Faru kulindwa kwa mitambo maalumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faru kulindwa kwa mitambo maalumu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 24, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Faru kulindwa kwa mitambo maalumu


  Na Reuben Kagaruki

  WIZARA ya Maliasili na Utalii itawawekea mitambo ya kisasa zaidi faru wanne waliobaki baada ya mwenzao kuuawa na majangili ili kuratibu mwenendo wa wanyama hao kila siku.Mbali na hatua hiyo, pia wizara hiyo
  imesema itawapatia mbinu mpya askari wanaowalinda, zitakazowasaidia kukabiliana na uhalifu. Mikakati hiyo ilitangazwa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ladislaus Komba alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

  Alitaja mipango mingine ya wizara yake kuwa ni kuhakikisha faru hao wanalindwa kwa kujenga vituo vipya vya askari katika hifadhi hiyo, ili kupunguza ukubwa wa maeneo yanayokaguliwa na vikundi vya doria.

  Faru huyo dume aliyepewa jina la George (12) ni kati ya watano walioletwa nchini kutoka Afrika Kusini Mei 21, mwaka huu na kuwaweka katika hifadhi ya Serengeti.

  Faru hao walinununuliwa na familia ya Paul Tudor Jones, mwekezaji katika eneo linaloitwa Sasakwa lililopo wilaya ya Serengeti na mapori ya akiba ya Grumeti na Ikorongo na hafla ya kuwapokea iliongozwa na Rais Jakaya Kikwete, ambaye alisema watapewa ulinzi mkali unaozidi wa rais.

  Dkt. Komba aliwaambia waandishi wa habari kuwa tangu kuuawa kwa faru huyo msako wa kuwatafuta majangili uliohusika ulianzishwa na uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kushirikiana na polisi kutoka Mugumu na kampuni ya Grumeti Reserves.

  Alisema hadi kufikia Desemba 21 ,mwaka huu wafuatiliaji walifanikiwa kukamata watuhumiwa nane ambao hadi sasa wanaendelea kusaidia polisi.

  "Katika kutafuta ushahidi wa silaha iliyotumika kuua faru huyo, chombo maalumu kilichotolewa na Franfurt Zoological Society kilitumika na kufanikiwa kupata kipande cha risasi ambacho kitasaidia katika uchunguzi," alisema Dkt. Komba.

  Alisisitiza kuwa ulinzi wa faru hao na wanyama wengine umeimarishwa kwa kuongeza askari, magari na vitendea kazi muhimu kwenye maeneo yote yenye faru.Alisema wananchi wamehamasishwa ili washiriki kuwafichua wahalifu wanaotafutwa ambao walishiriki kuua faru hao.

  "Wadau mbalimbali wameshirikishwa kuendeleza juhudi za kubaini mtandao wa wahalifu waliohusika na tukio hili," alisema. Faru hao baada ya kuuawa majangili walitoweka na pembe.

  Alitoa mwito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na serikali kutoa ulinzi wa wanyamapori.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  JK aliahidi kama kawaida yake ya kuwa faru hao watapewa ulinzi mkali sasa imekuwaje hapo..............................

  Hili linatuthibitishia sote ahadi za JK na ahadi tu........................................hana mkakati wa kiutekelezaji..................................a mere lip service.....................
   
 3. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mitambo maalum? kuna dili hapo la procurement linachongwa! si mnajua tena 2015 si mbali? another ufisadi, just wait
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kama wanapewa ulinzi mkali zaidi ya Rais na bado wameuliwa sasa na Usalama wa rais wetu utakuwaje?TANAPA angalieni sana hilo majangili wamezidi kwa sasa!
   
 5. F

  Fenento JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hakuna cha mitambo maalum hapo,kwani hawa viongozi wetu hawapo makini wanachojaribu kufanya ni kuficha aibu ya kuuawa kwa huyo Faru.
   
 6. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hata hao wanne waliobaki jamaa watatambaa nao. Mitambo maalamu haitasaidia sana kwa vile huko walikotoka kuna mitambo bora zaidi na bado faru wanauwawa. Ujangili umerudi kwa kasi sana. Badala yake waanzishe ulinzi shirikishi na wenyeji wanaozunguka hifadhi.
   
Loading...