikia kiongozi fulani amesaini mkataba mbovu kwa niaba ya nchi hii hotelini, kaiba fedha, kaghushi nyaraka au vyeti vya shule.

  Kila kukicha viongozi hushindana katika kutafuta masilahi binafsi, kujilimbikizia mali, kuwasomesha watoto wao nje ya nchi kwa kodi za walalahoi ili baadaye waje kushika nafasi za uongozi na maovu mengi ya aibu mbele za watu.

  Ni kiongozi gani hivi sasa anaweza kusimama mbele za watu na kuhubiri utawala bora ilhali hata yeye mwenyewe nafsi inamsuta kuwa si muumini mzuri wa kile anachokizungumza bali ni propaganda za siasa.

  Viongozi wa nchi hii sasa wanaelekea kulewa madaraka ndio maana kila kukicha wanatoa maamuzi au vitisho vya kudumaza demokrasia na mawazo ya kuliendeleza taifa.

  Wanataka kila siku wawe na upeo zaidi ili kuwarahisishia watawale kadri wanavyotaka bila kujua kuwa zama hizo zilishapitwa na wakati na wakifanya mchezo ipo siku kauli zao zitawatokea puani.

  Viongozi wengine wanafanya maamuzi ya ajabu kwa nia ya kuwafurahisha wakubwa au marafiki zao, bila kujua kwamba ni hatari zaidi kwani nafasi walizonazo wasingezipata kama wasingechaguliwa na wananchi.

  Upofu gani alionao Dk. Nkya kiasi cha kushindwa kuona ufisadi uliofanywa kwenye EPA, Richmond na mikataba ya madini, jinsi ulivyochangia kwa kiasi kikubwa kudunisha maendeleo ya wananchi.

  HakiElimu ndio waliowajenga viongozi na watendaji hao kutafuna rasilimali za nchi kwa maslahi binafsi? Au kwa kuwa HakiElimu ni mnyonge na rahisi kushughulikiwa?

  Kwa nini ukali wa aina hiyo asiouonyeshe kwa mafisadi waliochota mamilioni ya EPA ambao bila shaka hata yeye anawajua? Lakini hakuna hata siku aliyowahi kutoa kauli yake dhidi yao.

  Ubadhirifu wa EPA ni mgeni machoni na masikioni mwa Dk. Nkya, kiasi cha kuitolea uvivu HakiElimu inayobainisha mambo yaliyo wazi tena yaliyofanyiwa uchunguzi wa kina?.

  Binafsi, naamini kwamba wakati mwingine mtu kama hana cha kuzungumza, ni bora anyamaze kuliko kuongea jambo litakalomshushia hadhi yake mbele ya jamii inayomheshimu.

  Leo, wote tu mashahidi kwamba utawala wa awamu ya tatu ulikuwa ukijisifu zaidi kwa kufuata misingi ya utawala bora, lakini mara baada ya kuondoka madarakani, tumegundua mambo mabaya mengi yaliyofanywa nayo.

  Kibaya zaidi, hivi karibuni aliyekuwa rais wa awamu hiyo Benjamini Mkapa kwa mara ya pili alishindwa kupata tuzo ya utawala bora iliyotolewa na bilionea Mo Ibrahim.

  Dk. Nkya kamwe Watanzania hawawezi kuwa na mawazo ya kale kwa maisha yao yote, laizma wabadilike hivyo ni vema nawe ubadilika. Kuitishia HakiElimu, hapo umeteleza!
   
 19. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...Mkuu, Utafungwa!! Ni BATILDA Buriani! Au unamsema Mwingine??
   
 20. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Je na wale wanawake waliotumia nyadhifa za waume zao za Ubunge na uwaziri ili kupora nafasi za Ubunge wa Viti Maalumu sio Mafisadi?
   
Loading...