SoC01 Fanya haya kama kila unachotaka kukianzisha hakimaliziki/hakifanikiwi

Stories of Change - 2021 Competition

kipenseli2021

JF-Expert Member
Jul 17, 2021
831
783
Changamoto za maisha /mafaniko katika maisha zinatufanya kuanzisha vitu vingi lakini tunashindwa kuona mwisho wake au matunda yake/mafaniko kwa mawazo yetu

Vitu vingi au mawazo mengi yanakufa kabla hatujaona mafaniko yake au mwisho wake mwema kwa mfano unaweza waza kuanzisha biashara lakini inakufa kabla haijaanza,tunasikiliza shuhuda mbalimbali za watu waliofanikiwa katika sekta Fulani na tunapata nguvu ya kuanzisha kitu lakini kina kufa kabla ya kuona mafanikio au matunda yake.

Katika vitu tunavyo viwanja kuna hatua mbalimbali tunapitia lakini hatua ya mwisho ni kuona mafanikio au rejesho lenye thamani au faida

Kama mtu ulikuwa unataka kufanya muziki basi mwisho tunategemea kuona unafaidika kupitia mziki,kama mtu unataka kufanya biasha basi mwisho tunategemea kuona unapata faida kupitia baishara uliyoanzisha,kama mtu unataka kutunga vitabu basi mwisho tunategemea kusoma vitabu vyako na ufanikiwi kupitia vitabu vyako

Hakuna kitu tunacho kianzisha tukitegemea mwisho mmbaya lakini kabla hatujafikia hata mwisho mawazo yetu yanakufa mapema sana.

Imekuwa kama ugonjwa wa kutaka kufanya na kuacha tunamawazo mengi sana mazuri lakini yanakufa mapema sana

Kumbuka “Mtu anaweza kufa lakini wazo aliweza kufa” usipo tumia wazo lako leo na kuona mwisho wake basi kesho litatumiwa na mwingine.

JE TUFANYAJE AU NIFANYAJE

FANYA YAFUATAYO HILI UWEZE KUWEKEZA KATIKA WAZO LAKO NA UPATE FAIDA

Fanya yafuatayo hili uweze kuwekeza katika wazo au miradi unayo taka kaunzisha


ELEWA LENGO LA MRADI/WAZO KWA UJUMLA
  • Kitu cha kwanza unatakiwa ujue lengo kuu la mradi au kitu unacho taka kufanya kwa upana na kujua mipaka yake,lengo kuu linakupa picha ya mradi wako au wazo lako litakavyo kuwa,pia linakusaidia kujua utalifikishaje mfano
  • Mfano:Utengenezaji wanishati ya mkaa kwa kutumia taka taka
  • Uanzishaji wa duka la kuuza bidhaa na nguo za watoto
  • Ukodishaji na uuzaji wa pikipiki (boda boda)
  • Uanzishaji wa blogu/tovuti ya habari za michezo
  • Uanzishaji wa blogu/tovuti ya kutoa mafunzo ya sekondari
  • Uanzishaji wa blogu/tovuti ya kutoa mafunzo ya kompyuta
  • Hapo juu ni mfano wa lengo kuu,hivyo kwanza lazima uelewe lengo kuu la kitu unacho taka kuanzisha au kufanya,ili ujue vizuri mradi wako au wazo lako
FANYA UTAFITI AU KUSANYA TAARIFA KUHUSU WAZO LAKO/UTAFITI WA SOKO NA WASHINDANI WAKO
  • Anza kukusanya taarifa kuhusu wazo lako,hapa fanya utafiti mdogo wa kujua ukweli wa kitu unacho taka kufanya hili kupata ukweli na kujua kwa upana zaidi kuhusiana na kitu unacho taka kufanya uhalali wa hicho kitu kulingana na sharia za nchi,maadali,Dini ili usije wekeza katika kitu ambacho kitakuletea matatizo
  • Tumia njia mbalimbali kama MTANDAO kutafuta taarifa ya kitu unacho taka kufanya kwani mawazo mengi tunayo taka kuyafanyia kazi tayari yalisha fanyiwa kazi hivyo kuondoa mgongano na uboreshaji ni vizuri kukusanya taarifa za kutosha,pia tunaweza fanya utafiti kwa kuuliza marafiki,ndugu,jamaa na watu mbalimbali
  • Katika utafiti unaweza fanya utafiti wa mambo yafuatayo
  • Utafiti wa soko
  • Utafiti wa washidani wako (kujifunza kutoka kwao)
  • Utafiti wa walengwa wako
  • Utafiti wa huduma au bidhaa tarajiwa
CHAMBUA TAARIFA NA BORESHA LENGO KUU
  • Umesha fanya utafiti na umesha kusanya taarifa mbalimbali kuhusiana na kitu unacho tarajia kufanya basi anza kuzichambua na kisha unaweza kuboresha LENGO KUU
ANDIKA WAZO LAKO
  • Kipengele muhimu sana andika wazo lako/andiko la biashara hapa utaandika kuanzia LENGO KUU ,MALENGO MADOGO,BAJETI NA MAMBO MENGINE MBALIMBALI KUHUSIANA NA WAZO LAKO,sehemu muhimu za andiko hili ni Kichwa cha Andiko(Title),Lengo kuu,Malengo mengine,Bajeti,Utangazaji wa biashara(Marketing strategy),Team(Timu) ,hii inakusaidia kuweza kutimiza wazo lako kwa utaratibu mzuri pia ANDIKO LA BIASHARA ni mwongozo mzima wa uanzishaji na uendeshaji wa biashara au mradi wako.
SAJILI WAZO LAKO ni vizuri ukasajili wazo lako hapa itategemea ni aina gani ya wazo unalotaka kulifanyia kazi lakini pia ni vizuri ukasajiri mapema kwenye vyombo au mamlaka husika ili uwe na hati miliki ya wazo lako
UNDA TIMU
WEKA FEDHA AU TAFUTA WADHAMNI
ENDELEA KUKUA ZAIDI NA KUFANYA TATHIMINI YA WAZO LAKO

Asante sana
 
Back
Top Bottom