Faustini Munishi: Malebo

Faustini Munishi: Malebo

fakalava

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2015
Posts
4,459
Reaction score
6,031

Huyu jamaa kabla ya kuokoka alikuwa ni jambazi wa kuogopwa hapa Tanzania na baadhi ya nchi jirani. Kwa hapa Tanzania alipatikana zaidi Keko (Dar es laam), Moshi (Kilimanjaro), Unga Limited (Arusha).

Alifanya matukio mengi ya ujambazi na kufanikiwa, lakini kuna matukio mengi alinusurika kifo ndiyo maana uso wake mpaka sasa umejaa makovu.

Mwishowe aliacha ujambazi na kuokoka akaamia Nairobi, akaanzisha kanisa na kuwa muimbaji. Kuna marafiki zake wakina Malebo, Mrefu pamaja na wanawake kadhaa ambao kati ya hao, Mrefu, pamoja na wanawake wawili alifanikiwa kuwashawishi wakaokoka lakini Malebo alikuwa kisiki cha Mpingo mpaka akaamua kumtungia wimbo.

Mpaka sasa kitu ambacho sikijui ni je, huyu Malebo alifanikiwa kuokoka na kuwa kondoo wa bwana au lah?
 
Kama Munisi alikuwa Jambazi basi majambazi wa zamani walikuwa mdebwedo.
 
Malebo jeuri saana na ngoma zote alizoimbiwa na jamaa yake aache ujambazi lakini bado alivunja na kuiba nyumbani kwa Munishi pale Nairobi. Ahahahaha!

Binadamu sio wa mchezo mchezo!
Duh hiyo kali...

kamwibia swahiba wake??? Inawezekana urafiki wake ulikuwa si wa kimchezochezo kama ule wa Jakaya na Edward...
 
Duh hiyo kali...

kamwibia swahiba wake??? Inawezekana urafiki wake ulikuwa si wa kimchezochezo kama ule wa Jakaya na Edward...
Ahahaha! Best friend siku zote ndo huwa wanageuka kuwa maadui wakubwa. Sijui kama wamepatana kwa sasa na sijui kama malebo ameokoka tayari kama ilivyokuwa mission ya Munishi!? Sijui!

Na ilisemekana malebo alikuwa anamind maana Munishi alimtumia kutenegeneza pesa na hakupewa hata mia maana kuanzia jina la wimbo hadi album iliitwa Malebo. Na iliuza saana kuanzia Tanzania hadi Kenya.
 
Hahahaha hiyo kali. Naona kuna kiongozi hapa chini kasema Malebo kishaokoka. Nadhani ni muda muafaka sasa wa Jakaya kumfuata Edward kwenye UKUTA

No mkuu kwa sasa Malebo kaokoka na tayari munishi alishatoa ngoma inaitwa Malebo aokoka
 
Malebo jeuri saana na ngoma zote alizoimbiwa na jamaa yake aache ujambazi lakini bado alivunja na kuiba nyumbani kwa Munishi pale Nairobi. Ahahahaha!

Binadamu sio wa mchezo mchezo!
Aaaah! Siyo mchezo.
 
Duh hiyo kali...

kamwibia swahiba wake??? Inawezekana urafiki wake ulikuwa si wa kimchezochezo kama ule wa Jakaya na Edward...
Teh teh teh! Ngoja tuone, labda kwa muujiza.
 
Back
Top Bottom