Falsafa ya CHADEMA ni hii, ya CCM iko wapi?

Hawa wanasiasa wa Kitanzania wote wapo sawa tu... Waliokuwa chama tawala na walioko nje ya chama tawala lengo lao moja tu... Maneno matamu kuyasikiliza, lakini matendo yao yanatia kinyaa kuyaona.

Nailinganisha Tanzania na mistari hii:

Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.
Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na hao ni wachungaji wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.
Husema, Njoni, nitaleta divai, Na tunywe sana kileo; Na kesho itakuwa kama leo, Sikukuu kupita kiasi.

Isaya 56:10-12

Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.

Q28:77

“Wala msitii amri za walio pindukia mipaka, ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi”.

Q 26:151-152
 
Hujalitendea haki neno falsafa. Hujalipa mapana yanayostahili. Itikadi/ideology kwa mtazamo wangu ndio falsafa ya chama. Pale chama kinaamua kufuata mkondo upi. Sera zake zimelala wapi. Chama kinaamini katika nini. Ni ipi mikakati ya muda mfupi na mrefu, n.k
 
Jamani jamani mbona magamba mazito kiasi hiki Nape Nnauye utaanzia wapi mzee mpaka CCM kije kianze kung'ara???

Kwani mpaka leo hamjajua falsafa ya CCM mbona iko wazi kabisa..

Angalia aliyofanya Lowana Kuchota mabilioni hadi Nyerere akamshtukia...

Ona aliyofanya Rostam na kampuni yake ya Caspian

Manji na kashfa ya Quality plaza

Mkapa na kiwira na hotel africa ya kusini

Jk na hotel ya serengeti na ikulu ya chalize

mramba na PrecisionAir wizi mtupu..

Mgonja na jengo refu kupita yote arusha next to Golden Rose hotel

yona na kuuwa General tyre na yeye kuwa agent wa tyres kutoka china na kwingineko..

KWA KIFUPI FALSAFA YA CCM NI CHUKUA CHAKO MAPEMA... KWANI WATANZANIA NI WAJINGA NA HAWAJASOMA..

SASA ITAWATOKEA PUANI...
 
Naomba kuuliza swali moja tu, hivi hii imesomwa na wale wasomi waliopo kwenye pay roll yenu kama akina baregu na Kitilla? hivi hata maana ya falsa nayo mfundishwe?

Falsafa ina maana zaidi ya moja - kama nne hivi kutokana na Cambridge dictionary. Sasa yawezekana wewe umeshikilia ambayo haifit kwenye context hii!
 
Ujamaa ni nini?:lol: Na azimio la Arusha bado lipo, maana nipo mbali na Tanzania.

Hebu some hapa chini:

Chama chetu ni miongoni mwa vyama vichache katika Afrika ambavyo vimefaulu kubuni nadharia ya ujamaa iliyo sahihi, wazi na ya kiwango cha juu. Nadharia hiyo ya Chama inajidhihirisha yenyewe katika Katiba, Azimio la Arusha, Mwongozo na maandishi mengine muhimu ya Chama. Nadharia hii ya siasa yetu ya Ujamaa na Kujitegemea imetujengea msingi wa uelewano, umoja na ushirikiano wa aina mpya katika ujenzi wa taifa na kutufanya tueleweke na wengi kimataifa, jambo ambalo limetupa sifa na heshima duniani kote.​
Ni Ujamaa gani na Azimio lipi la Arusha mnalolisema? ni ule mliounajisi kwa kuweka Azimio la Zanzibar na kuanza wimbi jipya la uporaji mali za serikali na nchi? Ni kichaa tu ndiye anayeweza kuaamini CCM ya sasa ni ya falsafa za kijamaa kutokana na yanayojiri ambayo yanathibitisha jambo moja tu, nalo ni kwamba falsafa ya Ujamaa ilishauwawa muda mfupi tu tangu mwasisi wake alipoachia ngazi yaani alipong'atuka.
Mwenyewe alifahamu hivyo na alisema waziwazi na mara nyingine kukemea alipoona CCM na serikali wanaenda arijojo. Baada ya kuuua ujamaa chama kilikabidhiwa wafanyabiashara na mafisadi walioliibia taifa na kuifilisi nchi katika kila nyanja. CCM imekuwa na tabiaya kuwaua au kuwanyanyasa "Manabii" walioibuka kuitetea. Tumeshuhudia kifo cha kutatanisha cha Kolimba na hata Nyerere mwenyewe, na wengi tu ambao sasa ni mashahidi wa CCM kupoteza mwelekeo. Mimi naona Falsafa za CCM ni umafia na ufisadi unaofunikwa na blanketi zito la ulaghai uluoundiwa idara maalum chini ya mwanafunzi msaliti wa Nyerere - Kingunge Ngombale Mwiru anayeongoza idara ya Propaganda! Nasikia sasa amemrithisha kijana mwingine msaliti - Nape Nauye ambaye kwa vyovyote vile ni msaliti wa baba yake aliyekufa akiwa mjamaa wa kweli na Tanzania ikiwa ndani ya damu yake! Sasa kijana wake ameshanunuliwa na mahasidi wa ujamaa na anazurura akifoka kuwa tetea wezi na vibaka mpaka povu linamtoka! Wakati CCM imeingiwa na virusi vya ufisadi katika nyanja zote yeye anasema idadi yao inajulikana! ukweli ni kwamba CCM nzima sasa imeoza kwa kuwa chaka la wezi, waporaji wa rasilimali za Taifa na vibakauchumi kiasi cha wote kutoaminika; kuanzia Rais hadi tarishi.
 
Falsafa ya Chama​
  1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika “Nguvu na Mamlaka ya Umma” (The People’s Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
  2. Aidha falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
  3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
  4. Historia inaonyesha kuwa “UMMA” wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
  5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka “Nguvu ya Umma”. Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
  6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa “kuchaguliwa” kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza “waliowachagua” kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
  7. Hivyo basi, falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
  8. Falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.

Kwa hayo yote uliyo yasema hapo juu niki summarize ni kuwa falsafa ya CHADEMA ni udini + ukabila + ukanda ! Hongera kwa kutujuza
 
Jamani CCM kinavyoadhirika hivi sana kwa kudandia kila kitu hadi hoja za wengine tu inasikitisha kweli kweli.

Tangu chama hiki kijitangazie kule Zanzibar kwamba tangu wakati huo kimeachana na Sera tanzu ya UJAMAA NA KUJITEGEMEA na kukumbatia mfumo mpya wa Soko Huria, nasema hadi leo hakijulikani kimatendo kwamba hasa wenzetu wanafuata dira na falsafagani kuleta maendeleo nchini.

Siku zote jitihada kubwa bila kuwa na malengo ni kazi bure, sijui kukifanyia tathmini hii serikali ya Kikwete ndio hasa watu tukaanzie wapi hivyo!!!!!

Sijui kama wanakusoma vizuri maana unasema kitu hapa:frusty:
 
Prof Shivji anawasaidia sana CCM, lakini wameweka pamba masikioni, Dira ya CCM ilikuwa Azimio la Arusha, kwa sasa hawana dira wala falsafa. Badala ya kukaa chini na kutafakeri, wanazungumzia kumvua kobe gamba.
 
Falsafa ya Chama​

  1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika “Nguvu na Mamlaka ya Umma” (The People’s Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
  2. Aidha falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
  3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
  4. Historia inaonyesha kuwa “UMMA” wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
  5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka “Nguvu ya Umma”. Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
  6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa “kuchaguliwa” kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza “waliowachagua” kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
  7. Hivyo basi, falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
  8. Falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.

Falsafa ya ni kuuza mali ya nchi kwa wageni na Ufisadi
 
Hata A Mwamri anajua.
Hata Mwalimu alijua

Lakini miaka kadhaa baadaye, Muasisi na Mwenyekiti wa kwanza wa CCM, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitamka wazi kwamba CCM haifuati siasa ya ujamaa na kujitegemea, nikinukuu kitabu chake cha uongozi wetu na hatma ya Tanzania : Halmashauri Kuu ya Taifa iliketi Unguja ikabadili Azimio la Arusha bila kwanza kutafuta maoni ya wananchi.Na walikuwa na haki ya kufanya hivyo, maana sera ni yao, ubaya wao ni kwamba jambo lenyewe walilifanya kwa hila na hadi sasa wanaendelea kuwadanganya wananchi kwamba sera ya CCM bado ni Ujamaa na Kujitegemea.’ Haya ni maneno ya kiongozi ambaye alishiriki moja kwa moja kuandika Azimio la Arusha na misingi ya siasa ya ujamaa na kujitegemea! Mwaka 2000, mwaka mmoja tu baada ya baba wa Taifa kufariki, serikali ikapeleka bungeni mabadiliko ya Katiba na kuweka tafsiri finyu ya ujamaa na kujitegemea! Mwaka 2006, Agrey Mwanri-Mbunge wa CCM akichangia katika Bunge la Kwanza la Bajeti alijenga hoja nzito kwamba nchi hii haina itikadi, kinachoendelea hapa ni shughuli tupu. Mwaka 2007, Agrey Mwanri huyo huyo, baada ya kuteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, alijenga hoja kinzani wakati wa kuchangia mjadala kuhusu muswada wa rushwa; kwamba nchi yetu bado inafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea. Na kwamba bila siasa hii; mustakabali wa taifa utakuwa mashakani. Hapa ndipo tulipofika! Je, mustakabali wetu hauko shakani?
 
Ninavyofahamu mimi, falsafa ya CCM ni kuwa:
1) Chama cha Wakulima na Wafanyakazi (ingawa siku hizi hata wafanyabiashara ni chama chao)
1) Binadamu wote ni sawa (ingawa si sawasawa).
2) Ili tuendelee tunahitahi ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora.
3) Ujamaa na Kujitetea ndio njia pekee ya kujenga Taifa la watu walio sawa na huru.
 
Kama vile kuna mtu alisoma kile kitabu cha animal farm na sasa anakijaribisha ndani ya CCM. Is a good experiment, let us see.
 
Falsa ya CCM imejengeka katika imani ya Binadamu wote ni sawa, kuanzia hapo ndipo linakuja suala la ujamaa, sasa suala la kama CCm inaonekanaje kwa miwani yako hilo ni lako binafsi lakini kuna watu wengi bado wanaamini katika CCM na utu, japo kwenye kundi la mamba kenge hawakosi.

binadamu wote ni sawa ili litakua jambo jipya sana ndani ya ccm kwa sasa,kwanza kama falsafa yenu ni hii basi mmepoteza dira kama inavyosemekana
 
Ndio maana nikasema kama ukisoma kitabu cha animal farm. Wale Hog waliweza kupofusha wenzao macho na hawakuona sahihi tena, kwa hiyo wakawa wanaimba tu kama huyu rafiki yako Ndu**.
 
Sanga, kwa katiba ya ccm toleo la 2010 sidhani kama wana itikadi na sera, ila wana imani za chama, navyojua imani sio lazima ziwe itikadi, ila sera kama chama hawana kwa sababu hazijaainishwa katika katiba yao.
 
Imani hiyo inasemaje? statement of faith inatakiwa itoe dira.
 
Kwa hayo yote uliyo yasema hapo juu niki summarize ni kuwa falsafa ya CHADEMA ni udini + ukabila + ukanda ! Hongera kwa kutujuza

hacha woga njoo utueleze falsafa yenu... Au wewe unapingana na baba wataifa aliyebainisha waziwazi ya kwamba hamna falsafa..
 
Kwa hayo yote uliyo yasema hapo juu niki summarize ni kuwa falsafa ya CHADEMA ni udini + ukabila + ukanda ! Hongera kwa kutujuza

Wewe hujibu swali, falsafa ya CCM ni ipi. Unapiga chenga tu. Au kuvua gamba kuvaa gwanda. maana naona Nape anavaa magwanda siku hizi.
 
Falsafa ya Chama​

  1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika “Nguvu na Mamlaka ya Umma” (The People’s Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
  2. Aidha falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
  3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
  4. Historia inaonyesha kuwa “UMMA” wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
  5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka “Nguvu ya Umma”. Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
  6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa “kuchaguliwa” kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza “waliowachagua” kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
  7. Hivyo basi, falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
  8. Falsafa ya “Nguvu na Mamlaka ya Umma” inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.

na ile ya ukaskazini
 
Back
Top Bottom