Manyerere Jackton
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 2,438
- 4,465
Kwa muda sasa, hili Shirika la Ndege la Fastjet limekuwa likilalamikiwa na wengi, lakini hakuna hatua wala mabadiliko yanayoonekana. Kero kuu niliyonayo kwa Fastjet ni kwenye mizigo.
Najua tofauti yao ya uendeshaji ikilinganishwa na mashirika mengine ya ndege. Lakini hili la kukataa kubeba mizigo ya abiria isiyozidi kilo 20 bila kuilipia nadhani ni uonevu uliopitiliza.
Wiki mbili zilizopita nilishuhudia jamaa mmoja pale KIA akiwa na kisu alichonunua mjini Arusha. Alipofika uwanjani wakati wa ku-check in akafuata taratibu zote-za kueleza kuwa ana kisu.
Jambo la ajabu akatakiwa alipe Sh 36,000 kusafirisha kisu alichonunua kwa Sh 10,000. Alibembeleza, lakini hatimaye alikwama. Akasaidiwa na binti mmoja kwa kukiweka kwenye mizigo yake.
Juzi tena, mzee mmoja akiwa na ki-sanduku kidogo akitoka Mwanza kwenda Dar, alilazimika kuacha sanduku na kubeba mkononi blanketi kwa sababu alilazimishwa kulipia Sh 35,000 hicho ki-sanduku, na yeye akawa hana.
Hoja yangu hapa ni hii; hivi kweli hiki kinachofanywa na Fastjet ni sahihi? Haki za abiria katika nchi hii kwa nini hazilindwi na mamlaka husika, hasa TCAA? Hiki kiburi cha Fastjet kinatokana na nini?
Kuna umuhimu wa kulichunguza shirika hili na kuona kama kweli linastahili kuendelea kuwapo. Pengine huu ndio wakati wa kuwa na Shirika letu la ndege la Taifa.
Nawasilisha