Fanya test nikupe marks.

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,231
Swali la kwanza(marks 40)
Jinsi ya kumwingiza simba ndani ya friji.
Fungua friji halafu msukume ndani na ufunge mlango wa friji.

Jinsi ya kumwingiza twiga ndani ya friji.
Fungua friji na umtoe simba nje halafu msukume ndani twiga na ufunge mlango wa friji.

Sasa ni mda wa wanyama wote/viumbe hai nchi kavu na majini kwenda kushiriki mashindano ya mbio huko msituni,
mnyama ambaye hatashiriki ni twiga aliyefungiwa ndani ya friji.

Swali inakuja.....kuna ziwa ambalo kuna mamba hatari na ngumu sana kuvuka hilo ziwa bila silaha,na unatakiwa uvuke bila silaha utafanyaje???

Swali la pili (marks 40)
Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ina wachezaji 11,ilienda kucheza nchini Uganda.
walipofika Uganda waliingia uwanjani,walipoingia uwanjani kulikuwa na mchezaji mmoja wa Tanzania ambaye anacheza
namba 5,wakati anaingia uwanjani amevaa jezi kama wenzake,kavaa viatu,akavaa soksi.ile anaingia uwanjani
refa akapiga filimbi ya kumrudisha nje ya uwanja.
Je huyo mchezaji ana kosa gani??????

Swali la tatu(marks 5)
Kuku alipanda mlimani,halafu akaruka juu na kutema chini.
je hayo mate yatadondokea chini au yataelekea juu?

Swali la nne(marks 5)
Ng'ombe ni watanzania ila huwa anaenda kula majani kenya,siku moja akazaa.
huyo ndama atakuwa wa tanzania au wa kenya?

Swali la tano(marks 10)
Unatakiwa uvuke mpaka wa tanzania na kenya,kwa sheria iliyowekwa anayetoka tanzania haruhusiwi kwenda kenya.
na wakenya harusiwi kwenda tanzania,na pale mpakani kuna mlinzi,unajua mda anaolala huyo mlizi ni sekunde 20,
unatakiwa uvuke kwa huo mda mlinzi analala,tatizo ile unafika mda umeshaisha na mlinzi anaamka.
sasa utafanyaje ili uvuke??
 
Swali la kwanza, ntavuka ziwani kwa raha zangu bila hofu kwa kuwa mamba wako bize kwenye mshindano ya mbio huko msituni.

Nipe maksi zangu 40 tafazali.
 
Swali la kwanza, ntavuka ziwani kwa raha zangu bila hofu kwa kuwa mamba wako bize kwenye mshindano ya mbio huko msituni.

Nipe maksi zangu 40 tafazali.
umetisha umechuka zako 40%
 
Swali la 5,ntakimbia nkifika katkat kabla ya sec 20 kwisha nageuka nlikotoka..mlinzi akiniona atajua naenda tz so atanirudisha kenya na ntakuwa nmevuka mpaka kiulainiiiiiiiiiiiiiiiii....npe 5
 
swali la tano pale mlinzi anapoamkia gafla nageuka na kujidai kua narudi tz nlipotoka.bila shaka ataniambia huruhusiwi kuingia tz kwaivyo rudi kenya kumbe mie tayari nlikua natoka tz and vice versa iwapo nimetokea kenya.lete marks wewe mtu.ha ha ha.
 
haya bhana,umepata 10%
 
Swali la 5,ntakimbia nkifika katkat kabla ya sec 20 kwisha nageuka nlikotoka..mlinzi akiniona atajua naenda tz so atanirudisha kenya na ntakuwa nmevuka mpaka kiulainiiiiiiiiiiiiiiiii....npe 5
Hapa pia 10%
 
Namba 5: kwa sababu anatoka usingizini unadesh kama ulikuwa unatoka kenya kuja tz then yeye atakurudisha kenya unakua ushavuka bila hata jasho.

Namba 3: kuku hatemi mate

Namba 4: Ndama aliyezaliwa ni wa ng'ombe na sio watz au wakenya.

Namba 2: Alikuwa amevaa soksi juu ya viatu badala ya viatu juu ya soksi.
 
umepata 95%
 
Back
Top Bottom