PMM naelewa concerns zako, ila kama nilivyojaribu kuainisha tatizo ni la washindani dhaifu. Kama wako makini na huo upotoshaji wa fastjet wangetumia huo mwanya kwa kupata abiria zaidi na kuishikisha adabu fastjet. Tatizo bado fastjet ni reliable kuliko hao washindani wake otherwise huna haja ya kununua tiketi zake. Swala la kuchelewa na cancellation ya ticket yako ni muhimu watu wakaelewa kuwa hiyo tiketi ina masharti magumu na inakuwa ghali ukikiuka masharti hayo iwe kwa bahati mbaya au kupenda! Hivyo jiulize mara mbili kabla ya kukata tiketi yao na kujidhihirisha kuwa utamudu masharti yao. Kuwa budget au kutokuwa budget ni swala la ushindani na wewe mlaji kuamua unafaidika vipi na hao budget ukilinganisha na conventional business model!