Familia ya Kidosi yalazwa nje ya Nyumba Arusha,So latinga Polisi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Familia moja ya watu zaidi ya 10 yenye asili ya kiasia wakazi wa eneo la Sabena katikati ya jiji la Arusha,hawana mahala pa kuishi kufuatia nyumba yao kuvamiwa na kuvunjwa na vitu kutolewa nje katika mgogoro wa Kifamilia unaoendelea.

Tukio hilo limetokea leo majira ya asubuhi ,ambapo kundi la watu wapatao 20 walivamia katika nyumba hiyo na kuanza kutoa nje vitu mbalimbali vya ndani huku wakidaiwa kufanya uharibifu wa Mali na uporaji.


Akizungumzia kadhia hiyo baba wa familia hiyo,aitwaye Zaneed Salahe amesema kuwa watu hao walivamia nyumba yao wakiwa wameambatana na mwenyekiti wa mtaa na kuanza kuvunja makomeo ya nyumba yao na kutoa vitu nje bila kuwashirikisha.

Alisema mgogoro huyo ni baina yake na mtoto wa baba yake Mkubwa aitwaye Murtaza mkazi wa jijini Dar anayedaiwa kuratibu zoezi la uvamizi wa makazi yake na kutoa samani za ndani nje ya nyumba huyo.

"Huyo Murtaza anatumia fedha za marehemu baba yetu kutunyanyasa ametuma watu waje kututoa kibabe ndani ya nyumba bila kuwa na kibali cha Mahakama wala kikao cha familia" Amesema

Amesema wakati watu hao wakitekeleza zoezi hilo, yeye alikuwa safarini akielekea nchi jirani ya Kenya na kulazimika kurejea haraka nyumbani , huku mkewe aitwaye Chandni Hanif Hussein akiwa amewapeleka watoto wake shuleni.

Amesema ndani ya nyumba yao kulikuwa na kiasi cha sh,million 10 pamoja na fedha za kigeni dollar 1000 fedha wanazotumia kwenye biashara yao ya M pesa ,ambazo zinadaiwa kupotea wakati kundi hilo LA watu wakitoa vitu nje.

Mama wa familia hiyo,Chandni Hussein alisema kuwa tukio hilo limewafedhehesha sana na mpaka sasa hawajui watalala wapi na wameiomba serikali iingilie kati iweze kuwasaidia kwa kuwa suala hilob linatokana na mgogoro wa Kifamilia kati ya mumewe na ndugu zake kuhusu Mali zilizoachwa na marehemu baba yao.












IMG-20190221-WA0004.jpeg
IMG-20190221-WA0006.jpeg
IMG-20190221-WA0007.jpeg
IMG-20190221-WA0007.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • VID-20190221-WA0008.mp4
    11.2 MB · Views: 15
Back
Top Bottom