FBI ndani ya Tanzania, kazi ipo

FBI ndani ya Tanzania, kazi ipo

Nkobe

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2013
Posts
2,230
Reaction score
3,332
MAOFISA wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamekubali kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi yaliyotokea Zanzibar Februari 17, mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizopatikana jana maofisa hao wako nchini na tayari wamekutana na baadhi ya viongozi wa Serikali kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.

Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa maofisa hao walikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kwa ajili ya kuangalia ni namna gani watafanya shughuli zao katika upelelezi huo.

Kutua kwa maofisa hao kumekuja baada ya kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete katika salamu zake za rambirambi baada ya mauaji ya Padri Mushi kuwa ameliagiza Jeshi la Polisi kutumia nguvu zake zote pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama vya hapa nchini na mashirika ya upelelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji hayo.

Pamoja na ushiriki wa FBI, pia Serikali inazungumza na nchi nyingine rafiki ili kushirikiana nao katika upelelezi ya matukio mengine ya mauaji ya hivi karibuni.

Taarifa zinaeleza kuwa maofisa wa Serikali wamezungumza na taasisi za upelelezi za nchi tano ili kuongeza nguvu katika kazi hiyo.
Taasisi nyingine inayotajwa kwamba huenda ikashiriki katika uchunguzi huo ni Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya Uingereza ya Scotland Yard.

Hatua hizi zinakuja baada ya Dk Nchimbi kutoa tamko la Serikali, Jumapili iliyopita, akidai kuwa mauaji ya Padri Mushi yalikuwa ya kigaidi hivyo Serikali itachukua hatua kali kuhakikisha waliohusika wanakamatwa.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa Serikali ya Tanzania kushirikiana na asasi za kimataifa katika ku chunguza matukio ya uhalifu na yale ya kigaidi.
Hii itakuwa mara ya pili kwa FBI kuja nchini kufanya operesheni kubwa ya upelelezi. Mwaka 1998, walifika kuchunguza kulipuliwa kwa Ubalozi wa Marekani na kugundua ilikuwa kazi ya Kundi la Al-Qaeda.

Pia mwaka 1984 walikuja wapelelezi kutoka Scotland Yard kuchunguza kuungua kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima alithibitisha Serikali kuanza mazungumzo na mashirika mbalimbali ya upelelezi duniani kwa ajili ya kushirikiana nayo kuchunguza mauaji ya Padri Mushi.

Alisema tayari wameanza kufanya mazungumzo na mashirika hayo kutoka nchi mbalimbali, lakini alisema ni mapema mno kuyataja... "Ila tukikamilisha kila kitu tutawaiteni na kuwaeleza hatua tuliyofikia, ila tumeanza kufanya mazungumzo nayo. Kama unavyojua Rais Kikwete alitoa agizo hilo, sisi tumeanza kulitekeleza."

Waziri Silima alisema kwanza wataanza kuchunguza mauaji ya Padri Mushi... "Tutaanza kuchunguza kwanza chanzo cha mauaji haya ili tujue kila kitu."

Watuhumiwa wakamatwa
Polisi Zanzibar inawashikilia watu kadhaa wakihusishwa na mauaji ya Padri Mushi.

"Tumekamata watu kadhaa kuhusiana na kifo cha Padri na tunaendelea kuwahoji na wengine tutawaachia," alisema Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa jana.


Source: Mwananchi
 
Tumeshindwa yote wapi TZ ya usalama wa taifa madhubuti?
 
Mkuu nikiwa kama raia wa tanzania sikubali hata mara moja kuhusiana na hili.hii siyo ishara nzuri ni bora vyombo vyetu vikafanya kazi ndo wakihitaji msaada ndo wawaite wenzetu.sikubali hata mara moja na nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa vyombo vyetu vimeshindwa nina imani navyo sana.

Ila nadhani tuwe watu makini katika kuhakikisha maamuzi mengine ya kisiasa hayatuadhiri mustakabathi wa nchi yetu. Hii natolea mfano kwa wenzetu wa kenya wao walikataa mara nyingi hata kama ulibahatika kumsikiliza wagombee wa urais kwenye mdahalo walitaka kwanza wale watu waliopelekwa hague watendewe haki kenya na sio the hague. Lazima tuvipe kipaumbele vyombo vyetu kwanza ndo tukishindwa tuombee msaad. Tanzania nakupenda sana
 
Na baadae serikali itueleze imetumia fedha kiasi gani kuwaleta hao FBI na wamesaidia mambo gani ambayo sisi tusingeyaweza katika kuwakata hao wahusika. Wasije wakawa wameletwa halafu wanatembezwa mbuga za wanyama.
 
mkuu nikiwa kama raia wa tanzania sikubali hata mara moja kuhusiana na hili.hii siyo ishara nzuri ni bora vyombo vyetu vikafanya kazi ndo wakihitaji msaada ndo wawaite wenzetu.sikubali hata mara moja na nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa vyombo vyetu vimeshindwa nina imani navyo sana.ila nadhani tuwe watu makini katika kuhakikisha maamuzi mengine ya kisiasa hayatuadhiri mustakabathi wa nchi yetu.hii natolea mfano kwa wenzetu wa kenya wao walikataa mara nyingi hata kama ulibahatika kumsikiliza wagombee wa urais kwenye mdahalo walitaka kwanza wale watu waliopelekwa hague watendewe haki kenya na sio the hague.lazima tuvipe kipaumbele vyombo vyetu kwanza ndo tukishindwa tuombee msaad.tanzania nakupenda sana

Haya na mimi nakubaliana na wewe, sasa kwa pamoja tujiulize ni lini vyombo veytu viliwahi kufanya kazi nzuri? Ni kwa kiasi gani tunaviamini? Vyombo vyetu vipo kidili sana kuanzia kupeana madaraka mpaka utendaji. Viongozi wanawapa madaraka kwa kuwadanganyishia nao wanafanya kazi kwa kuwadanganyishia.
 
Yaaani tunashindwa kumkamata hata muuaji hadi tuite FBI?? Kwani ule "mkono mrefu wa serikali" ulikatika? au sikuhizi umepooza au umepata kiharusi? au ni mrefu tu kwa wanachadema??? Hahahahahaaaaa kazi ipo
CC: zumbemkuu MANI saudari

We acha tu tusaidiwe maana wenyewe tumeshindwa kujisaidia.
Ila ujue hawa jamaa hawajagi kwa shughuli moja.
Kuishi Tz yataka moyo.
 
We acha tu tusaidiwe maana wenyewe tumeshindwa kujisaidia.
Ila ujue hawa jamaa hawajagi kwa shughuli moja.
Kuishi Tz yataka moyo.
Hii mishenzi inaanza kutuletea taabu, ona sasa serikali inaingia ktk garama kwa sababu ya wapuuzi hawa.
 
Yaaani tunashindwa kumkamata hata muuaji hadi tuite FBI?? Kwani ule "mkono mrefu wa serikali" ulikatika? au sikuhizi umepooza au umepata kiharusi? au ni mrefu tu kwa wanachadema??? Hahahahahaaaaa kazi ipo
CC: zumbemkuu MANI saudari
mgosi TISS ni kitengo cha CCM, haiwezi kufanya lolote, bora hata jumuiya ya waganga wa kienyeji na wapiga ramli wanaweza kufanya uchunguzi.
 
[FONT=courier
new]MAOFISA wa Shirika la Upelelezi la Marekani
(FBI), wamekubali kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi
yaliyotokea Zanzibar Februari 17, mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizopatikana jana maofisa hao wako
nchini na tayari wamekutana na baadhi ya viongozi wa Serikali kwa ajili
ya kuanza kazi hiyo....
[/FONT]
Huu ni uamuzi mzuri wa serikali lazima tutumie marafi kuongeza nguvu kwa suala hili,maana leo wataua viongozi wadini kesho viongozi wa serikali.
 
MAOFISA wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamekubali kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi yaliyotokea Zanzibar Februari 17, mwaka huu.

Kwa mujibu wa habari za kuaminika zilizopatikana jana maofisa hao wako nchini na tayari wamekutana na baadhi ya viongozi wa Serikali kwa ajili ya kuanza kazi hiyo...
Mwisho wa siku watatuambia hao ni magaidi na watapendekeza walete majeshi yao ili kuwasaka ili wachukue gesi yetu na mafuta
akili kumukichwa!!!!!!!!!
 
Haya na mimi nakubaliana na wewe, sasa kwa pamoja tujiulize ni lini vyombo veytu viliwahi kufanya kazi nzuri? Ni kwa kiasi gani tunaviamini? Vyombo vyetu vipo kidili sana kuanzia kupeana madaraka mpaka utendaji. Viongozi wanawapa madaraka kwa kuwadanganyishia nao wanafanya kazi kwa kuwadanganyishia.
mkuu kama niko sawa and i stand to be corrected kuna issue inaitwa state soveregnity. na pili ingekuwa bora hizi statement za kuomba msaada zitoke kwa watawala wenyewe na sio kwa political figures
 
Mwananchi linamilikiwa na nani vile?
FBI wa USa au wa Mabwepande??

Werevu ndio waliao!
 
Haya na mimi nakubaliana na wewe, sasa kwa pamoja tujiulize ni lini vyombo veytu viliwahi kufanya kazi nzuri? Ni kwa kiasi gani tunaviamini? Vyombo vyetu vipo kidili sana kuanzia kupeana madaraka mpaka utendaji. Viongozi wanawapa madaraka kwa kuwadanganyishia nao wanafanya kazi kwa kuwadanganyishia.
Ujue tatizo ni kwamba kwa kiasi fulani kwa sasa watu hawana imani ya kutosha na vyombo vya usalama vya nyumbani kwa hiyo lengo la kuleta vyombo vya kimataifa ni ili kuepuka lawama.
 
Usalama wa Taifa tunaulipa mishahara ya kazi gani? Tunashindwaje kukamata wa halifu wenyewe mpaka tuagize watu kutoka nje? Hawa watu kiusalama tunawaamini vipi? Watanzania tunahitaji kufanya maamuzi ya haraka sana na siyo lazima 2015 hata sasa ikibidi tufanye hivyo, kwa hali hii nchi ulinzi ni zero... Aliyesema JK ni chaguo la mungu na alaaniwe milele... Tunawalipa kiasi gani cha fedha na zinatoka wapi? Wanakaa kwa siku ngapi? Taifa liwekwe wazi!
 
JK anataka kuhakikisha kuwa zanzibar inaendelea kuwa koloni la tanganyika, wazenji wamejitela na sababu imepatikana ya kuwaletea wababe kuikalia ardhi yao kwa niaba ya tanganyika kwa kisingizio cha ugaidi, yakheee... imekula kwenu hiyo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom