Fanikisha mahusiano ya mbali. . . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fanikisha mahusiano ya mbali. . .

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Dec 11, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Watu hawaishi kuuliza kama inawezekana kuwa na mtu ambae yuko mbali nae na mahusiano yao yakasurvive.
  Jibu ni NDIO, ila kuna mambo ambayo mnatakiwa mzingatie ili mfanikishe mahusiano yenu.

  First things first...
  1.Kama wewe ni mtu ambae una "commitment issues" this is not for you.Kuweza kuvumilia kutokuwepo kwa mwenzio karibu kunahitaji kujitoa kwa hali ya juu na dhamira iliyonyooka.
  2.Kama humpendi mwenzako (unamtamani tu) this is not for you. Ukiwa unatamani kitu ambacho hukipati kwa wakati ni rahisi kuangalia kile kilichopo karibu yako.
  3.Kama humwamini mwenzi wako/mwenzi wako hakuamini wewe au wewe mwenyewe hujiamini this is not for you. Bila kuaminiana mtakua na mtafaruku kila siku. Umbali utasababisha maneno/kuwekana hatiani na kuhisiana vibaya kuwepo sana.Kitu ambacho kitasababisha ugomvi mara kwa mara na kusababisha mrudi nyuma kimahusiano badala ya kusonga mbele.
  4.Kama huna malengo ya mbali na mwenzako this is not for you. Ikiwa huoni ukiwa na huyo mwenzako miaka miwili mitatu mbeleni mwache aende tu. Hamna haja ya kumfunga mwenzako na mahusiano ya mbali wakati hana umuhimu sana kwako.
  5.Kama ni mwepesi wa kuchukua maneno ya watu bila kuyafanyia kazi this is not for you.Utaishia kupata presha bure na kugombana na mwenzio kila siku.
  6.Kama ni mvivu wa mawasiliano this is not for you. Kitu pekee kinachoweza kukuweka karibu na mwenzako wakati mko mbali mbali ni mawasiliano.E-mail, Simu, Texting, Skype n.k ndivyo vinavyoweza kupunguza umbali uliopo kati yenu walau kidogo.Hivyo kama hili huliwezi basi jua fika ni muda tu haujafika wa mahusiano yenu kuanguka.

  Kwa wale ambao wanafikiria kujiingiza kwenye mahusiano ya mbali jua inawezekana ikiwa tu una nia ya kuyawezesha mahusiano yenu.Kama huna bora uende uendako siku ukarudi na kumkuta mwenzako bado yuko yuko ndio ujaribu.

  Kwa wale ambae ndio wanahangaika nayo sasa hivi muhimu ni uwe mwaminifu,uwe na imani na mwenzako,ujitume kwenye swala zima la mawasiliano na msisahau kuongelea "them good times".Hii inasaidia kukumbushana umuhimu wenu kwa kila mmoja na kwamba japo mnakosana kwa muda, mtakapoweza kuwa karibu tena maisha yenu yatapendeza. Mjali mwenzako kwa maneno mazuri, epuka kuanzisha maugomvi yasiyo na pembe wala mkia, usimpe sababu ya kufurahia umbali wako.

  Mwisho. . . kama ni kucheat hata unaelala nae kitanda kimoja kila siku, unaekunywa nae chai kila asubuhi na kubebana kazini kila jioni anaweza kucheat, hivyo hili haliletwi na umbali bali tabia binafsi. Hivyo kama wewe ni mvumilivu go ahead and give it a try huku ukiomba na kuamini kwamba mwenzako nae yuko hivyo hivyo pia kama hajakupa sababu ya kufikiria vingenevyo.

  Nawatakieni LDS(s) zitakazovuka na kukwepa vikwazo. Kila la heri wote mnaohusika.

  PS
  Mawazo zaidi na experience zinakaribishwa.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kuna watu haya mambo hawayawezi full stop...
  wazee walisema fimbo ya mbali haiui nyoka......
  wazee wetu wana akili mno...
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hilo linaeleweka. . . hata kusoma sio kila mtu anaweza.

  Kuwa na mahusiano na mtu ambae yuko mbali requires a lot of discpline, which most people don't have.
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Lizzy,

  Unaongelea umbali gani? Na huo uhusiano utakaa hivyo kwa muda gani??

  Binafsi naamini naweza ila sipendi kabisa...!!! Labda kama kuna ulazima sana wa kuwa mbali na tena kwa muda mfupi tu!
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Babu naongelea umbali wowote, hata ule ambao mmoja anaweza kuwa upande wa pili wa dunia. Muda inategemea, hata kama atakuwepo huko kwa muda mrefu kidogo mkipanga vizuri na kujitoa mnaweza mkakutana mara kwa mara mpaka hicho kinachomweka mbali kiishe.
   
 6. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Thaaank yu for the thread sista,nimefumbuka macho indeed......
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kwa uzoefu wangu wanawake ndo wengi hawawezi
  mume anafungwa jela mwaka mmoja tu..
  akitoka anakuta 'nyumba ina harufu za watu wengine kabisa' lol
   
 8. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mimi ni wa hapa hapa nilipo cha kujifia?
   
 9. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mmmh ya wanaume je? ukigeuka tu kidogo upo safarini hata gari haijaondoka kituoni watu washahamia loh?
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kama mtu sio mwaminifu hata ukimpa kisogo tu atakua ashakonyezana na partner wake in crime achilia mbali kuwekwa jela au kusafiri kwa mwaka mzima.
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Karibu mwaya.
   
 12. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena
  Hekima ni Busara, PAW
  Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!
  [​IMG][​IMG]
  Kuwa na Busara
   
 13. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  wacheni kudanganyana hapa....long distance dnt work period.
  yange-work kama binadamu wangekuwa wakamilifu.
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ndio maana nikasema hili sio la kila mtu.Kila mtu afanye mambo kuendana na uwezo wake,hamna haja ya kulazimisha.
   
 15. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  mie naweza kabisa kabisa kama penzi la dhati liko
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Dec 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo wale ambao yao yamesurvive sio binadamu kama wewe? Unaedanganya ni wewe unaesema hamna anaeweza, wapo wanaoweza kama ambavyo wapo wasioweza. Muhimu ujue uko kwenye kundi gani bila kulazimisha kila mtu ajiunge na wewe.
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
   
 18. BORNCV

  BORNCV JF-Expert Member

  #18
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lecture nimeikubali!
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Sorry Lizzy,

  Bado naomba tu unifafanulie kidogo na pia unisamehe kama nitakuwa nakusumbua...

  Why long distance relationship kama kuna uwezekano wa kuwa na wallet yako mfukoni?? Yaani kwa nini kuwa katia halo hiyo?? Na hapa sijui hata ndoa inahusika???

  Kuna jamaa alinambia hivi...."Dogo DC, hakikisha wewe na familia yako mnaishi pamoja kama inawezekana. Huo ndio mpango wa mwenyezi Mungu. Don't allow the means of life to outweigh the meaning of life"

  Babu DC!
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Dec 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
   
Loading...