Fast Food Sinza kwa Remmy ni wezi

Fast Food Sinza kwa Remmy ni wezi

ZionTZ

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2009
Posts
1,282
Reaction score
541
Chukueni taadhari wakuu mnapoenda kula pale fastfood Sinza kwa Remmy. Yaani wale wahudumu ni wezi wote kasoro mzee mmoja wa makamo hivi nahisi atakua Mhaya kutokana na lafudhi yake.

Wanaibaje?
Wewe ukienda wanakupokea pale counter alafu unatoa oda yako afu unaenda kukaa baadae wanakuletea. Ukimaliza anakuja anajifanya anaandika andika kwenye kikaratasi flani kwa mwandiko wa mcharango hivi afu anakutajia bill kubwa kuliko uhalisia.

Mimi nligundua baada ya kuwa nakula chakula kimoja kwa siku tatu mfululizo na wahudumu tofaut kila siku napata bill tofaut. Alafu ukitaka kujua bei halisi wewe ulizia palepale counter wale hawana cha kukuibia kwa sababu kazi yao ni kupakua chakula tu.

Kuna kadada pale kanaitwa Aisha na jamaa mwingine mweusi hivi kama Mkurya hao ndo wezi hatari. Hili swala lina baraka kabisa kwa uongozi wao kwa sababu kila mara nauliza Menu hawanipi wala ubao wa bei hamna.

Mi naomba kwa yeyote mwenye connection na uongozi wao awafikishie hii habari, wengi wanalalama sana. Tena wakikuona umekuja na wife ndo balaa!

Sio tabia nzuri kabisa.
 
Lunch wengi hatuli majumbani mkuu...ajira zinabana.
 
Tatizo mnaenda kibosi bosi,,,,sehemu kama hizo ikibidi unaulizia bei kaunta au unaomba menu
 
Njia pekee ya kuleta mabadiliko ni kuacha kutumia huduma zao.
 
haya yote ni kwasababu ya ccm,na october ndo mwisho wake,peeeooopleeee...
 
Jamani utaagizaje chakula kwa mdomo? Heshima ya hela yako iko wapi? Unatakiwa ufike, ukae mezani, umwambie mhudumu akuletee menu kisha unachagua chakula na bei ndo unaagiza. Hela yako ni ya gharama atii aloo
 
Niliwahi kuchukua chakula hapo kwa ajili ya mgeni wangu wala sikukumbuka kuangalia menu yao. Cha msingi ni kumtafuta meneja wao.
 
Ungegoma kulipa mpaka umuone manager na kama una risiti za chakula aina moja bei tofauti ungewaumbua, tatizo letu wengi hamna confidence
 
Yote inasababishwa na tabia hizi miongini mwa vijana wengi wa kitanzania:-
1.Wengi wanadhani kuuliza bei ni ushamba.
2.Tabia ya kutopenda kuchukua risiti na hata tukichua huwa hatuna kawaida ya kusoma kwa makini kilichoandikwa kwenye risiti.
3.Tabia ya kupenda kung'ang'ania mahala pamoja pa kula na kupata mahitaji bila sababu ya msingi, mfano unakuta sehemu watu wamejazana na foleni kisa ni chipsi tu na mishkaki, ukimuuliza mtu anakwambia "chipsi zao ni tamu" wakati si kweli bali ni mkumbo tu wa kadamnasi!
4.Sinza sio kwa wajanja kama wengi wanavyodhani bali kwa wakuja wengi sanaa hivyo wafanyabiashara wanatumia hali hiyo kama fursa!

Asanteni.
 
Mi nlishajifunzaga sehem kama izo nazama mwenyewe naagiza nalipa palepale narudi kulaa na sahani yangu niko radhi nisimame mpaka kiwe tayari
 
haya yote ni kwasababu ya ccm,na october ndo mwisho wake,peeeooopleeee...

Sasa uadilifu wa mtu unaingiliana vp na ccm,kabla ya kuchangia jambo tafakari kwanza maana unakuwa unaonyesha ni jinsi gani ni mchovu wa kufikiria.
 
Kuna kadada pale kanaitwa Aisha na jamaa mwingine mweusi hivi kama Mkurya hao ndo wezi hatari. Hili swala lina baraka kabisa kwa uongozi wao kwa sababu kila mara nauliza Menu hawanipi wala ubao wa bei hamna.
Sio tabia nzuri kabisa.
The name speaks louder than .......
 
Yote inasababishwa na tabia hizi miongini mwa vijana wengi wa kitanzania:-
1.Wengi wanadhani kuuliza bei ni ushamba.
2.Tabia ya kutopenda kuchukua risiti na hata tukichua huwa hatuna kawaida ya kusoma kwa makini kilichoandikwa kwenye risiti.
3.Tabia ya kupenda kung'ang'ania mahala pamoja pa kula na kupata mahitaji bila sababu ya msingi, mfano unakuta sehemu watu wamejazana na foleni kisa ni chipsi tu na mishkaki, ukimuuliza mtu anakwambia "chipsi zao ni tamu" wakati si kweli bali ni mkumbo tu wa kadamnasi!
4.Sinza sio kwa wajanja kama wengi wanavyodhani bali kwa wakuja wengi sanaa hivyo wafanyabiashara wanatumia hali hiyo kama fursa!

Asanteni.

number 3 ni kweli ila kuna siri nzito dunia hii ni zaidi ya uijuavyo
njoo fyatanga kuna nyama tamu gari zinajaa kuanzia asubuhi mpaka usiku!
 
number 3 ni kweli ila kuna siri nzito dunia hii ni zaidi ya uijuavyo
njoo fyatanga kuna nyama tamu gari zinajaa kuanzia asubuhi mpaka usiku!

Hata pale Rombo Green View Hotel ya Shekilango wahudumu wana tabia ya wizi wa namna hiyo. Hakikisha umeiona menu ndio uagize chakula, ni wezi sana
 
Back
Top Bottom