linguistics
JF-Expert Member
- Jun 22, 2014
- 4,734
- 4,395
Wacha waisome nambaee...naniliu mbele kwa mbelee...haakuna kuandamanaeee... Naniliu mbele kwambelee..tumeipenda wenyewe ...ngenge..chaguo letu milele ngenge....Ule wimbo unaimbwaje kweli!!!
Wacha waisome nambaee...naniliu mbele kwa mbelee...haakuna kuandamanaeee... Naniliu mbele kwambelee..tumeipenda wenyewe ...ngenge..chaguo letu milele ngenge....Ule wimbo unaimbwaje kweli!!!
Kwa NSSF hawajawahi kuzuia kuchukua but ilipofika mwezi wa August 2016,walibadili utaratibu na kuwa kama ilivyokuwa zamani. maana yake ni kwamba ukiishaacha kazi utasubiri kwa muda wa miezi 6 ndipo unafungua madai yako ya kupewa mafao. Kabla utaratibu huu mpya wa kusubiri miezi sita haujaanza,walikuwa wanafanya uchunguzi kwanza kuhakikisha kwamba ni kweli umeacha kazi na hufanyi kazi sehemu nyingine na ikithibitishwa kwamba umepata ajira sehemu nyingine ,utaendelea kuchangia bila kuchukua mafao. Nafikiri katika kipindi cha miezi sita ya kusubiria iwapo utapata ajira sehemu nyingine,kuna uwezekano wakazuia kuchukua mafao yako.Kazi kwakoJaman wanajamvi naomba kufahamu kuhusu taarifa hizi maana Mimi nimesikia tetesi tu, eti FAO hili utalichukua baada ya miez 6 baada ya kuacha Kazi tofauti na ilivokua? Msaada pls
Sielewe sera za CCM zitatunyonya mpaka lini ,Kipindi cha uchaguzi wankuja na ahadi lukuki ambazo hazitekelezeki na ndio mana wanarusha mate mengi kwnye mifuko hizi .SSRA yaja na mbadala wa fao la kujitoa
![]()
Mkurugenzi wa Utafiti na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi
WAKATI fao la kujitoa likiendelea kujadiliwa kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imependekeza kuanzishwa kwa fao mbadala la upotevu wa ajira.
Fao hilo litatolewa kwa wafanyakazi waliopoteza ajira kwa njia ya kufukuzwa kazi au kupunguzwa kazini lakini si kwa wale walioamua kuacha kazi wenyewe.
Pia mamlaka hiyo, imebainisha kuwa hadi sasa takribani wafanyakazi milioni 23 kati ya wafanyakazi milioni 25 waliopo kwenye sekta rasmi ya ajira ambayo ni sawa na asilimia 91.2 hawajajiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii.
Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Utafiti na Sera wa mamlaka hiyo Ansgar Mushi, wakati akiwasilisha mada kuhusu dhana ya hifadhi ya jamii na changamoto ya wanachama kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, katika semina ya siku moja ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na mamlaka hiyo.
Alitaja sifa za fao hilo la ukosefu wa ajira kuwa ni pale mwanachama atakapothibitika kufukuzwa kazi au kupunguzwa kazi, mfuko utampatia asilimia 33 ya mshahara wa mfanyakazi huyo kwa kipindi cha muda wa miezi sita.
“Ila masharti ya fao hili, litatolewa pekee kwa mfanyakazi aliyechangia kwa kipindi cha miezi 18 kwa wale waliochangia kwa chini ya miezi 18 watapewa asilimia 100 ya kile walichochangia,” alisema Mushi.
Alisema sifa nyingine ya fao hilo, halitoathiri mafao ya pensheni ya mfanyakazi ikiwemo mafao mengine yanayotolewa na mifuko ya jamii kama vile, fao la elimu, uzazi, matibabu na ulemavu.
Alisema fao hilo la upotevu wa ajira halitatolewa kwa mfanyakazi aliyeacha kazi mwenyewe kwa kuwa kwake itakuwa si janga linalohitaji msaada kama ilivyo dhana nzima ya uanzishwaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
“Tafiti zetu zinaonesha takribani asilimia 78 ya wafanyakazi wanaoomba fao la kujitoa wengi ni wataalamu wakubwa kwa maana ya kuwa na uwezo wa kuendelea na kazi sehemu nyingine. Wengi wao wanaacha kazi huku wakiwa na mikataba ya ajira sehemu nyingine, wanaomba fedha hizi tu kwa ajili ya shughuli nyingine,” alisema.
Mushi alisema lengo la kuanzishwa kwa mifuko ya jamii kwa mujibu wa sheria na Katiba ni kumlipa mafao mfanyakazi wakati wa uzeeni ili kumrahisishia maisha yake katika kipindi hicho ambacho hawawezi kujiingizia kipato.
Hata hivyo, alisema athari za fao la kujitoa ni nyingi ikiwemo mfanyakazi kukosa fursa ya kupata mafao ya muda mfupi kama vile, uzazi, elimu, ulemavu na ugonjwa, kupoteza sifa ya kupata mafao ya pensheni na kukosekana kwa ukwasi katika mifuko ya hifadhi ya jamii na hivyo kushindwa kulipa mafao kwa wafanyakazi wengine wanaostahili.
“Katika fao la kujitoa, mfanyakazi akishalipwa mafao yake ndio anakuwa ameondolewa kwenye mfuko huo wa hifadhi ya jamii hata akizeeka au kupata janga lolote mfuko haumtambui. Ofisi yangu imekuwa ikipokea wafanyakazi wengi tu takribani 34,000 waliopewa fao hilo la kujitoa sasa wanaomba warejeshwe,” alisisitiza.
Naye, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa mamlaka hiyo Honorius Njole alisema bado fao hilo katika hatua ya mjadala na halijapitishwa wakati pia mjadala kuhusu fao la kujitoa ukiendelea kwa kupokea maoni.
Alisema katika kusimamia mifuko ya hifadhi ya jamii, SSRA imeanzisha miongozo 14 tangu kuanza kwake kazi mwaka 2008, ikiwemo miongozo ya ukomo wa gharama za matumizi ya mifuko hiyo, mwongozo wa usajili wa wanachama na utunzaji wa kumbukumbu au taarifa za mwanachama.
Miongozo mingine ni wa kuhamia mfuko wowote wa hifadhi ya jamii, mwongozo wa uwekezaji, usalama wa fedha za wanachama, ukwasi wa mifuko ya hifadhi za jamii na mwongozo kwa bodi za wadhamini wa mifuko.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sara Kibonde, alisema bado jamii inahitaji kuelimishwa kuhusu umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuwa ina manufaa kwa jamii yote wakiwemo wale wasiokuwepo kwenye sekta rasmi ya ajira.
Alisema kwa mujibu wa takwimu za mamlaka hiyo, jumla ya wafanyakazi waliopo kwenye sekta rasmi ni mmilioni 2.1 kati ya wafanyakazi milioni 25 waliopo.
“Kwa maana hiyo wafanyakazi takribani milioni 23 ambao ni sawa na asilimia 91.2 hawajiunga na mifuko hii.”
Aidha alisema wakati mifuko ya pensheni ina wanachama milioni 2.1, kati yao, mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii wapo wanachama milioni 1.1 wakati mfuko wa bima ya afya wapo wanachama 920,701.
Alisema mpaka sasa mifuko hiyo ina wastaafu 105,057, michango ya wanachama hao inayofikia Sh trilioni 1.69 na bima ya afya Sh bilioni 88.5, ambayo jumla yake ni Sh trilioni 1.78.
Chanzo: Habari Leo