Fedha za Manji bado zachunguzwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Tuesday, July 14, 2015

Manji-14July2015.jpg

Mfanyabiashara Yusufu Manji.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema linaendelea kufanya uchunguzi wa mamilioni ya fedha zilizokamatwa katika Hoteli ya St. Gaspar mjini hapa, zinazodaiwa kuwa zilitolewa na Mfanyabiashara Yusufu Manji, kwa nia ya kuwahonga waliokuwa wajumbe wa vikao vya maamuzi vya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, David Misime, jana alisema kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo na kuahidi kutoa taarifa kamili kwa vyombo vya habari.

"Bado tunalishughulikia, subirini taarifa ikikamilika, tutaitoa tu, msiwe na wasiwasi wala msisababishe, tufanye kazi kwa shinikizo, " alisisitiza Kamanda Misime, wakati akizungumza na NIPASHE jana jioni.

Kwa upande wake, Kamanda wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa(Takukuru), Emma Kuhanga, aliliambia NIPASHE jana jioni kuwa pamoja na kupata taarifa kuhusiana na tukio hilo kutoka kwa vyanzo mbalimbali, hawako tayari kulizungumzia kwa sababu linachunguzwa na Jeshi la Polisi.

Kuhanga alisema wao polisi wanachunguza tukio hilo kwa kuwa maofisa wa taasisi yao (Takukuru) hawakuwapo kwenye eneo la tukio na kwamba kwa kawaida polisi pia hushughulikia makosa ya rushwa.

"Ikitokea ushahidi ukakamilika, kwakuwa sisi tuna prosecutor (mwendesha mashtaka) wetu, polisi wakiona umuhimu wa kuhamishia suala wanaloshughulikia ambalo linahusu rushwa, wanaweza kulihamishia kwetu kwa kufahamu kuwapo kwa chombo maalumu kinachoshughulikia makosa ya rushwa tu, " alisema Kuhanga.

Fedha hizo zilikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli hiyo iliyopo eneo la Kisasa, zikiwa mikononi mwa mfanyakazi wa Kampuni ya Quality Group (T), Amit Kevaramani, akiwa na hati ya kusafiria M1470774 ya nchini India.

Kiasi cha fedha kilichokamatwa ambacho hakijathibitika mara moja kinadaiwa kufikia Sh. 725,2050,000.

Inadaiwa kuwa fedha hizo zilikamatwa baada ya kuwapo kwa watu walioshtukia mwenendo wa mfanyakazi huyo wa kampuni ya Manji, aliyeonekana akihamisha mabegi makubwa mawili na kupeleka kwenye gari lililokuwa limeegeshwa nje ya hoteli hiyo likiwa aina ya Toyota Land Cruiser.

Katika hoteli hiyo ambayo kulikuwa na wajumbe wengi wa Mkutano Mkuu, na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM inadaiwa kuwa mamilioni hayo yalikuwa yanapelekwa kwa kambi ya mmoja wa wagombea watano waliopitishwa na Kamati Kuu wiki iliyopita kuwania kuteuliwa kuwa wagombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.


CHANZO: NIPASHE
 
Danganya toto wanavuta muda ili walizime hili kimya kimya kisha warudishe pesa zake. Hizi pesa zingetumika kununulia madawati katika mikoa 7 yenye hali mbaya kwa Wanafunzi kukaa chini kila mkoa milioni 100
 
ndo hela za lowasa alizokuwa anawaambia watu kuwa anachangiwa na marafiki zake? marafiki wenyewe ndo hawa wahindi wezi? kazi tunayo.
 
hiv bado mnaziamini habari za gesi retu ra porice....!! tangu rini rikachunguza fweza ndefu kama iree aisee??
 
ndo hela za lowasa alizokuwa anawaambia watu kuwa anachangiwa na marafiki zake? marafiki wenyewe ndo hawa wahindi wezi? kazi tunayo.
Mkuu umeambiwa zilikuwa za mmoja wa wale walioingia tano bora......sasa hapo Lowasa anaingiaje?
 
Na yule kijana mdogo aliyekamatwa nazo yuko wapi, polisi au kapata dhamana!?
 
Membe ndio aliopitishwa ktk tano bora, ndio fedha zake... sio Lowassa.. watu wana vichwa vimejaa makamasi humu
 
Danganya toto wanavuta muda ili walizime hili kimya kimya kisha warudishe pesa zake. Hizi pesa zingetumika kununulia madawati katika mikoa 7 yenye hali mbaya kwa Wanafunzi kukaa chini kila mkoa milioni 100
Umesema kweli hao polisi wanatuzuga tu kuhusu hayo mamilioni ya Manji.

Jeshi letu halina ubavu wa kumkamata wala kumfungulia mashitaka mhindi huyo ambaye ni 'swaiba' mkuu wa Mkulu.

Si mnakumbuka wakati ule wa sakata la EPA?

Huyo huyo Manji alikuwa miongoni wa watuhumiwa wakuu wa wizi huo wa mabilioni ya shilingi.

Lakini wote si tunakumbuka namna JK alivyotoa msamaha kwa 'vibaka' hao wa pesa za EPA akiwemo Manji na akawaeleza kuwa wakizirejesha tu pesa walizoiba za EPA, yeye Mkulu atawasamehe, na ndiyo maana tunaendelea kumwona huyo Manji akiendelea kutamba na kuendelea kumwaga takrima kwa viongozi wa Sisiemu?

Kwa tafsiri nyingine ni kuwa huyo Manji ni UNTOUCHABLE na vile vile yupo above law!
 
Mkuu umeambiwa zilikuwa za mmoja wa wale walioingia tano bora......sasa hapo Lowasa anaingiaje?
Usishangae sana sifongo, inawezekana huyo jamaa anatumia 'masaburi' yake kufikiri, ndiyo maana ameshindwa kubaini kuwa wakati pesa hizo za Manji zinakamatwa tayari jina la Lowassa lilikuwa limeshakatwa na CC, kwa hiyo hayo mamilioni yalikuwa yamepangwa kwenda kugawiwa kwa wajumbe wa NEC ambako jina la 'bamdogo' lilikuwa limepenya huko.

Lakini kutokana na TAKUKURU kuzipiga tanchi pesa hizo na hivyo wajumbe wa NEC kuukosa 'mshiko' huo, jamaa akajikuta anaangukia pua kwa kuburuza mkia kati ya wagombea wale 5 waliotinga kwenye kikao cha NEC.
 
Kadri siku zinavyokwenda hizo pesa zinageuka na mwisho wa siku tutaambiwa, zote zilikuwa feki na thamani yake siyo 700M bali Buku 7!

Tanzania kuna mazingaombwe mengi sana. Tusubiri mtashuhudia kabla Dk. Yohana Alcohol Padlocks hajaingia ikulu.
 
nngu007

Saa nyingine kuna wakati Mungu huamua kuanika uovu wa mtu hadharani! Mwezi haujapita tangu siku Manji alipoitwa kwenye mdahalo ambapo alimtuhumu Mengi kuwa anamzushia tuhuma za rushwa. Tena alienda mbali na kusema ataacha madaraka yanga kutokana na kuchafuliwa jina lake licha ya kazi nzuri anayofanya. Natamani wamwite tena na wamwulize maswali yaleyale
 
Last edited by a moderator:
Huyu huyu si ndio aliye usishwa na Kampuni hewa ya Kagoda Agricalture iliyemweka rais Kikwete madarakani!! Kwa kifupi huyu na Rostam ndio wanatupatia rais na baadhi ya wabunge!

Kagoda alimsingizia marehemu baba yake. Hii sijui atamsingizia nani?
 
Back
Top Bottom