BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linawashikilia watu saba, wakiwamo wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Kitarungu Wilayani Sereni kwa tuhuma za kuhusika kufanikisha ndoa ya wanafunzi hao wenye umri wa miaka 12 na 16 kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibushubwamu alisema watu hao wamekamatwa cha Getarungu baada ya polisi kupata taarifa za kiintelijensia.
Alisema nyumbani kwa wazazi wa bwana harusi' kulikokuwa na sherehe za ndoa. Aliwataja katika tukio hilo lililotokea wilayani Seren katika Kijiji polisi walifika wanaoshikiliwa Aprili 2 kuwa ni Nyang'ombe Magere (50) na Ghati Masero (38) ambao ni wazazi wa mtoto wa kiume aliyekuwa anaozwa.
Mwingine anayeshikiliwa ni Kibaki Rioba (23) mkazi wa Sirari Wilaya ya Tarime pamoja na watoto wenye umri wa miaka 12 na 16 waliokuwa wanaoana.
Polisi pia inamshikilia msimamizi wa ndoa hiyo batili kwa upande wa mwanamume ambaye pia ni mtoto mwenye umri wa miaka 10 (jina limahifadhiwa), darasa la pili Shule ya Msinggi Kitarungu," alisema Kamanda Tibushubwamu.
Akizungumza kwa sharti la kuhifadhiwa jina lake, mkazi mwanafunzi wa Kijiji cha Kitarungu alisema wazazi wa mtoto wa kike (16) anayesoma darasa la saba walipokea mahari ya ng'ombe Sita kutoka upande wa mwanamume ambaye ni mwanafunzi (12) wa darasa la nne.
Alisema baada ya wazazi wa mtoto wa kike kupokea mahari, walimkabidhi binti yao kwa mume wake mtarajiwa, maandalizi ya sherehe yakaanza nyumbami kwao mwanamume.
"Baada ya taarifa hizo kufika polisi, askari walivamia sherehe hiyo na kuwatia mbaroni watuhumiwa," alisema mtopa taarifa huyo.
Juliana Kobiro ambaye ni mdau wa haki za watoto mjini Musoma alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kuchukua hatua za haraka kudhibiti uvunjifu wa sheria na haki za watoto ulio karibia kufanyika, huku akiomba wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine.
Chanzo: Mwananchi