Familia ya Nd.Ally aliye uwawa na polisi kwa kupigwa risasi yaingia kwenye mvutano na Chadema

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Katika hali ya kushangaza familia ya ndugu ally imelalamika kuwa imetalekezewa msiba kwani haijapewa msaada wowote toka chama cha demokrasia na maendeleo.

Wala taasisi yeyote ya serikali kufuatia msiba wa ndugu yao aliyefariki katika ghasia zilizotokea kati ya polisi na wafuasi wa Chadema.

Msemaji huyo wa familia amelalamika kuwa hakuna kiongozi yeyote wa Chadema aliyewasaidia hata kusafirisha mwili wa marehemu hadi ulipofika nyumbani kwao mkoani tanga.

kufuatia hali hiyo katibu wa Chadema mkoa wa tanga alipo ulizwa kulikoni hawajatoa msaada wowote kwa familia ya marehemu.

Katibu huyo alisema alipokea maagizo kutoka Chadema makao makuu kwaajili ya kushughulikia msibahuo toka mwanzo hadi mwisho,lakini imekuwa vigumu kwani walikosa kabisa ushirikiano na familia hiyo.

Katibu huyo aliendelea kulalamikia familia hiyo kuwa walijitenga nao kwani kila mwanafamilia aliye fwatwa kwaajili kufanikisha safari hiyo ya mwisho Ng.Ally walikwepa na kila mmoja akisea hausiki na maswala hayo.

Katibu huyo aliendelea kusema bado hawajakata tamaa na kuwa bado wanaendelea na juhudi za kutafuta mawasiliano na familia hiyo.

KWAKO TUMAINI MAKENE CHAMA KINASEMAJE JUU YA HILI,LISIJE LIKACHAFUA SURA YA CHAMA CHETU.

CHANEL 10

Chadema mmestukiwa, mnaua halafu mnajipendekeza kusaidia shughuli za mazishi na kutupia lawama serikalini. Ole wenu siku yaja nayo i-karibu, mtaulizwa habari ya wangwe, rejia n.k. na mtakosa la kujibu.
 
Policcm walipoua watu Arusha walijaribu kuwarubuni familia za marehemu bila mafanikio kutokana na msimamo wa familia za wafiwa.
Policcm walipoua watu nyamongo Tarime walijaribu kuwarubuni familia za wafiwa bila mafanikio hatimaye wakaamua kupora miili ya marehemu na kwenda kuitelekeza porini na barabarani.
Policcm wameua mtu morogoro kama kawaida yao wamejaribu kuirubuni familia ya marehemu na hatimaye wamefanikiwa na sasa tunashuhudia vibweka toka kwa ndugu wa marehemu!
 
Chadema mmestukiwa,
mnaua halafu mnajipendekeza kusaidia shughuli za mazishi na kutupia
lawama serikalini. Ole wenu siku yaja nayo i-karibu, mtaulizwa habari ya
wangwe, rejia n.k. na mtakosa la kujibu.

mkuu nimekudharau sana
 
ndugu wa marehemu walikataa maiti ya ndugu yao ally kuwekwa hadharani, chadema walitaka kutumia msiba kufanya siasa, ndugu wakawaambia sheria ya dini yetu hairuhusu kuaga maiti kama hamtaki anza mbele. wakaondoka kuelekea iringa kufanya vurugu wapate maiti nyingine.
 
Chadema mmestukiwa, mnaua halafu mnajipendekeza kusaidia shughuli za mazishi na kutupia lawama serikalini. Ole wenu siku yaja nayo i-karibu, mtaulizwa habari ya wangwe, rejia n.k. na mtakosa la kujibu.

mbona nyie mnateka na kutesa.
 
Undumilakuwili siyo mzuri. CCM wamewarubuni ili kukataa ushirika na CHADEMA na kuficha ushahidi na baada ya mazishi CCM wameendelea na usanii wao kama kawa kwani kwao Mission is accomplished na hao jamaa baada ya kuona hawakupata kitu kwa CCM ndo sasa wanaikumbuka neema ya CHADEMA waliyoikataa. They can clearly distinguish between CDM and CCM
 
Katika hali ya kushangaza familia ya ndugu ally imelalamika kuwa imetalekezewa msiba kwani haijapewa msaada wowote toka chama cha demokrasia na maendeleo.

KWAKO TUMAINI MAKENE CHAMA KINASEMAJE JUU YA HILI,LISIJE LIKACHAFUA SURA YA CHAMA CHETU.

CHANEL 10

Ndio maana naipenda JF, hii habari ilikuja jana hapa jamvini kama tetesi kuwa Familia imenunuliwa ili waseme hayo waliyosema sema. Sasa tunaweza thibisha kuwa haikuwa tetesi bali ni kweli tupu........Hawa familia wanafanya jambo baya sana, huku ni kumdhalilisha marehemu https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/315166-ccm-wakishirikiana-na-jeshi-la-polisi-tanga-wamewanunua-ndugu-wa-marehemu-ally-4.html
 
Nilimsikia Dr Slaa, kwenye taarifa ya habari akiongea na waandishi wa habari alisema anasubiri ripoti ya Daktari kuhusu mwanachama wao Ally...kumbe ulikuwa usanii mtupu siasa bana.
 
Acha pumba ndugu, hivi unategemea CDM waue na serikali ikae kimya basi hatuna serikali kama ipo basi ndo iliyoua na ndo maana imekaa kimya.

serikali itauaje wakati aliekuwa na maandamano ni chadema
 
ndugu wa marehemu walikataa maiti ya ndugu yao ally kuwekwa hadharani, chadema walitaka kutumia msiba kufanya siasa, ndugu wakawaambia sheria ya dini yetu hairuhusu kuaga maiti kama hamtaki anza mbele. wakaondoka kuelekea iringa kufanya vurugu wapate maiti nyingine.
dah! Huu ndio uwezo wako wa kufikiri? Pole sana
 
Policcm walipoua watu Arusha walijaribu kuwarubuni familia za marehemu bila mafanikio kutokana na msimamo wa familia za wafiwa.
Policcm walipoua watu nyamongo Tarime walijaribu kuwarubuni familia za wafiwa bila mafanikio hatimaye wakaamua kupora miili ya marehemu na kwenda kuitelekeza porini na barabarani.
Policcm wameua mtu morogoro kama kawaida yao wamejaribu kuirubuni familia ya marehemu na hatimaye wamefanikiwa na sasa tunashuhudia vibweka toka kwa ndugu wa marehemu!

kila mahali wanapopita chadema lazima damu imwagike.hiyo ni laana kuu
 
Hizi siasa za Tz sasa zimefika pabaya, sikutwgemea msiba wa Ally Zona ungetumika kama mtaji wa kisiasa na kutugawa kiitikadi. Napenda kutoa angaliz, tunapoelekea ni kubaya na si rahisi kurekebisha.
 
Nilimsikia Dr Slaa, kwenye taarifa ya habari akiongea na waandishi wa habari alisema anasubiri ripoti ya Daktari kuhusu mwanachama wao Ally...kumbe ulikuwa usanii mtupu siasa bana.
Usanii upi Ritz? hakuna taarifa thabiti PM ilifanyika saa ngapi nani walikuwepo wakati inafanyika, pia hata maiti ya mpendwa wetu Ally imesafirishwa kinyemela kwa kuwarubuni ndugu wa marehemu hususani shemeji yake, na baada ya kuona lengo lao la kutorosha maiti na kuizika ndo wakaamua na kutoa majibu ya PM yaliyostaajabisha ambayo unayajua. Kilichofanyika hapo CCM na Polisi wamejifanya kupoteza ushahidi ambao hauwezi kupotea kirahisi hivyo.
 
ndugu wa marehemu walikataa maiti ya ndugu yao ally kuwekwa hadharani, chadema walitaka kutumia msiba kufanya siasa, ndugu wakawaambia sheria ya dini yetu hairuhusu kuaga maiti kama hamtaki anza mbele. wakaondoka kuelekea iringa kufanya vurugu wapate maiti nyingine.

stupid comments!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom