MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,612
- 21,346
HARMORAPA,rapa anayetikisa soko la mziki barani Afrika na vibao vyake kadhaa kama UTHIGAWE PATHI na vingine vingi vinavyopigwa na vituo mbalimbali vya kimataifa amejikuta anaingia kwenye migogoro isiyo na maana na familia ya Mose Iyobo.
Ugomvi kwa mara ya kwanza ulianza baada ya Harmorapa kununua gari baada ya singo yake kuongoza mauzo ya mtandao kwa downloads nyingi ambapo Mose Iyobo hakufurahi nakuamua kumuita nyani,Jamani eti nyani gani anapata watoto wakali kama wale?
Kama hiyo haitoshi Harmorapa alipoweka mipango yake ya kununua nyumba South Afrika,ambapo alimtuma AliKiba kumuulizia bei, mchumba wa Iyobo ameibuka na kudai ''Simkubali Harmorapa maana hana kipaji cha muziki anatumia nguvu nyingi sana", lkn wadadisi wa mambo wanadai Aunty Ezekiel kuna movie anataka kuitoa hivyo anataka kutumia jina la Harmorapa kuipa kiki movie yake.
Wadau wa rap ambao mara kadhaa wamekuwa wakimuweka Harmorapa kwenye lane moja na mtu kama Biggie hasa kwa aina zao za flow,wameshauri rapa huyo kuongenza ulinzi kwny misafara yake ambayo mara kadhaa husababisha barabara kadhaa kufungwa.
Mdau nini maoni yako kuhusu hizi chuki dhidi ya Tanzanias finest?