JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Akifafanua hali ya sintofahamu inayoendelea kuhusu mchakato wa uwekezaji unaendelea kati ya Klabu ya Simba na mwekezaji Mohamed Dewji ‘Mo’, Mkurugenzi Mkuu Tume ya Ushindani (FCC), William Erio amesema kinachoangaliwa na watu wengi ni upande wa Mwekezaji na kusahau kuhusu kile kinachotakiwa kufanywa na Klabu ya Simba.
Amesema “Walipewa masharti ya Mwekezaji na yale ya Simba, walipokamilisha tukatoa cheti kuwa muungano umepitishwa na klichoombwa kimeridhiwa, kinachofuata ni utekelezaji.”
Ameongeza “Wiki mbili zilizopita upande wa Klabu (Baraza la Wadhamini wa Klabu) waliitwa RITA (Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini) wakitakiwa kuweka Hati za Jengo la Klabu zote ziwe mali mali ya Simba Sports Club Limited, sijajua nini kimeendelea huko.”