Falsafa ya uongozi na mbio za Marathon

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
284,235
738,452
Mbio za marathon ni tofauti kabisa na mbio fupi za mita mia au mia mbili , zote hizi ni mbio lakini zinatofautiana ukimbiaji, mbio za marathon zinataka pumzi wakati zile fupi zinataka kasi

Kwenye uongozi nako ni hivyo hivyo uongozi wa kikao cha harusi ni tofauti kabisa na uongozi wa taasisi, ukikurupuka tu imekula kwako.

Makonda kaishiwa pumzi hasikiki tena alikurupuka akitaka kukimbia mbio ndefu kwa mbinu za mbio fupi.

Akitokea UVCCM alipanda haraka ngazi za kiuongozi hata kufikia kuwa mkuu wa mkoa wa Dsm jiji lenye changamoto nyingi sana...akataka kwenda na kasi hiyo ya kupanda vyeo na utendaji kazi.

Yule Makonda wa kwenye media na ukaguzi wa kushtukiza amepwaya na kupotea hii ndio bye bye.

Kifuatacho ni kushuhudia uongozi mbaya pengine kuliko mwingine wowote katika mkoa wa Dsm Kwa nafasi ya ukuu wa mkoa..a

Muda huongea
 
Ni falsafa hiyo hiyo ambayo hata mkuu wa kaya na watendaji wake wengi wanashindwa kabisa kuifuata ukianzia kwa Mapi Makonda na msururu mrefu tuu bila kumsahau kigwangala Makamba nk nk.

Hakuna tena kutumbua jipu serikali imelemewa na kesi zilizoko mahamani wanaofaidi kwa sasa ni wanasheria.

Operation zote zimesimama na pengine hazitaendelea tena bomoabomoa na kurudisha maeneo ya wazi zimebaki story
 
Head of the state pumzi imekata au inakaribia kukata, ile amsha amsha haipo tena ule msisimko wa leo kunani haupo tena! Je ndio kuna kufufuka tena au ndio kwaheri?
 
Makonda ameteuliwa kuwadhibiti wapinzani DSM, maadamu upinzani upo kazi yake ipo. Pumzi itakata kwenye mambo mengine ya kuleta maendeleo maana huko kunahitaji mtu mwenye uwezo wa marathon na sio kasi ya mita mia.
 
Makonda ameteuliwa kuwadhibiti wapinzani DSM, maadamu upinzani upo kazi yake ipo. Pumzi itakata kwenye mambo mengine ya kuleta maendeleo maana huko kunahitaji mtu mwenye uwezo wa marathon na sio kasi ya mita mia.
Matatizo yameshaanza kuonekana kwenye maeneo mengi
Wizi unachipuka kwa kasi, Vibaka ni kama wamezaliwa upya
Panya road na makundi mengine ya jinsi hiyo
Uchafu
Ishu ya sukari inaonekana wazi sasa ni mfupa ulioshindikana
 
Wiki chache zijazo tunaweza kushuhudia maamuzi ambayo yanaweza kuligharimu taifa hasa kama wa udom wataamua kuandamana na upinzani kutoa support
 
Back
Top Bottom