Fastjet waleta ndege mpya

Jamaa inaonekana hawajaja kujaribu soko..nimepanda precision ya Dar-Arusha jana ikiwa na viti vingi wazi..hali itazidi kuwawia mbaya kwa style hii hakika.
 

HII NI NDEGE YA KWENDA WAPI? Naona babu umekolea :bange:
 
Naona Kenya airways nao wanataka kuleta low cost coz wameona mambo yanaweza kuwa mabaya kwao
 

We sio msafiri, Kama unapenda airbus nenda kwa BA au Lufthansa


Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk
 
Kwa kile kinachoonesha Fastjet wamedhamiria kufanya mapinduzi ya Anga. wameleta ndege nyingine aina ya Airbus A319.....

mpya imetoka wapi na imetoka nch gani.uwezo huo wa kununua mpya wanao?
 
mpya imetoka wapi na imetoka nch gani.uwezo huo wa kununua mpya wanao?

Hapana SIO MPYA, imetoka VIETNAM na WAMEKOPESHWA... Umefurahi sasa???


Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk
 
Pole bwana shirika lenu ndo linakufa hivyo.Mnaona wivu fastjet wanashika market
 

ungeanzisha sredi bandugu hapa sio
 
Una kiroba cha ngapi hapo?hahaaaa duh full kumix au unania nyengine ya kubadilisha mjadala kwa makusudi

Huyo ni mgeni, hajajua bado jukwaa la malalamiko. Ndio kwanza ana posts 4. Msamehe bure tu, tuendelee na kujadili dili za fastjet
 
Safi kabisa, hawa jamaa wa Precision na ATC wametuibia sana!
Kusafiri kwa ndege yaani mtu ilibidi ujiandae miaka!

Hongera sana kwa jamaa wa fastjet

Of course hao PW na ATC ndio walitufanya tuone kusafiri kwa ndege kama ni anasa. Bei zao zilikuwa prohibitive, ndio sababu wakasuka mpango wa kuua community Air ya Mwanza ili ndege zao ziendelee kuhodhi soko.
 
Shirima kazu buti, wapinza wanakuja juu, wewe huduma zinashuka
 

£68.60 ni nauli toka london kwenda Gatwick by january 2013 na easyjet. This is a distance of 40 km. Kwa distance hiyo na nauli hiyo, it seems to me kuwa usafiri wa ndege ni ghali Uingereza. najaribu kujiuliza kama sio hawa low cost, za kawaida zinakuwaje. Naomba unielimishe kidogo.
 

Kuku mgeni hakosi kamba!

Sent from my LT26i using Tapatalk 2
 


Nashukuru sana mkuu,ngoja niwahi kufanya booking..this time nimedhamiria nikapate mchemsho wa Sato original toka Ziwani! Nitakua Malaika pale..
 
Fastjet ukweli sasa wanashika soko la anga kwa kasi ya ajabu.
Ningeishauri PW na wao wabuni aina ya ushindani kibiashara ili waendane na hali hii kuliko kubuni mbinu za propaganda na kuhonga ma-engineer wa ndege pinzani ili wafanye itilafu katika ndege kama walivyo fanya ATC.
Na fastjet wasipokaa sawa na hizo mbinu za PW watatoka kwenye soko mapema na PW waendelee kuvuna mapesa!
 

At least wiki mbili kabla ya safari though nadhani na wao wanaangalia zile siku za sikukuu mfano ukiingia kwenye website yao zile tarehe za mwanzo kuanzia tarehe 1 mpaka 6 nauli unakuta 80,000 lakini mtu akikata let say tarehe 31 December kama unatokea Dar - MZA utapata ile ya 32,000 (43,000 pamoja na kodi) but tarehe hiyo hiyo kama mtu anatokea MZA - Dar nauli ni 48,000 (59,000).

Search to website yao fastjet for detail, ipo simple na inakuwezesha kufanya maamuzi maana bei zote zipo pale unachofanya ni kutafuta tarehe ambayo unaona mfuko wako unaweza
 
Safi sana. Tuwakomeshe kabisa kabisa hawa precision. Wametunyonya kiasi cha kutosha, wametudhulumu kiasi cha kutosha, na wametunyanyasa kiasi cha kutosha. Sasa tunataka mapinduzi. Mapinduzi haya yanaletwa na fastjet.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…