Kapuchi,
Ebu lione hili. Darasa hilo lina wanawake tu hakuna wanaume? Je, kama wanaume wapo wanashindwa test ni wanawake? vipi wanaume wanaoshindwa test je, nao wanafukuzwa shule? Ninavyoona, hapa kuna mchanganyiko wa mambo mengi. Kwanza, kama test ni ya darasa zima (wanaume na wanawake) iweje, washindwe wanawake tu? nini kinawatokea wanaume walioshindwa au wao hawashindwi hiyo test? Kama wanaume wanashinda hiyo test basi Dr. Barongo yupo sahihi kuwawajibisha walioshindwa test yake na mambo ya kuombana uroda yasitumike kama 'defense mechanism? Nawashauri wale wanaoshindwa test ya jamaa wakati wengine wanaifaulu kwanza waongeze bidii wasome na waishinde. Dr. Barongo atawakosa hawezi kuwakamata, sasa kama hausomi na unasubiri ukibabwa useme umeombwa uroda basi hayo ni majungu.
Niungane na Caroline Danzi, kwamba mida ya kulialia na kulalamam imepitwa na wakati. Simu zetu siu hizi zinarekodi sauti, mtegee simu atongoze then utakuwa na ushahidi. Au kubaliane naye nendeni guest house anayoipenda huku ukiwa umewasuka wakokota mikokoteni ili wawakute mle quest house ili badala ya kushughulikiwa wewe wamshughulikie huyo Dr. Barongo, atakoma hatarudia, Acha kulialia amka ujipiganie.
Tulione hilo kutongozwa kwa hila kupo lakini visingizio vipungue pale wanawake wanaposhindwa test kwa uzembe then wanatuambia si unajua nilimnyima......