Farao asiyemjua Yusufu

Dunamist

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
474
682
Mpaka ninapoandika uzi huu, kama sio lockdown ya corona, huko Misri kuna watoto wangekuwa darasani kwenye somo la historia wanajifunza habari za Mwebrania aliyeitwa Yusufu.

Huyu ndo yule jamaa aliokoa Taifa lao na lake yasiangamizwe na njaa baada yakumpa ufunuo wa ndoto ya njaa kali aliyoota mfalme wao.

Baada ya muda kidogo tu kwenye karne ya 13 B.C eti akatokea Mfalme (Farao) ambaye hakumjua Yusufu!! Hii ni zaidi ya joke, mtu anayesomwa kwenye historia za nchi yake mpaka leo eti zamani hizo mtu elite kama mfalme wa nchi eti akawa hamjui? Ndipo huyo Farao akaanza kuwatesa ndugu zake Yusufu.

Nchi yetu inaye Yusufu;

-Yusufu ambaye ametusaidia vijana tulio wengi kuijua na kuanza kuifatilia siasa, tofauti na zamani ambapo siasa ilikuwa mambo ya kizee (yaani ameipa siasa msisimko flani hivi ambao haikuwa nao kabla yake)

-Yusufu ametuonesha kuwa inawezekana kudai haki zetu na kuzipata.

-Yusufu wetu ameisaidia serikali yetu kuwa makini na responsible. Business as usual is no more an order of the day.

-Yusufu wetu ameliamsha sana bunge letu, zamani hatukuwa na time na bunge. Bunge lilikuwa linaboa sana, unadhani kipindi kile Nape kazima bunge live. Tulihamaki kwa sababu hatungepata nafasi ya kuona minyukano mikali kati ya Lissu na mwanasheria mkuu wa serikali, mchuano kati ya Spika na Godbless Lema. Na minyukano mingine mingi kati ya ma-Yusufu na ma-Farao.

- Kwa sababu ya Yusufu, hata wanasiasa wa chama tawala(hasa vijana) wamelazimika kuwa smart, na hii imewaongezea mvuto wa kisiasa.

Kuna kila dalili ya kwamba Farao wa sasa hatambui kazi yoyote aliyofany aYusufu kwa hii nchi, sisi Waebrania tunatambua. Mungu atakulipa Yusufu. Jina lako limeandikwa kwa wino wa dhahabu, utasomwa na vizazi...
 
2020-5=
 
Back
Top Bottom