*Nukuu za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere katika Mikutano yake tofaut baada ya Uhuru*
1.Tumekubaliana kwamba tunataka kujenga Taifa lenye uhuru wa kweli,Siyo uhuru wa bendera tu,tumekubaliana kwamba tutaamua mambo yetu wenyewe kwa utashi wetu wenyewe na kwa manufaa yetu wenyewe
1971
2.Chama chochote kinapenda umoja kwa hivyo kinapenda Mshikamano wa Viongozi wake wakuu katika masuala yote muhimu.Na kama viongozi wanao msimamo huo kuwapinga tu kwa ajili ya kupinga ni jambo la Kipumbavu:
(Uongozi wetu na hatima ya Tanzania :63)
3.Daima hatutakubali kuwa vivuli,Vibaraka au Vijibwa vya Watu wengine au Taifa jingine.Hivyo tumeelewana sisi wenyewe na ndivyo dunia inavyotuelewa:
(Mwaka 1989)
4.Ujamaa Maana yake si kugawana Umaskini kwa usawa:Maana yake ni maendeleo ya watu wote na kugawa mali inayopatikana kwa haki kati ya wote walioizalisha ,Isipokuwa wale wenye haki ya kula bila kufanya kazi
(Mkutano Mkuu Maalum wa CCM 1985)
5."Zanzibar ikijitenga kutokana na Ulevi tu Sisi Wanzibara ina Wao Watanganyika wakumbuke kwamba Muungano ndiyo Unaofanya wanasema 'Sisi Wanzibar' Wao Watanganyika
(Nyufa: 10)
6.Viongozi wakigawanyika katika Makundi Chama pia huwa kimo katika hatari ya kugawanyika katika Makundi na kukosa shabaha yake"
(Tujisahihishe:11)
7.Viongozi wa Chama, Waliopo na waliong'atuka ,Wanapaswa kusaidiana na wananchi kuanzisha na kuendesha shughuli za Ushirika wa Uzalishaji mali
(Mkutano Mkuu wa CCM 1987:14)
8.Kazi ya Chama ni kuwa macho wakati wote kuangalia yanayotokea nchini,Kuielekeza Serikali.Chama kinahitaji kusikiliza maelezo yanayotolewa na serikali juu ya vitendo vyake na sababu zake
(Mkutano Mkuu Maalum wa CCM 1985)