Falsafa ya Hekima,Busara na Uvumilivu KTK Utawala bora

Mwana Kwetu

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
652
562
Hakuna mpenda maendeleo atakayepinga kuwa Hekima, Busara na uvumilivu ndizo sifa kuu muhimu zinazotofautisha na kufikia mtu kuitwa a "GREAT LEADER". Hivi ndivyo vinavyomfanya kiongozi yeyote kufikiri habari za kuleta maendeleo badala ya kuchochea chuki miongoni mwa watu wa itikadi tofauti za kidini na kisiasa pia ndizo zinazomfanya kiongozi kuachilia na kusamehe badala ya ku advocate na kushawishi kulipiza visasi. Kwa kawaida visasi vinamfanya mtu au kikundi cha watu kutosonga mbele na badala yake kucheza mchezo hatari wa kuviziana' tit for tat'.
Haya siyo maisha bali ni vita.
Kiongozi asipotambua kwamba yeye ni baba wa jamii anayoongoza siyo rahisi kuwa na uvumilivu, hekima wala busara kwani badala ya kutatua changamoto zilizopo utajikuta unatengeneza chuki na kuongeza uhasama. Kwa kawaida baba anapoona watoto wanagombana au hawaelewani hujitahidi kusimama katika na siyo kumchochea mtoto mwingine ampige yule aliyemkosea. Kiongozi ni jalala na ni lazima ajue anapoongopoza siyo watu woote watakao mkubali na hivyo ajiendae ku prove kuwa waliomteua au kumchagua hawakukosea. Lakini ukiona kiongozi anapotumia muda mwingi na rasilimali kupambana kwa nguvu na wachache wanaompinga badala ya kuleta maendeleo kwa wengi wanaomunga mkono ujue kiongozi huyo hajitambui wala hajiamini yaani hana CONFIDENCE.
Ni vema akumbuke kati ya wanaomuunga mkono wana ndugu zao wanaompinga vilevile na ndio maana busara inatakiwa itumike kuleta maridhiano badala ya kuongeza mpasuka ukifikiri unatengeneza.
Hekima na Busara ndizo zilizomfanya Nabii Sulemani awe tofauti na viongozi wengine hadi kutembelewa na Malkia wa Sheba kutaka busara zake.
Utawala wa maguvu wa kudhibiti, kufukuza na kuwakamata wanaokupinga mara nyingi hata Mungu anapingana nao ni hivyo kubomoka kwa muda mfupi badala ya kujengeka. Tunaposoma hadithi za akina Nebkadnessa na Belshaza tunapata mafunzo ya jinsi viongozi waliotaka kuabudiwa na kusifiwa walipogeuka kuishi porini na kula majani kama wanyama kutokana na kipigo toka kwa Mungu.

Kiongozi kama jalala tukubali kuvumilia kwani tusijiwekee mazingira ya kushabikiwa hadi kudhalilika kama yule mfalme mjinga aliyedanganywa ameshonewa nguo special kumbe alikuwa uchi wa mnyama na hata alipopita mbele za watu wake wakamshangilia kwa kuogopa kusema yuko uchi wasije wakauawa. Mfalme yule mjinga alisikia mtoto akisema innocently "the king is naked" ndipo alipong'amua kuwa wenye busara walificha busara zao wasije wakauawa. Viongozi wasisubiri hali ifike huko ni muhimu wakajitambua mapeeema.
Balanced decision making itatokana na hekima , busara na uvumilivu tu na si vinginevyo.
Ukichukua metaphor ya baba viongozi watagundua kuwa ukiwa na watoto wawili hadi watano hawafanani kitabia na kwa sababu ni wa kwako huchoki kuwashauri na kuwasimamia ili mwisho wa siku muweze kuongea lugha moja. Sijamwona baba anaua , au kupiga tu watoto kwa sababu wanatofautiana naye bali busara lazima imsaidie jinsi ya kuishi nao co exist.

Maamuzi yote yanayofanywa katika muktadha wa Hekima ,Busara, Uvumilivu huambatana na usikivu wa upande mwingine. Maamuzi ya namna hii hayaleti majuto wala malalamiko bali furaha , sifa na heshima kwa viongozi. Kinyume chake ni malalamiko, upinzani na manung'uniko na hatimaye kujenga nidhamu ya uoga haswa kwa viongozi wa chini. Na hii inapelekea kiongozi ajitune kwenye interest ya kiongozi mkuu then afanye maamuzi kwa kuangalia impact yake. Hali hii kwa kawaida huwafanya viongozi wa chini kushindwa kuwa wabunifu hivyo kutofanya kazi kwa weledi.
 
Back
Top Bottom