Fastjet ni jipu

mgombea uvccm2017

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
505
376
Jumatano ilikuwa mzee asafiri tukawa tumeshamkatia tiketi ila kwa bahati mbaya tukapata msiba ile kuomba kubadilishiwa tiketi kusogeza mbele gharama ikawa kubwa kuliko tiketi mpya

Tukakata tiketi mpya ya kuondoka leo

Leo mzee alipaswa kuondoka sa nne na dak kumi asubuh tukafika pale Airport na akaingia cheking! Pale akarudishwa mara tatu mzigo wako ulikuwa na pafyum na kachuma kadogo eti alipofanikiwa kupita mbele wakamrudisha kuwa kachelewa dak mbili

Kuwaeleza amecheleweshwa na walinzi wakagoma na hapo ni sa 3 na nusu inamaana bado dak 40 nzima ndege iondoke

Mzee akarudi nje baada ya kuelekezwa aende ofisi za kampun anayotaka kusafiri nayo ili wao ndo wampeleke pale apitishwe

Kufika ofisi ya fastjet pale eti wanagoma hawana nafasi ya kutoka hivyo mzee akate tiketi nyingine

Nilijikuta nawatukana matusi mpaka nikaondolewa na walinzi

Mtu yupo palepale uwanja wa ndege na bado muda wa kuondoka ndege anazuiwaje kuingia???

na hizi pesa tulizomkatia mzee mara mbili anashindwa kusafiri nani anazila?

Magufuli tusaidie hili jipu
 
mkuu check in time ikipita umeachwa na ndege...pia ndege sio basi kiasi cha kubadili tu utakavyo
 
Fastjet tena!! Hapa maelezo ya kutosha si yalitolewa vya kutosha jinsi gani mashirika hayo yanayochaji bei ya chini yanavyoendeshwa? Na kwa maelezo yako ni kweli wanachaji rahisi maana ulivyoambiwa ukate tiketi nyingine ulikata. Mambo ya mizigo na kuwahi kufika uwanjani ni mambo muhimu ya kuzingatia!!
 
Fastjet tena!! Hapa maelezo ya kutosha si yalitolewa vya kutosha jinsi gani mashirika hayo yanayochaji bei ya chini yanavyoendeshwa. Na kwa maelezo yako ni kweli wanachaji rahisi maana ulivyoambiwa ukate tiketi nyingine ulikata. Mambo ya mizigo na kuwahi kufika uwanjani ni mambo muhimu ya kuzingatia!!
Mkuu walinambia nbadilishiwe tiketi ila nilashangaa gharama ni kubwa kuliko kununua tiketi mpya! Imebidi nilipie tiketi mpya mzee aondoke
 
Pole sana mkuu. Ila hawa jamaa kiujumla hiyo check in time limit yao ni jipu. Unaweza kunja mtu mashati airport
 
Kwa msaada zaidi peleka malalamiko yako FAIR COMPETITION COMMISSION UBUNGO. This are industry regulators and consumers protectors. Usisubiri magufuli afanye kila kitu wakati kuna waliopewa majukumu hayo.. fanya nilivyokuambia utaona matokeo yake
 
Fastjet ni jipu Lakini inapokuja kwenye suala la usafiri wa ndege wanakuwa wanazingatia sana taratibu kwa hali ya kawaida unaweza kuona kama ni kitu cha kawaida lakini ikifika kwenye suala la ukaguzi kukiwa na tatizo hata kidogo wanakuwekea wasiwasi na hasa ukizingatia katika ukaguzi mlirudishwa
 
Mkuu walinambia nbadilishiwe tiketi ila nilashangaa gharama ni kubwa kuliko kununua tiketi mpya! Imebidi nilipie tiketi mpya mzee aondoke
Vitu vyote ulivyoelezea ni kosa lako/lenu. Inaonekana wewe ni mgeni wa safari za ndege. Ndege sio kama basi. 1. Huruhusiwi kuingia na vimiminika (Naona dingi yako ni mgeni kwani ukikutwa na kimiminika ni kiasi cha kukitupia kwenye dustbin tu). 2.Kuna muda wa check-inn na ukipita huwezi kuingia hata kama ndege haijaondoka. 3. Tiketi ya ndege sio kama ya basi. Kama ulikata hizi za bei ndogo na zina masharti ya kutobadilisha tarehe ya kusafiri basi ukichelewa/ukiahirisha safari hurudishiwi fedha na kubadilisha ni gharama kubwa.
 
Precision air ndo suluhisho kwa situation kama hzo, kubadili tiket ni elf 40 bila shaka, fastjet inahudumiwa na agent wa pemben(swizpot) mbali na precision ambayo wanaihudumia wenyew kwahyo wanaweza wakakusaidia bila shida hata kama umechelewa robo saa japo kama ndege imewah kufika na wenyew wanaweza wakakuacha vilevile ukifika baada hzo dk 40 za kufunga checkin
 
It's a budget airline.

Ndivyo zilivyo kuna Kitu kinaitwa terms and condition yaani vigezo na masharti ndo kilichotumika hapo.

Hukuti vitu Kama hvyo kwenye precision air.

Next time nakushauri vya bure ni ghali , omba uelezwe masharti Yao Kabla ya kutumia huduma za Bei nafuu .
 
We acha uwongo ukichekiwa ukakutwa na tatizo ukirekebisha si ndio mpango sasa iweje wakuzuie usisafiri kwa kisingizio cha usalama hao ndo zao wanafidia kwa usanii wao wakushusha nauli huku msiojitambua mnaumia mimi ni fundi haraka za kuwahi nikakutwa na testa pen air tz nikawakabidhi nikaendelea na safari hakuna longolongo kama ya hao wasanii
 
hivi check in inaanzia wapi? unapovuka scanner au unapokaguliwa ticket?
Counter ndo checkin inapofanyika, kweny scanner ni mamlaka ya kiwanja haihusian na shirika la ndege
 
Haina shida maana unakuwa na boarding pass, hat ukijichelewesha makusudi hawatakuacha kama unayo watakutangaza mpaka upatikane hata kama watu wote washaingia kwenye ndege
#eddy
 
Back
Top Bottom