Fedha za Radar Kurudishwa: Mgogoro kati ya BAE, TZ na UK

Huyo naibu Spika mwenyewe wameona ana uwezo kuliko Balozi wetu kweli?
Spika yuko vile, je, Naibu!

Membe yeye ana bahati mbaya kwamba hata usoni hana sura ya ufahamu kabisa! Maongezi yake yamekuwa kama anamuiga Che Guevara badala ya kuonyesha uwezo wake wa kutumia Diplomasia!
 
Haya ni marudio ya hoja ambayo imejadiliwa sana. Ukweli unabaki pale pale kwamba kama wewe umeibiwa lakini kwa sababu yoyote ile ukashindwa kumfuatilia mwizi wako, au ukashindwa kujua kwamba umeibiwa, akitokea whistle blower akakuambia na hata akafanikisha kurudishiwa mali yako, msamaria mwema huyo hajinyakulii haki ya umiliki wa mali hiyo.

Anaweza tu akaomba kushukuriwa lakini siyo kukupangia matumizi ya recoveries zako. Uingereza walifuatilia issue hii kwa sababu kampuni ya BAE ambayo ilihusika na wizi huu na yenyewe ilikuwa ina-face credibility problems kama serikali isingeingilia kati. Haikuwa favour kwa Tanzania japo Tanzania ilikuwa ni beneficiary ya ufuatiliaji huo.

Hakuna justification yoyote ya fedha hizi kutorejeshwa kwa aliyeibiwa na msimamo wa Membe na serikali ndiyo utashi sahihi na wanaoshangaa wanaendekeza ukoloni ambao hauna nafasi katika hili. Membe endelea kudai mpaka kieleweke!

Unatoa maelezo ya kizembe kuliko hata Membe. Mifano gani hiyo unayotuletea JF.
Mumeulizwa mara nyingi kwamba wezi walio kula njama za kuhamisha pesa hizo wako Tanzania, tena serikalini ktk ngazi za maamuzi. hujawaajibisha na hata huna niya ya kuwatia adabu. Unang'ang'ania urudishiwe pesa hizo.

Kwa maana nyingine unataka wezi hao wapange upya matumizi ya pesa hizo ktk serikali yako. Nosense!

Inaeleweka kwamba pamoja na BAE kulipa, sehemu ya pesa hizo ilichukuliwa na maafisa wa serikali yenu ya TZ, tena kwa makusudi kwa kukubaliana na mafisadi wengine na kuwekewa huko kwao. Leo hii unaanza kuziomba kwa ukorofi eti usipangiwe matumizi!

Kuna lolote unaloona kwamba litazuia pesa hizo kutotumika vibaya? Hata kwa sheria zetu TZ, kweli hujui mtoa rushwa na mpokeaji wote ni hatiani?
UK wamefanya la kwao wewe je huko TZ?
Hili nalo unahitaji masaa mangapi ya kufundishwa?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kampeni iliyoanza ya kuunga mkono uamuzi wa BAE, ijumuishe mwito wa kulaani spika wa bunge na wenzake kupoteza mamilioni ya fedha za walipa kodi katika kupeleka ujumbe wa watu wanane huko uingereza kufuatilia suala lisiokuwa na tija yeyote.
 
Huyo naibu Spika mwenyewe wameona ana uwezo kuliko Balozi wetu kweli?
Spika yuko vile, je, Naibu!

Membe yeye ana bahati mbaya kwamba hata usoni hana sura ya ufahamu kabisa! Maongezi yake yamekuwa kama anamuiga Che Guevara badala ya kuonyesha uwezo wake wa kutumia Diplomasia!

Mzee Mapesa ndiye wanayemwona mwenye kutoa ushawishi mkubwa? Njaa hii itawaweka pabaya
 
Something is wrong na nchi yetu, hivi kweli kuna umuhimu wa kutuma delegation kubwa yote hii? Kwanza Membe alikuwa huko juzi juzi tu, na je nini maana ya kuwa na balozi huko? hizi gharama nani anazilipia? na bado zikifika hizi pesa zinapitiliza kwenye warsha. Mkulima asiye na hata kinua mgongo, na ambaye ndo hela yake hii hana hata dawa katika zahanati.
Tunapeleka watu kwenda kupiga picha???
 
Kampeni iliyoanza ya kuunga mkono uamuzi wa BAE, ijumuishe mwito wa kulaani spika wa bunge na wenzake kupoteza mamilioni ya fedha za walipa kodi katika kupeleka ujumbe wa watu wanane huko uingereza kufuatilia suala lisiokuwa na tija yeyote.

Kumbe wabunge nani plus Membe, kusafiri daraja la kwanza, hoteli daraja la kwanza, posho za kujikimu, posho za vikao wanapokutana na BAE, posho wanapojipangia wenyewe kujadili namna ya kuwathibiti BAE, magari wanayokodi kwa ajili ya safiri, wakati huo huo wanahesabika wako kikazi hivyo posho ma mishahara ya ubunge inali palepale, huu wizi jamani hata hawana dhamiri.
 
Napata wasiwasi kama hawa jamaa wana lolote la kutusaidia kuhusu hili! sikuwasikia wakijadili lolote kuhusu hili njia nzima kuelekea London...
 
Wachambuzi kadhaa wanaona hili jambo kwa namna tofauti,wengine wakisema ni halali hizo pesa zilipwe kwa serikali ya tz moja kwa moja kwa sab ni jasho la watanzania,na kwamba Membe yupo sahihi
Mimi nalazimika kuamini kwamba tulikuwa na haki ya kufuatulia hizo hela kama inavyofanyika sasa hivi kama wahusika wote(naesema wote) waliohusika wangeshafikishwa kwenye mkono wa sheria
Kama tumekubali kujidhalilisha wenyewe kwa kushindwa kuwachukulia hatua wahusika nafikiri tukubali kudhalilishwa na Uingereza kwa namna wanavyotaka hizo hela zirejee kupitia NGO.
Kwa hiyo hata wakikataa mapendekezo ya serikali kwangu mimi ni sawa.
 
Naunga mkono uchambuzi wako
 
Hapo utakuta ni US $250 per head in posho! Hizo pesa bora zibaki hukohuko hata zitupwe kuliko kuwapa Serikali ya Kifisadi ili iende kwenye akaunti zao! Upuuzi mtupu mlikua wapi wakati wa kesi mbona hamkua na interest!!! Anyway muinjoi posho hiyo ndo iliyowapeleka huko, shopping kwa kwenda mbele rudini na masanduku matano kila mmoja:A S 114::A S cry:
hivi jamani kam serikali imeshindwa kuchukua hatua kwa wale waliokula hizo hela maana wanafahamika sasa leo serikali hiyo hiyo inataka hizo hela izichukue, BAE na sisi wavuja jasho wengine tutaamini vipi kama hazitaishia mifukoni mwa mafisadi wengine, maana tukija uliza baadae hela za zilizotoka BAE ziko wapi mbona zimeliwa itakuwa kama EPA, kwani hela zenu hizo mmelipia kodi mnauliza za nini, haziwahusu.
 
Wachambuzi kadhaa wanaona hili jambo kwa namna tofauti,wengine wakisema ni halali hizo pesa zilipwe kwa serikali ya tz moja kwa moja kwa sab ni jasho la watanzania,na kwamba Membe yupo sahihi
Mimi nalazimika kuamini kwamba tulikuwa na haki ya kufuatulia hizo hela kama inavyofanyika sasa hivi kama wahusika wote(naesema wote) waliohusika wangeshafikishwa kwenye mkono wa sheria
Kama tumekubali kujidhalilisha wenyewe kwa kushindwa kuwachukulia hatua wahusika nafikiri tukubali kudhalilishwa na Uingereza kwa namna wanavyotaka hizo hela zirejee kupitia NGO.
Kwa hiyo hata wakikataa mapendekezo ya serikali kwangu mimi ni sawa.

Kimsingi Membe hayuko sahihi kabisa kwa vile serikali haina macho wala masikio kwamba hela hizo walilipwa watu ambao ni viongozi wa serikali na serikali imeogopa hata kuwahoji tu hao watanzania, sasa leo itakuwa ni aibu kwa BAE kuipa serikali hizo hela maana ina uhakika kama wengine tulio nao vichwani kwamba hiyo hela italiwa na wajanja, bora ziende kwenye NGO zinazotoa misaada kwa watanzania. Shame on you Membe kwa kujifanya kiziwi na kipofu
 
Something is wrong na nchi yetu, hivi kweli kuna umuhimu wa kutuma delegation kubwa yote hii? Kwanza Membe alikuwa huko juzi juzi tu, na je nini maana ya kuwa na balozi huko? hizi gharama nani anazilipia? na bado zikifika hizi pesa zinapitiliza kwenye warsha. Mkulima asiye na hata kinua mgongo, na ambaye ndo hela yake hii hana hata dawa katika zahanati.
Tunapeleka watu kwenda kupiga picha???

Ndo yale yale ya kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku. Nina amini zikijumlishwa hela zilizotumika eti kwenda Uingereza kuufuatilia BAE ulipwaji wa hela hizo unaweza kukuta ni zaidi ya robo ya hizo hela maana kila wakati ujumbe unaoenda ni mkubwa, kuna gharama za tiketi, posho, hotel, magari ya kukodi, functions kwa balozi n.k
 
Haya ni marudio ya hoja ambayo imejadiliwa sana. Ukweli unabaki pale pale kwamba kama wewe umeibiwa lakini kwa sababu yoyote ile ukashindwa kumfuatilia mwizi wako, au ukashindwa kujua kwamba umeibiwa, akitokea whistle blower akakuambia na hata akafanikisha kurudishiwa mali yako, msamaria mwema huyo hajinyakulii haki ya umiliki wa mali hiyo.

Anaweza tu akaomba kushukuriwa lakini siyo kukupangia matumizi ya recoveries zako. Uingereza walifuatilia issue hii kwa sababu kampuni ya BAE ambayo ilihusika na wizi huu na yenyewe ilikuwa ina-face credibility problems kama serikali isingeingilia kati. Haikuwa favour kwa Tanzania japo Tanzania ilikuwa ni beneficiary ya ufuatiliaji huo.

Hakuna justification yoyote ya fedha hizi kutorejeshwa kwa aliyeibiwa na msimamo wa Membe na serikali ndiyo utashi sahihi na wanaoshangaa wanaendekeza ukoloni ambao hauna nafasi katika hili. Membe endelea kudai mpaka kieleweke!

Kama Tanzania wanafuatialia hizi pesa za BAE tafsiri yake ni kwamba wamekubali waliibiwa/rubuniwa na BAE systems. Sasa, je kama ndivyo wamechukuwa hatua zozote dhidi ya waliohusika katika wizi huo (kwa upande wa Tanzania)?
 
Haya ni marudio ya hoja ambayo imejadiliwa sana. Ukweli unabaki pale pale kwamba kama wewe umeibiwa lakini kwa sababu yoyote ile ukashindwa kumfuatilia mwizi wako, au ukashindwa kujua kwamba umeibiwa, akitokea whistle blower akakuambia na hata akafanikisha kurudishiwa mali yako, msamaria mwema huyo hajinyakulii haki ya umiliki wa mali hiyo.

Anaweza tu akaomba kushukuriwa lakini siyo kukupangia matumizi ya recoveries zako. Uingereza walifuatilia issue hii kwa sababu kampuni ya BAE ambayo ilihusika na wizi huu na yenyewe ilikuwa ina-face credibility problems kama serikali isingeingilia kati. Haikuwa favour kwa Tanzania japo Tanzania ilikuwa ni beneficiary ya ufuatiliaji huo.

Hakuna justification yoyote ya fedha hizi kutorejeshwa kwa aliyeibiwa na msimamo wa Membe na serikali ndiyo utashi sahihi na wanaoshangaa wanaendekeza ukoloni ambao hauna nafasi katika hili. Membe endelea kudai mpaka kieleweke!

MIMI naamini kabisa kama wewe si mmojawapo wa kundi lilelile la mafisadi wa rada, basi uwezo wako wa kuchambua mambo ni sawa na mjukuu wangu anaeanza kusoma vidudu leo hii, duuu! jamani meneno yako hata mwanao akisoma atakudharau
 
Tangu asubuhi TBC imekuwa ikitangaza ya kwamba ujumbe wa Tanzania upo Uingereza kufuatia fidia ya malipo ya rada.

Kwa kumbu kumbu zangu hii si mara ya kwanza kwa waziri Membe kutuma ujumbe wa aina hiyo huko uigereza kwaajili ya malipo husika. Suala la kujiuliza ni kwamba kama Membe mwenyewe alikwisha wasilisha suala hilo kwa serikali ya uingereza kwa kupitia waziri wa nje mwenzake wa nchi hiyo, anawezaje tena kuanzisha mazungumzo ya moja kwa moja na kampuni husika!

Diplomasia ya aina hiyo aliiona wapi?

Swali lingine kwanini wakati habari zilipoanza kuvuja ya kwamba Tanzania iliuziwa rada kwa bei mbaya, mbona hakuwa anajishugulisha kutoa ushirikiano wake katika kutafuta ukweli wa tuhuma hizo, iweje sasa wakati mambo yamekamilika awe mwepesi kutaka kuvuna asikopanda.

Katika hali halisi kukaa kimya kwa serikali ya Tanzania wakati suala hili linafanyiwa uchunguzi kumeiondolea uhalali wowote wa kudai tuzo iliyotolewa kwa suala hilo. Hivyo wahusika wana haki ya kuunda chombo chao kitakachobuni njia muafaka wa kufikisha tuzo hiyo kwa walengwa ambao ni watanzania.

Katika hali hiyo ni matumizi mabaya ya fedha za umma kuendelea kuingia gharama za mara kwa mara kwaajili ya kwenda uingereza eti kufuatilia malipo hayo wakati tuna ubalozi huko.

===================
KATIKA PICHA:

wabunge1.jpg

Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb.) akiongea na Naibu Spika wa Bunge la uingereza, Mhe. Nigel Evans (Mb) katikati ni Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania. Ujumbe wa Wabunge wanne wa Tanzania unaongozwa na Naibu spika. (Picha Assah Mwambene)
wabunge2.jpg

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai akiteta jambo na Spika wa Bunge la Kenya walipokutana katika Bunge la Uingereza jana. Waheshimiwa Wabunge wako nchini Uingereza kufuatilia malipo ya zaidi ya paundi milioni 29 kutoka BAE System baada ya Mahakama nchini hapa kuiamuru kampuni hiyo kuilipa Tanzania baada ya kugumdulika kwamba kampuni hiyo iliongeza bei ya ununuzi wa Radar.

wabgunge3.jpg

Balozi wa Tanzania Uingereza, Mheheshimiwa Peter Kallaghe akiteta jambo na Waheshimiwa Wabunge wa Tanzania, Jobu Ndugai (Naibu Spika), Mussa Azzan Zungu (Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mhe. Angela Kairuki

Hao jamaa waache uzushi, ni bora wangetuaga tu kwamba wanakwenda kusafisha macho huko Uingereza kuliko kujidai wanafuata chenji. Inawahusu nini? Kama inawahusu si tungeona jitihada zao kuwashughulikia watuhumiwa wa sakata la rada? Hovyo kabisa! Viongozi wa nchi hii wanatudhalilisha sana sasa! Hivi wanatumia nini kufikiri?????
 
Haya ni marudio ya hoja ambayo imejadiliwa sana. Ukweli unabaki pale pale kwamba kama wewe umeibiwa lakini kwa sababu yoyote ile ukashindwa kumfuatilia mwizi wako, au ukashindwa kujua kwamba umeibiwa, akitokea whistle blower akakuambia na hata akafanikisha kurudishiwa mali yako, msamaria mwema huyo hajinyakulii haki ya umiliki wa mali hiyo.

Anaweza tu akaomba kushukuriwa lakini siyo kukupangia matumizi ya recoveries zako. Uingereza walifuatilia issue hii kwa sababu kampuni ya BAE ambayo ilihusika na wizi huu na yenyewe ilikuwa ina-face credibility problems kama serikali isingeingilia kati. Haikuwa favour kwa Tanzania japo Tanzania ilikuwa ni beneficiary ya ufuatiliaji huo.

Hakuna justification yoyote ya fedha hizi kutorejeshwa kwa aliyeibiwa na msimamo wa Membe na serikali ndiyo utashi sahihi na wanaoshangaa wanaendekeza ukoloni ambao hauna nafasi katika hili. Membe endelea kudai mpaka kieleweke!

kuna kitu unajichanganya ni nani mmiliki wa kodi au mali za umma?
kama una amini ni serikali basi huko sahihi , ila sio mtazamo sahihi kwa sababu serikali sio wamiliki
wa mali za umma ila sisi wananchi ndio wamiliki wake, hawa wote wawili serikali na BAE sio wamiliki wa hiyo mali

na hapo ndipo nawapa hongera BAE kwa maana wao wameamua kuirudisha hiyo pesa kwa mmiliki wake
ambaye ni sisi wananchi.
hivyo hakuna walichofanya kosa.
 
Something is wrong na nchi yetu, hivi kweli kuna umuhimu wa kutuma delegation kubwa yote hii? Kwanza Membe alikuwa huko juzi juzi tu, na je nini maana ya kuwa na balozi huko? hizi gharama nani anazilipia? na bado zikifika hizi pesa zinapitiliza kwenye warsha. Mkulima asiye na hata kinua mgongo, na ambaye ndo hela yake hii hana hata dawa katika zahanati.
Tunapeleka watu kwenda kupiga picha???

kwanza bunge linajiusisha na hii issue kivipi?
kama wao wana huruma na watanzania mbona hakuna hata mbunge mmoja anayesema tuchukuwe hatua kwa waliohusika hata kwa kufukuza kazi wwale ambao bado wako serikali kama watumishi wa umma
 
Haya ndio maajabu. Tanzania haijachukua hatua yoyote kwa fisadi aliehusika na hii kashfa ya rada inayuhusu BAE lakini wanatuma ujumbe mkubwa kuulizia fidia kutoka BAE !!! hiki kiini macho.
 
Wanasiasa bana, Ndungai anasema watazitumia kununua vitabu. madawati na watajenga nyumba za walimu. Sasa kama ndio hivyo bora jamaa wawape vitabu na hayo madawati hukohuko kisha waseme wanataka nyumba ngapi za waalimu ili jamaa watujengee kabisa hizo nyumba za maticha. Wabongo tumejaliwa kuongea ila matendo sifuri. Bora zibaki hukohuko, naandika email sasa hivi
 
Back
Top Bottom