Fedha za Manji bado zachunguzwa

Mwenye hela karudishiwa hela zake maana hapakuwa na ushahidi kuwa alikuwa anatoa rushwa
 
Mkuu hebu jaribu kufuatilia matukio vizuri
mkuu huyo lowasa namemfahamu kwa kiasi chake. akiwa arusha watu walikula hela za kutosha tu. ilikuwa ukiwa tayari gari yako kuwepo kwenye msafara unapata mshiko wa kutosha, pikipiki nao pia. kwa kifupi kagawa sana pesa huyo jamaa. nayaandika haya nikiwa nawafahamu kwa majina na sura rafiki zangu waliofaidika na pesa ya huyu jamaa. nilikuwa nikiwauliza swali moja tu ambalo hakuna hata mmoja aliyejaribu kulijibu; ''hivi hizi hela anazogawa lowasa zitarudi vipi''hakuna aliyenijibu. kwa hiyo naelewa ninachokisema.
lakini hata hivyo nikiri kuwa jamaa anapiga kazi tatizo lake mwizi.
 
Mkuu sipingi hayo ambayo pengine uliyashuhudia mwenyewe. Ila kwa muda ambao hizo pesa za Dodoma zinakamatwa ni kuwa jina la Lowasa tayari lilikuwa lishakatwa hivyo issue ya matumizi ya pesa kwake haikuwepo. Ndio maana inasemwa ni za Maembe. Hapa nilipo kuna waarabu wamebakia na mapicha yake ambayo alitaka kuanza kuprint.
 
Mkuu umeambiwa zilikuwa za mmoja wa wale walioingia tano bora......sasa hapo Lowasa anaingiaje?
lakini zimekutwa kwenye hoteli ambayo wapambe wa lowasa walikokuwa wamepanga. Anyway, unaweza kuwa sahihi pia. hata hivyo kuupata ukweli ni shida maana kila mmoja anaandika kwa kuvutia upande wake.
 
Mkuu hebu jaribu kufuatilia matukio vizuri

Lowasa hausiki hapo
mhusika amekutwa akiwa kwenye hotel walikokuwa wamepanga wapambe wa lowasa. inawezekana kabisa zikawa sio zake japo ushahidi wa mazingira hayo ninayowaeleza yanaonesha mhusika.
anyway, hata hivyo ni vigumu sana kuujua ukweli maana watu wanaandika kwa kuvutia upande wao. hatuna source neutral. mfano kama mmawia yeye anajulikana siku zote ni team lowasa na chadema kwa hiyo sitegemei habari yoyote anti-lowasa kutoka kwake.
 
Mkuu tafadhali nitake radhi,tukirudi kwenye hoja nikuwa huyo mhindi ni swahiba wa baba riz moko,na huyo mgombea urais aliye mwachia jimbo nape ni maswahiba na mkulu,
 
Wewe subiri soon utaambiwa hazikuwa pesa ni karatasi chezea wabongo, Sijui nani atadhibitisha kuwa ni pesa halali kabla ya kujua ni za nani
 
Nashangaa kitu kimoja, kama kweli ni fedha za kuhonga kwanini hawakusubiri wamkamate redhanded wakati anahonga ili wawe na solid proof? Ushahidi kuwa ni fedha za kuhonga uko wapi wakati alikuwa bado hajahonga (yaani alikuwa in the process na activity yenyewe ilikuwa bado kabisa)? Mmh sijui kama kesi hii unaweza kui-prosecute!!!!
nngu007
 
Last edited by a moderator:
Huyu huyu si ndio aliye usishwa na Kampuni hewa ya Kagoda Agricalture iliyemweka rais Kikwete madarakani!! Kwa kifupi huyu na Rostam ndio wanatupatia rais na baadhi ya wabunge!

Kagoda alimsingizia marehemu baba yake. Hii sijui atamsingizia nani?
mkuu wa kagoda ni rostam sio manji
 
Danganya toto wanavuta muda ili walizime hili kimya kimya kisha warudishe pesa zake. Hizi pesa zingetumika kununulia madawati katika mikoa 7 yenye hali mbaya kwa Wanafunzi kukaa chini kila mkoa milioni 100
Tayari zimerudishwa kwa mwenyewe hakuna uthibitisho wa rushwa tembelea Mwanahalisi
 
Pesa ni za Manji tusimungunye maneno, sasa Manji akamatwe aseme kwanza kwa nini abebe pesa kwenye mabegi na amtume mfanyakazi wake na halafu akikie walipokuwa wajumbe wa mikutano muhimu kama ile. Ila kwa vile Manji akikatiwa bilioni 40 wakati ule wa mkuu wa kaya kuusaka, labda ndo zilikuwa zimebaki kazileta kurudisha kwa wenyewe. Kwa maneno mengine EPA ilikuwa ni hao hao jamaa waliokuwa wanaishi naye hapo St. Gaspar....sjui nini kinachunguzwa...kukamatwa na pesa zile zote ilikuwa lazima mtu awe ndani na si vinginevyo.
 
Saa nyingine kuna wakati Mungu huamua kuanika uovu wa mtu hadharani! Mwezi haujapita tangu siku Manji alipoitwa kwenye mdahalo ambapo alimtuhumu Mengi kuwa anamzushia tuhuma za rushwa. Tena alienda mbali na kusema ataacha madaraka yanga kutokana na kuchafuliwa jina lake licha ya kazi nzuri anayofanya. Natamani wamwite tena na wamwulize maswali yaleyale

Mengi ndio aliyekataa kwenda na ni Manji ndie aliyeandaa mdahalo!
 
Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi kuhusiana na fedha alizokamatwa nazo mfanyabiashara na kuelezwa kwamba ni za Mkurugenzi Mtendaji Mkuu, Yusuf Manji anayemiliki kampuni ya Quality Group.

Mitandao na vyombo vingine vya habari vilieleza kuwa fedha hizo zilitoka katika kampuni hiyo ya Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Yanga na kupeleka Dodoma kuhusiana na suala la uchaguzi wa mgombea yupi ashinde ugombea wa Urais katika Chama cha Mapinduzi (CCM).

Baada ya uchunguzi kukamilika, Kamanda wa Polisi Dodoma, amezungumza na waandishi na kufaganua hivi:

"Napenda kutoa taarifa fupi kuhusu tukio lililotokea tarehe 11/07/2015 majira ya saa 10:00 hrs huko katika Hoteli ya St. Gasper hapa mjini Dodoma, kuwa wananchi walitoa taarifa majira ya saa 10:00 hrs kwamba kuna mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia amekamatwa na wananchi akiwa na fedha nyingi na kuna vurugu kubwa. Baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifika eneo la tukio ili kuona kama taarifa hizo ni za kweli.

"Askari walithibitisha kuwa ni kweli walimkuta mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia ambaye alijulikana kwa jina la AMIT KEVALRAMANI mwenye umri wa miaka 31, Mhindi, Mfanyabiashara, Mkazi wa Dar es Salaam akiwa na fedha kiasi cha Tshs. 722,500,000/= ambacho alipohojiwa alisema kuwa tarehe 10/07/2015 alifika Dodoma kwa ajili ya ununuzi wa mazao ya nafaka.

"Alipofika Dodoma tarehe 10/07/2015 majira ya asubuhi alifikia katika Hoteli ya St. Gasper na tarehe 11/07/2015 aliamua kurudisha fedha benki kutokana na kuona mkusanyiko wa watu wengi wasioeleweka na wenye viashiria vya vurugu.

"Akiwa katika harakati ya kurejesha fedha hizo benki, ndipo kundi la watu waliokuwa katika eneo la Hoteli ya St. GASPER walimtilia mashaka na kumzuia asiondoke na ndipo taarifa zilitolewa polisi.

"Mashaka ya watu hao yalitokana na vuguvugu za kisiasa/mchakato wa uchaguzi kati ya makundi mbalimbali kuwa kuna watu wanahonga wajumbe. Taarifa za aina hiyo ambazo hata Jeshi la Polisi lilikuwa limepokea bila uthibitisho.

"Katika tukio hili na uchunguzi tulioufanya tumebaini kuwa hakuna kosa la jinai lililothibitika licha ya kukutwa na kiasi hicho cha fedha, tuhuma za rushwa ambazo ndiyo zilikuwa msingi wa ukamataji wa mtu huyo hazikuthibitika, kwa kuwa hakuna aliyeona akizigawa fedha hizo wala hakuna aliyedai kushawishiwa au kugawiwa fedha hizo.

"Aidha, imethibitika fedha hizo ni mali yake halali na kwa kuwa hakuna ushahidi mwingine uliyo thibitisha vinginevyo amerejeshewa fedha zake," alisema kamanda huyo.
 
ndo hela za lowasa alizokuwa anawaambia watu kuwa anachangiwa na marafiki zake? marafiki wenyewe ndo hawa wahindi wezi? kazi tunayo.

Na hivi hao marafiki hakuwataja kwa majina..., inawezekana na huyu nae akawemo!
Mbaya sana alipotuachia kazi ya kudodosa ni akina nani hao anaowatia marafiki zake..., ndio kama hivi sie tunajaza tu humo humo!
 
Mkuu tafadhali nitake radhi,tukirudi kwenye hoja nikuwa huyo mhindi ni swahiba wa baba riz moko,na huyo mgombea urais aliye mwachia jimbo nape ni maswahiba na mkulu,
nisome vizuri kwenye post yangu uliyojibu. wewe sio reliable source kwa sababu uko-bias. mbona huelewi. hata ungesema ukweli wa aina gani hutaaminika. kwa wewe utomaso ni lazima. huchelewi kuingiza mtu chaka.
 
Mkuu sipingi hayo ambayo pengine uliyashuhudia mwenyewe. Ila kwa muda ambao hizo pesa za Dodoma zinakamatwa ni kuwa jina la Lowasa tayari lilikuwa lishakatwa hivyo issue ya matumizi ya pesa kwake haikuwepo. Ndio maana inasemwa ni za Maembe. Hapa nilipo kuna waarabu wamebakia na mapicha yake ambayo alitaka kuanza kuprint.
wengine wanasema ilikuwa kwa ajili ya kwenda kuanzisha riot kwenye mkutano jina la lowasa lirudishwe. kama utakuwa na kumbukumbu nzuri utakuwa uliwaona au kuwasikia vibaraka wake akina nchimbi, kimbisa, na sofia wakilianzisha kuanzia pale tu walipotoka kwenye kikao kuwa taratibu hazikufuatwa.
 
Mi nashindwa kuelewa kwani hizo pesa ni za aliekatwa Mwanzo au katikati?
wengine wanasema za aliyekatwa katikati. ila wengine wanasema aliyekuwa wa mwanzo.
binafsi naamini zitakuwa za yule wa mwanzo maana lengo lilikuwa kuwahonga baadhi ya wafuasi wake walianzishe palepale kuwa jina lililokatwa lirudhishwe na mchakato uanze upya. kama utakumbuka hata wakati kikwete akiingia ndani watu walianza kumuimbia juu ya yule mgombea wao pendwa.
 
Pesa ni za Manji tusimungunye maneno, sasa Manji akamatwe aseme kwanza kwa nini abebe pesa kwenye mabegi na amtume mfanyakazi wake na halafu akikie walipokuwa wajumbe wa mikutano muhimu kama ile. Ila kwa vile Manji akikatiwa bilioni 40 wakati ule wa mkuu wa kaya kuusaka, labda ndo zilikuwa zimebaki kazileta kurudisha kwa wenyewe. Kwa maneno mengine EPA ilikuwa ni hao hao jamaa waliokuwa wanaishi naye hapo St. Gaspar....sjui nini kinachunguzwa...kukamatwa na pesa zile zote ilikuwa lazima mtu awe ndani na si vinginevyo.

Mkuu hii inchi siya kidikteta,na mtu kusafirisha fedha zake siyo dhambi unajuwaje kama alikuwa anaenda kulipa mishahara?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom