Fanya makosa yote ila usije fanya hili

zegamba180

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
818
536
Binadamu kukosea katika maisha ni jambo la kawaida sana. Binafsi naamini asiyekosea ni yule asiyefanya lolote. Japo hilo haliwezekani kwani usipofanya kwa vitendo basi utakosea kwa maneno tu.

Twende kwenye hoja;

"Kosa la kukosea kuoa ama kuolewa ni kosa baya sana maishani." Mtu mmekutana hata mwezi kuisha unahitaji kuoana nae.

Umepata muda wa kutosha kumfahamu? Ndoa haina majaribio kaka yangu/dada angu. Nimeshuhudia rafiki, ndugu, jirani wakijuta na kulia kwa kukurupuka kuoa/kuolewa. Unapata uthubutu gani kumuoa ama kuolewa nae huyo?

Tuliza akili mnoo kuchuja aina ya mwenza anayemhitaji kufanya nae maisha.
kosea yote ila usikosee kuolewa ama kuoa.
 
mkuu ndhani unaongea kitu kizuri lkn unaongea kinadharia na si kiuhalisia na yamkini haujaingia hata ktk ndoa ama bado mchanga sana.dakika moja ktk ndoa na maisha inatosha kabisa kumbadirisha mtu ulomchunguza na alokuwa mwema na bora kwa miaka kumi.hakuna kanuni bro.mungu tu ndo anaejua kuchunguza na kukuchagulia hivo usijidanganye kuwa unaakili ya kuchunguuuuuuza.afu km ww ni ME basi jua KE ni viumbe hatari sana sana nabwasumbufu sana na baya zaidi hawajijui km wana mapungufu sana.
na km ww ni KE basi jua ME wanaamini kuwa wao wapo juu ya KE.haya endelea na uchunguzi wako
 
Bora nihamie upande wa pili! Ndoa ukiona inaenda ndivyo sivyo unadai talaka faster unadandia kwamwengine......
Ila ni heri kuoa au kuolewa ukiwa na miaka 40 hukoo lakini unauhakika na mwenzako na mtaishi maisha matamu kuliko kukurupuka na miaka yako 20 ndoa ndoa kwenda kuivamia shubiri
 
Wanawake ukijua kuwatumia vizuri wanaraha zote, yaani utapewa Nyama ya steki, utapewa utumbo, utapewa kisamvu, utachumiwa mchicha yaani we acha tu

Wewe ndo unajua maana ya maisha. Big up.

Kwenye ndoa kila mmoja anatakiwa kukubali kuacha yake na kuendana na mwenza. Ukianza kulazimisha yako unajitengenezea mazingira magumu wewe mwenyewe.

Wape vijana wenzako tuition wafaidi kama wewe.
 
1. Huwezi kumchunguza mtu mkiwa wapenzi coz hata matatizo utakayomuona nayo hayatakukera kwa wakati huo, na unaweza kujipa matumaini atabadilika.

2. Kuna watu wanajua kuigiza kuliko hata kina Angelina Jolie na Harrison Ford, hawachunguziki hata kwa mtutu.

3. Ni kumuomba mungu tu akupe jicho la ndani kuweza kumjua mtu mapema.

4. Mnaweza ku date kwa miaka kumi na msidumu kwenye ndoa, na mnaweza ku date kwa miezi mitatu na mkadumu kwenye ndoa, hamna formular kama za magazijuto kwenye mapenzi.
 
chukulia ww umeacha yako na kuendana na mwenzako kwa pamoja lkn yy bado anafanya yake binafsi tena kwa kukutamkia kashfa unafanyaje na hasa ukiwa ME.
 
1. Huwezi kumchunguza mtu mkiwa wapenzi coz hata matatizo utakayomuona nayo hayatakukera kwa wakati huo, na unaweza kujipa matumaini atabadilika.

2. Kuna watu wanajua kuigiza kuliko hata kina Angelina Jolie na Harrison Ford, hawachunguziki hata kwa mtutu.

3. Ni kumuomba mungu tu akupe jicho la ndani kuweza kumjua mtu mapema.

4. Mnaweza ku date kwa miaka kumi na msidumu kwenye ndoa, na mnaweza ku date kwa miezi mitatu na mkadumu kwenye ndoa, hamna formular kama za magazijuto kwenye mapenzi.
nimelipitia hili unalolisema kwa vitendo.na sasa nipo motoni.sijyi la kufanya maana kila kitu kibaya nadhani nasubiri muda tu wa kujilipua.serious
 
Back
Top Bottom