Familia ya Nd.Ally aliye uwawa na polisi kwa kupigwa risasi yaingia kwenye mvutano na Chadema

Nilimsikia Dr Slaa, kwenye taarifa ya habari akiongea na waandishi wa habari alisema anasubiri ripoti ya Daktari kuhusu mwanachama wao Ally...kumbe ulikuwa usanii mtupu siasa bana.

Hata wewe!?
 
Chadema mmestukiwa, mnaua halafu mnajipendekeza kusaidia shughuli za mazishi na kutupia lawama serikalini. Ole wenu siku yaja nayo i-karibu, mtaulizwa habari ya wangwe, rejia n.k. na mtakosa la kujibu.

TATIZO LA KUJENGA HOJA KWA KUTUMIA MAKALIo
 

Kauli kama hizi utajua tu kuwa ni za wapuuzi walewale wa Chama Twawala,yaani CCM.

Kwanza kichwa cha thread hii hakitakiwa kisomeke ati, "Familia ya marehemu Ally inavutana na CDM". Hii siyo sahihi hata kidogo.Isomeke kuwa, ''Familia ya marehemu Ally yavutana na Serikali au Polisi" kwa vile hawa ndiyo waliosababisha kifo cha marehemu. Ni ukweli ulio wazi kuwa kama Polisi wasingetumia nguvu kuzuia maandamano ya CDM nani angelipoteza uhai pale Morogoro???

Haingii akilini kutaka kuwashawishi watu kwamba CDM ndiyo wanahusika na kifo cha marehemu Ally. Kila mtu ni shuhuda kwamba CDM walianza kampeni zao za OpSangara/M4C kwa takribabi wiki tatu katika mkoa wa Morogoro. Kama CDM kweli ndiyo walikuwa na mpango wa kuua raia kutokana na mikutano yao hiyo mbona hatukusikia habari za mauaji sehemu zingine???

Serikali,Policcm na CCM acheni kuwafanya Watanzania kuwa hawana akili! One day you gonna pay for this. Kama siyo kwa ICC ya Ocampo it will be any other tribunal whether local or international. But you have got it coming!
 


Ni wadhaifu sana ndio maana wanakurupuka na kuropoka manbo ya uzushi.
 
ccm haiwezi kuua lakini chadema wanakuja kasi kweli,walianzia na chacha wangwe,wakaua raia watatu arusha wakaenda igunga wakala mmoja na mwingine wakammwagia tindikali.majuzi wakaua iramba na sasa ally wa morogoro.waha jamaa ni mafia kweli kweli.
We ni mpumbavu kweli sijawahi ona yani unatumika bila hata kujua??? Nape siku hizi kasitisha halipi tena acha ujinga kilaza wewe
 

Hii nayo naona inatoka mabwepande.
 
Pole, wewe na ccm lenu moja
 

Hii ya Kutelekeza Barabarani Imekaa vizuri!! Mwenye ile Picha ya jeneza kutupwa barabarani Tunaomba atuwekee Hapa Tafadhali!!
 
ccm wamepata propaganda lakini wananchi tunaelewa kinachoendelea.!
 
serikali itauaje wakati aliekuwa na maandamano ni chadema
Kama huna cha kujibu ndugu si uwe unapita tu, Hivi kifo kikitokea katika maandamano yaliyofyatuliwa risasi na polisi(Serikali) basi basi walioua ni wenye maandamano kweli fikra zako ndugu ni fupi kama ID yako inavyojionyesha
 
Siasa za CCM zimefikia kiwango ambacho ni chini ya kiwango cha binadam toka uumbaji. Ok Zomba, Ritz na wasaidizi wote wa Nape tahadhari ni kuwa haya mnayoyshabikia sasa ombeni Mungu yasiwapate hata 1%.

Toka Polisi walipotenda uhalifu ule humu JF ziliandikwa zredi kadhaa zenye tahadhari juu ya mpango wa ccm kutumia kifo cha Zona (R.I.P.) kisiasa; na kweli CCM wamefanya yote kama yalivyoandikwa. CCM kimekuwa maajenti wa mauti. CCM kimepoteza sifa na uhalali wa kuwa chama cha siasa Tz.
 
Ni wadhaifu sana ndio maana wanakurupuka na kuropoka manbo ya uzushi.

Mtaji wa ccm vilikuwa ni umaskini na ujinga wa wananchi wa Tz. M4C imefanya kazi na kwa sehemu kuna mafanikio. Lakini nina masikitiko kwa baadhi ya wanafamilia ya marehemu Ally kudhihirisha kuwa kazi ya ukombozi bado inahitajika iongezwe zaidi. Wamekubali kutumiwa na ccm malipo ya kipande cha mkate na kumsaliti marehemu ndugu yao. Hao waliofanya unafiki huu tutasikia mwisho wao, hauwezi kuwa mzuri hata kidogo.
 

Aliyerubuniwa na Magamba ni shemeji wa Marehemu Ally. Yeye pia ndo msemaji wa familia. Nimemdharau sana yule mzee. Tena yeye ndo alikuwa anakwamisha zaid CHADEMA wasitoe chochote ili alalame.. Ushahd wa video alipokuwa anapewa rambiramb upo wazi kabisa.
 
Chadema mmestukiwa, mnaua halafu mnajipendekeza kusaidia shughuli za mazishi na kutupia lawama serikalini. Ole wenu siku yaja nayo i-karibu, mtaulizwa habari ya wangwe, rejia n.k. na mtakosa la kujibu.
inaonekana chadema wana agano na israili hufi mpaka wakue wenyewe
 
Hebu jaribu kupunguza utoto hasa hapo sentensi ya mwisho!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…