:yell::yell::yell::yell::yell:
Nilikutana nao pale BAKITA majuzi......kumbe ndio ilikuwa barua yako ile? Wataalam wa BAKITA waliwashangaa sana!
:heh::heh::heh::heh::heh::heh:
Mkuu Masanilo,
Pole sana kumbe tungeweza kuwa kwenye flight moja siku hiyo. Hebu niambie hiyo ndege iliondoka saa ngapi kesho yake? Au na wewe uliamua kuwakimbia? Usitarajie wakujibu hata siku moja, hiyo imetoka.
Tiba
Wana Jamvi,
Siku ya tarehe 26 April 2013, nilikutana na mkasa wa hawa jamaa zetu wa Fastjet na tangia siku hiyo nilinuia, kutokufikiria kutumia usafiri wa hii ndege tena. Kisa chenyewe kilikuwa hivi;
Nilisafiri kwa gari binafsi kutoka Dar kwenda Arusha tarehe 21 April 2013 na nilitarajia kurudi Dar Ijumaa ya tarehe 26 April 2013 kwa kutumia ndege ya Fastjet iliyokuwa iondoke Arusha (KIA) saa 3:30 usiku. Nilikuwa na tiketi mkononi. Taratibu za Fastjet ni kuripoti dakika 40 kabla ya muda wa ndege kuondoka. Nilikodisha taxi kutoka Arusha na nilifika KIA saa 2:40 usiku. Nilipofika, taxi iliyonipeleka pale iliondoka. Kufika mlangoni, walinzi wakanimbia kwamba nimechelewa na kwamba counter tayari imefungwa na hakuna mtu wa kunicheck in. Nilimkuta na Bwana mwingine aliyekuwa amenitangulia kufika na yeye akibembeleza kuruhusiwa kuingia. Wale walinzi walikataa katakata na ukweli ni kwamba pale counter hakukuwa na mtu hata mmoja. Kwa kushirkiana na msafiri mwenzangu niliyemkuta pale, tulianza jitihada za kutaka kuonana na mwakilishi wa Fastjet pale uwanjani. Jitihada zetu za kumwona mwakilishi wa Fastjet hatimae zilifanikiwa lakini to our suprise, yule Bwana alikuwa too arrogant kupita kiasi. Alitwambia hakuna msaada wowote anaoweza kutupatia. Ndege ilikuwa bado iko pale uwanjani. Wakati tukiendelea kumbembeleza, aliitwa kwenye radio call na hivyo akatutaka tutoke ofisini kwake na kwamba angekuja kutusikiliza baadae lakini akasema msaada pekee anaoweza kutupa ni kutukatia ticket nyingine kwa ajili ya ndege ya Jumamosi asubuhi tarehe 27 April 2013.
Baadae tulipata taarifa kwamba ndege haiwezi kuondoka kwa kuwa imepata hitilafu na kwamba abiria ambao tayari walikuwa wamepanda wameshushwa na kurudi waiting room. Yule mwakilishi wa Fastjet hakurudi tena ofisini pale ingawaje tuliendelea kumsubiri. Kwa kuwa nilikuwa na mkutano muhimu wa kuhudhuria Dar Jumamosi tarehe 27 April 2013, nilianza kufanya mpango wa kuangalia uwezekano wa kupata seat kwenye ndege ya Precision Air iliyokuwa iondoke Arusha (KIA) saa 1:55 asubuhi kuelekea Dar. Bahati nzuri nilimpata mwakilishi wa Precision Air pale uwanjani ambaye baada ya mawasiliano alinihakikishia kunipatia seat kwenye hiyo ndege. Tatizo sikuwa na cash ya kulipia hiyo ticket ambayo gharama yake ilikuwa Tshs. 195,000 one way. Baada ya kuhakikishiwa seat, nililazimika kukodisha taxi ya kunirudisha mjini ili kupata hela za kulipia ticket ya Precision kutoka kwenye ATM. Nilifanikiwa kupata hela na baada ya hapo kazi ya kutafuta hotel ikaanza. Nilipata Hotel na nililala karibu saa 6 usiku.
Saa 11:30 alfajiri tayari nilikuwa kwenye ofisi za Precision Air pale Arusha ili kupanda shuttle kwenda KIA. Kufika tu, nikaambiwa tayari shuttle ilikuwa imeondoka hivyo nalazimika kutumia usafiri wangu kwenda KIA (Ukweli ni kwamba shuttle ilikuwa haijaondoka na wala ilikuwa haijafika ila mlinzi anashirikiana na taxi drivers kudanganya abiria ili wakodishe taxi zao). Nilifanya hivyo na kufanikwa kufika Dar kwenye saa 3:45 asubuhi Jumamosi. Wakati turuka pale KIA, ile ndege ya Fastjet tuliiacha pale na sijui iliondoka saa ngapi. Abiria walilala pale uwanjani bila huduma yoyote hata maji ya kunywa hawakupewa.
Nia ya kuleta uzi huu ni kuwaambia wana Jamvi kwamba wakati mwingine rahisi ni ghali. Safari hii ilinigharimu pesa nyingi sana kwa kuwa tu nilitaka ticket rahisi ya Fastjet (Tshs. 107,000) one way lakini matokeo yake niliingia gharama zifuatazo;
1. Ticket ya Fastjet Tshs. 107,000
2. Taxi Arusha KIA x 3 Tshs. 150,000
3. Hotel tarehe 26/4 Tshs. 50,000
4. Ticket ya Precision Tshs. 195,000
Jumla Tshs. 502,000
Nilinuia hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kujaribu kusafiri na Fastjet na ilikuwa mara ya mwisho pia. Sitakaa nithubutu kufanya makosa tena hata kama Fastjet wata improve huduma kwa wateja na kuajiri watu wanaoweza kuwasiliana kwa heshima na wateja.
Tiba
Nilinuia hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kujaribu kusafiri na Fastjet na ilikuwa mara ya mwisho pia. Sitakaa nithubutu kufanya makosa tena hata kama Fastjet wata improve huduma kwa wateja na kuajiri watu wanaoweza kuwasiliana kwa heshima na wateja.
Pole sana kwa matukio na samahani kwa nitakayoyasema.
Nilishaona kwa macho yangu, desk check ya Turkish Air ikiwa imefungwa saa moja kabla. Ila alikuwepo Mbabe mmoja akapiga simu kwa mama mmoja ndani na wakafungua ingawa wafanyakazi wa Turkish Air walishasema kuwa hadi kesho.
Naona nyie mlikosa mtu kama huyo.
Ila nashindwa kuelewa kitu kimoja, ninavyofahamu mie ni kuwa kwa sasa kwa sheria za ulinzi zilivyo uwanja wa ndege, unatakiwa ufike masaa mawili kabla yaani dakika 120 kabla. Sasa wewe nani alikuambia unafika dakika 40 kabla? Dakika 40 kabla ni kuwa ndiyo mnajiandaa kwenda kuingia kwenye ndege tayari na si kwamba ndiyo unafanya Check-In.
Naona ukaja tena kuchelewa hata Bus la kwenda KIA. Yaani hata Bus likakuacha jamani? Nalo sijui utasingizia nini?
Pole sana kwa tukio ila kumbuka kuwa uwanja wa ndege unatakiwa kufika saa MBILI kabla popote pale duniani.
Ndio tatizo letu wabongo..Tuna alegry na kutunza muda afu tuliambiwa utaratibu tunakuwa wakali.Wenzetu ngozi nyeupe ukikuta mlango umefungwa hakuna kubembelezaPole kwa yalio kukuta,lakini shirika gani la ndege unatakiwa ufike 40 min before dep? hiyo kali na wewe mwenyewe vile vile kama msafiri sidhani kama ulijitendea haki,zisinge kutoka hizo zote kama ungekwenda 90 minutes before ya flight yako
ungeweza kupita kila sehemu bila tatizo kuliko unakwenda last minute una rush,ungeweza pia kupata ufumbuzi wa ndege nyengine kama ingekuwepo, anyway sikunyengine jipange fika mapema.
Nilinuia hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kujaribu kusafiri na Fastjet na ilikuwa mara ya mwisho pia. Sitakaa nithubutu kufanya makosa tena hata kama Fastjet wata improve huduma kwa wateja na kuajiri watu wanaoweza kuwasiliana kwa heshima na wateja.
Tiba
Hapa unasukumwa na hasira tu, inawezekana usirudie kutumia Fastjet hivi karibuni lakini siyo hata waki-Improve kama ni hivyo utaacha kupanda ndege hapa Tanzania, binafsi Air Tanzania walishawahi kunisababishia usumbufu na hasara kubwa sana niliapa kutopanda tena ndege zao, lakini pia hata Precision Air walishawahi kunisababishia usumbu wa ajabu sana kwa hiyo nime conclude kwamba Usafiri wa anga kwa hapa Tanzania bado hauja 'seto' vizuri, mimi nitaendelea kuwatumia Fastjet, Precision Air na hata Air Tanzania kwasasa na hata watakapo improve huduma zao, kwasababu so far Air Tanzania na Precision wameshanikwaza kwa nyakati tofauti na hii haitanifanya niseme wao hawafai kuliko Fastjet ambao kwa route zangu zoote sijapata bahati mbaya nao
Mkuu issue sio gharama bali ni ubabaishaji wa huduma za usafiri hapa Tanzania.
Usumbufu wa usafiri wa ndege upo pia Precision Air, tena upo sana tu.
Let be fair.
Mkuu Sikonge huna haja ya kuomba msamaha kwani hakuna lolote baya ulilolisema, tuna elimishana na kupeana maarifa tu. Kwanza naomba nifafanue kwamba sikuachwa na shuttle asubuhi ya tarehe 27 kama unavyodai. In fact nilifika mapema kabla shuttle haijafika pale na dereva taxi na mlinzi wakaniambia uongo kwamba shuttle tayari imeondoka ili nikodishe taxi yao. Shuttle ilifika KIA wakati namalizia kucheck in. Suala la muda wa kuripoti uwanjani unategemea airline na airline lakini in general local flight unatakiwa uwe uwanjani one hour before departure time na international flight ni two hours, lakini hawa wenzetu wa Fastjet wao wanatangaza 40 minutes before departure kitu ambacho nilitimiza.
Hakuna mahali ambapo nilikwenda kinyume na matakwa yao. Lakini kumbuka pamoja na kukataa kunicheck in, hiyo ndege bado haikuondoka usiku huo.
Masanilo ni shahidi alikuwa asafiri na ndege hiyo pia.
Tiba
Pole Tiba
Mimi bahati huna si mwepesi sana wa kufanya conclusion kwa mkasa/ tukio moja. Kwa jinsi ulivyojieleza unaonekana ni mtu mwenye mwenye elimu kubwa ambayo ingekusaidia katika kufanya conclusion ambazo ni 'objective'. Sikubaliani na wewe katika kurusha hizi shutuma as if kwamba kilichotokea hakiwezi kutokea katika shirika la ndege lolote hapa duniani.
Mimi niliachwa na precisionair pale JNIA nikielekea mwanza nikiwa kwenye mstari saa 1.20 kabla ndege haijaondoka. Tulikuwa kama wanne hivi na mtu mmoja ambaye alionekana ni mkubwa tu. Ningekuwa peke yangu ningesema labda wamenionea mimi msukuma wa watu. Tukapewa ndege ya kesho yake saa 2 asubuhi kupitia kilimanjaro. Kilimanjaro tuliondoka saa tisa mchana.
But toka kipindi hicho nasafiri kama kawaida tu
Mkuu hayo ni matukio tu ambayo yangeweza kukupata hata ukiwa na usafiri wowote ule iwe meli, gari binafsi n.k
Ila nikuachie semi mbili, ya kwanza " WAKATI MWINGINE KUKOSA HUWA NI BAHATI" ya pili " EVERYTHING HAPPEN FOR A REASON". Unaweza kubisha lakini ipo siku utayakumbuka haya maneno yangu
Bye, cheeerz
Pole kwa yalio kukuta,lakini shirika gani la ndege unatakiwa ufike 40 min before dep? hiyo kali na wewe mwenyewe vile vile kama msafiri sidhani kama ulijitendea haki,zisinge kutoka hizo zote kama ungekwenda 90 minutes before ya flight yako
ungeweza kupita kila sehemu bila tatizo kuliko unakwenda last minute una rush,ungeweza pia kupata ufumbuzi wa ndege nyengine kama ingekuwepo, anyway sikunyengine jipange fika mapema.
Nimekupata vizuri sana mkuu hapo kwenye nyekundu. Kwa kweli hata mimi ndiyo kilichonipata, ilibidi niingie mfukoni na nikaspend zaidi ya nauli. Inasikitisha mno. Bahati mbaya sijawahi kusafiri na ndege za wenzetu kwenda nje ya nchi, ningeweza kulinganisha. Tena ingekuwa enzi zangu zile nizungumzia miaka ya 20+ walai ningenasa mtu kibao. Lakini ndo hivyo binadamu tumeumbwa kusahauMkuu Polisi, yumkini wewe ni kati ya wachache wenye busara. Nashukuru kwa kunishirikisha kisa chako na mimi ni mtu ninayesafiri mara kwa mara kwa hiyo matukio ya ndege kuchelewa au kuhairishwa ni ya kawaida sana. Tatizo langu kubwa hapa pamoja na kwamba niliingia gharama za ziada ni majibu ya huyo mwakilishi wa Fastjet pale uwanjani usiku ule. Kama angeweza kunishawishi kwa lugha ya staha ni kwa nini hawawezi kuniruhusu kucheck in kwa wakati ule inawezekana leo nisingeweka bandiko ili hapa. Yaani anatoa majibu as if nimeenda kwake kumuomba hela ya kula au nauli ya kunifikisha mjini? Wanapashwa wajue kwamba we are their customers and we need to be treated with dignity.
Tiba
Mkuu Polisi, yumkini wewe ni kati ya wachache wenye busara. Nashukuru kwa kunishirikisha kisa chako na mimi ni mtu ninayesafiri mara kwa mara kwa hiyo matukio ya ndege kuchelewa au kuhairishwa ni ya kawaida sana. Tatizo langu kubwa hapa pamoja na kwamba niliingia gharama za ziada ni majibu ya huyo mwakilishi wa Fastjet pale uwanjani usiku ule. Kama angeweza kunishawishi kwa lugha ya staha ni kwa nini hawawezi kuniruhusu kucheck in kwa wakati ule inawezekana leo nisingeweka bandiko ili hapa. Yaani anatoa majibu as if nimeenda kwake kumuomba hela ya kula au nauli ya kunifikisha mjini? Wanapashwa wajue kwamba we are their customers and we need to be treated with dignity.
Tiba
Pole sana Tiba, ila ni vyema, hata kama hutatumia usafiri wa FastJet tena, uende kwa top boss wao hapa nchini ueleze mkasa wote huo. Unajua sisi Waafrika mtu akiwa kwenye ofisi ya kutoa huduma anajiona sijui kama kitu au mtu gani! Ule wajibu wake anakuwa haujui; even if huwezi kumsaidia mtu kupata solution ya tatizo lake, hata namna unavyowasiliana na mteja wako inaweza kuwa msaada kwake! Aisee nenda Ofisi za FastJet utoe malalamiko haya labda itakua fundisho kwa wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo, INAUMA SANA! POLERedDevil, ungejua nilivyokuwa nimekasirika usiku huo baada ya majibu ya huyo mwakilishi wao, kwa kweli hilo sikulifikiria kabisa kuongea na mtu yeyote kutoka Fastjet na hata leo hii hamu sina kabisa.
Tiba
Aisee ulikosea muda wa kureport kwa hili nawatetea 40minutes?!nawachukia precision lakini sitaacha kupanda ndege zao to settle for the less imewahi kunisubiri twice KIA yani napigiwa simu na naingia ndani nakuta captein anatangaza jina langu.na nikiwa na masunduku yangu sina presha ya kulipia mzigo wala kukataliwa ndoo ya samaki.wananiuzi tu wanavyotaka kuhodhi hii huduma