GE2025 Fatuma Kange akiomba kura kwa wajumbe Same Magharibi

GE2025 Fatuma Kange akiomba kura kwa wajumbe Same Magharibi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea ubunge wa Jimbo la Same Magharibi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fatuma Kange, amewataka wananchi wa jimbo hilo kufanya mabadiliko ya kihistoria kwa kumchagua mwanamke mwenye maono, uthubutu, na dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo kwa watu wote.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara iliyofanyika kata kwa kata ndani ya jimbo hilo, Fatuma amesema ni wakati wa wananchi kuachana na siasa za mazoea na kuwapa nafasi viongozi wapya wenye ujasiri wa kusimamia masuala ya msingi kama elimu, afya, kilimo, na ajira kwa vijana.

"Ninafahamu changamoto zenu. Nimesikiliza kilio cha kina mama, vijana, na wakulima. Niko hapa si kwa maneno bali kwa vitendo. Nataka tuandike historia kwa kumchagua mwanamke wa kwanza kuwa Mbunge wa Same Magharibi — mwanamke anayetoka miongoni mwenu, anayewajua na anayewapenda," amesema Fatuma kwa msisitizo huku akishangiliwa na umati wa wananchi.

Kange ameahidi kushirikiana kwa karibu na wananchi katika kupanga vipaumbele vya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara, kuongeza huduma za afya vijijini, pamoja na kuhakikisha kuwa fedha za vijana na wanawake zinapatikana kwa wakati na kwa usawa.

Ameongeza kuwa maendeleo hayaji kwa bahati mbaya, bali kwa mipango, usimamizi, na uongozi bora — mambo ambayo amesema yamekosekana kwa muda mrefu katika jimbo hilo.


Chanzo: Global Tv​
 
Ninamfahamu Fatuma Kange, niliwahi kufanya naye kazi mahali.

Ana udhubutu.

Wananchi wa Same (sijui ni Same ipi, je ndo kwa Ana Malechela?) mpeni kura zote Fatuma Kange.
 
Back
Top Bottom