Falsafa ya CHADEMA ni hii, ya CCM iko wapi?

Namuombea samahani sana kwa kukuumiza, sikupenda iwe hivyo naye kakubali, ila ailitaka ufikirie kuhusu neno demo-cracy halafu umma na nguvu yake. Narudia anaomba samahani kwa kukuofend.
Napenda kukushukuru kwa kunisaidia kuomba radhi, Nisaidieni ninapo onewa. "MUNGU AKUBARIKI KWA MOYO WA UPENDO"
 
Wanabodi,

Wananchi wanataka kujua ni nini hasa sera na itikadi inayosimamiwa na Chadema mlianza na falsafa ya oparesheni sangara katika kile mnachodai kupambana na mafisadi nchini, lakini falsafa hiyo imetupwa na kurukia falsafa nyingine ya vua gamba vaa gwanda, kabla ya falsafa hiyo nayo kuyeyeka njiani na sasa wananchi wanashangaa kuja na falsafa nyingine ya M4C.

Profesa mmoja kutoka Ujerumani amefichua falsafa ya M4C inatumiwa na Chadema baada ya wafadhili wa nje kukibana chama hicho kueleza namna kinavyotumia fedha kinazopewa, kwa mujibu wa Profesa huyo, falsafa ya oparesheni sangara na ile ya vua gamba vaa gwanda hazina tafsiri nzuri ya kisiasa inayoweza kueleweka mbele ya wafadhili, wanataka falsafa ya vuguvugu la mabadiliko M4C.

Chadema katika mikutano yao ya M4C wamekuwa watu wakulalamika tu kuhusu ufisadi, hali ngumu ya maisha na umasikini lakini hawasemi wao watafanyaje kuondoa umasikini huo, karibia majimbo yote yanayoshikiliwa na Chadema yanakabiliwa na changamoto nyingi zinazohusu kero za wapiga kura wao, badala ya wabunge hawa kwenda majimboni kukaa na wananchi wao kuona ni namna gani wanaweza kuzitatua kero kazi wao kazi kupuyanga na hovyo na hiyo M4C wanasahau wamebakiwa na miaka miwili kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mwingine.

Miaka miwili kisiasa ni michache mno kama hujafanya kitu chochote cha maana hadi sasa, huwezi kukifanya tena ndani ya muda huo uliobaki.
 
Mkuu
"Operesheni Sangara" ni Falsafa??

Naona umeanza kuchanganyikiwa!!

Tulia tu, si lazima uongee na kujishushia heshima!
 
Mkuu
"Operesheni Sangara" ni Falsafa??

Naona umeanza kuchanganyikiwa!!

Tulia tu, si lazima uongee na kujishushia heshima!

Umeniwahi (na umenisemea niliyotaka kusema)! Magamba hayajui tofauti kati ya sera, falsafa na operation!
 
Mkuu Ritz,
Hizo sio falsafa...Ni Kaulimbiu!
Kaulimbiu huwa haidumu, inasoma tu upepo wa kipindi hicho na huisha.
Labda tukufundishe; mfano ni mwenge ule wa ccm, kila mwaka mkiupitisha kuroga watu kunakuwa na kaulimbiu au ujumbe tofautitofauti...kuwa mwelewa jombaa!
Falsafa ni mawazo mapana sana ya msomi ambayo anaamini kuwa yanaweza kugeuzwa katika vitendo na kuonekana hadharani; mfano falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea.
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri hujui maana ya falsafa, tofautisha falsafa itikadi na moto (slogan) wakati wenzio wanaongeza wanachama na majimbo wewe kalia kuongelea falsafa!! kwaheri:israel:
 
njaa mbaya sana.! Unafanya na kusema lolote ilimradi wewe na watoto wako mpishane kwenda chooni.!
 
UNAZI wa kichama kama CCM au CHADEMA si hoja za kimsingi bali mashiko yake katika jamii, falsafa ya operation sangara ni kufahamisha umma kuwa CHADEMA ni chama cha siasa ambacho kimedhamiria kushika dola, na pia vua gamba vaa gwanda ni msemo katika jami kuuleza umma kuwa ufisadi si jambo jema vyema kuvaa gamba tujenge nchi.

Pia M4C, ni namna cdm inavyowajibika kisiasa hasa kuwafikia umma na kutoa elimu ya uraia na wajibikaji katika demokrasia.

Chama chochote cha siasa hakiwezi kuwa hai bila kuwalisha wanachma wake uhai wa chama na pia kupta wanachma wapya.

M4C ni namna ya kupata mtaji katika jamii wa kufikia umma mkubwa badala ya kukaa maofisini na kwnye vyombo vya habari pekee. M4C imedhamiria kufikia jamii yote bila kusubiri kampeni za uchanguzi ili kujitanua na kupata wapiga kura wengi wenye ufahamu. Kwahiyo havifi bali ni dhana ile ile.

Pia chama hakiko kwa ajili ya wafadhiri bali wanachama wake na umma kwa ujumla. Hivyo ni vyema kuwapa ufahamu wa msitakabari wa nchi na sera zinazotekelezeka.

Kwahiyo hapa hakuna propaganda ya wafadhili huo ni upuuzi wako wafadhili hawawezi kujenga chma bali umma ndo unaojenga chama.

Hayo unayoelezea ni utumwa wa fikra potofu na pia uzadiki wa kutumwa na akina Nape.
 
Mkuu
"Operesheni Sangara" ni Falsafa??

Naona umeanza kuchanganyikiwa!!

Tulia tu, si lazima uongee na kujishushia heshima!

Naona unataka kujivunjia heshima yako humu Jamvini tofautisha sera na falsafa...Chadema sera zao ni za kibepari na ndio maana mfadhili wake mkuu wa nje ni chama cha Conservative cha Uingereza ambacho ni cha mapepari.
 
Mkuu Wangu.
Ni bora ujiandae kuhesabiwa tu, hakuna hoja ya msingi unayoweka hapa!
Kumbuka watakao hesabiwa Usiku ni wale wenye mahitaji maalumu, usifungulie mtu usiku usije pelekwa Mabwepande!
Naona unataka kujivunjia heshima yako humu Jamvini tofautisha sera na falsafa...Chadema sera zao ni za kibepari na ndio maana mfadhili wake mkuu wa nje ni chama cha Conservative cha Uingereza ambacho ni cha mapepari.
 
Naona unataka kujivunjia heshima yako humu Jamvini tofautisha sera na falsafa...Chadema sera zao ni za kibepari na ndio maana mfadhili wake mkuu wa nje ni chama cha Conservative cha Uingereza ambacho ni cha mapepari.
Hao viongozi CDM wamelimbikiza shs Ngapi kwenye hizo bank za Uswisi? Mimi nachoona uji wa pilipili uliokuwa unatumia umekufanya uwe mwehu
 
Humu naona kuna level tofauti za elimu, sio kosa kujifuna litz! Jifunze utaelewa tuu baada ya muda! Ila ongeza bidii
 
Mkuu Ritz,
Hizo sio falsafa...Ni Kaulimbiu!
Kaulimbiu huwa haidumu, inasoma tu upepo wa kipindi hicho na huisha.
Labda tukufundishe; mfano ni mwenge ule wa ccm, kila mwaka mkiupitisha kuroga watu kunakuwa na kaulimbiu au ujumbe tofautitofauti...kuwa mwelewa jombaa!
Falsafa ni mawazo mapana sana ya msomi ambayo anaamini kuwa yanaweza kugeuzwa katika vitendo na kuonekana hadharani; mfano falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea.

Mkuu usilete mazoea Movement for Change M4C ni Falsafa ambazo wafadhili kutoka nje ya nchi wanazitumia kwa Chadema, ukienda Zimbabwe kwa Morgan Tsinvagirai kuna MDC, ukienda Uganda kuna A42, ukienda Kenya kuna ODC Raila Odinga..

Wafadhili wa hivyo vyama hiyo ndio falsafa yao wanawatumia lakini nyie ambaye mnatumia hamjui chochote masikini mnatumiwa kama madodoki.
 
Last edited by a moderator:
Hebu tueleze na hizi vipi

Siasa ni kilimo,kilimo uti wa mgongo na sasa kilimo kwanza.

Yaani bandika bandua alafu utekelezaji zero.
 
Back
Top Bottom