Faini zitumike kununua Madawa

Michewen

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
24,567
32,215
Faini mbalimbali (ikiwemo makosa ya barabaran,) zitumike kununua Madawa hospital za Umma na sio kulipana posho
 
Faini mbalimbali (ikiwemo makosa ya barabaran,) zitumike kununua Madawa hospital za Umma na sio kulipana posho
Kwenye matumizi ya rasilimali tuna tatizo kubwa sana. Ila hao wote kwenye meza za maamuzi ni zao la maandalizi mabaya.

Cha kujihoji ni Kwann watumie mapato ya faini kama chanzo tegemezi cha mapato. Hakuna namna yoyote ya kuwa na chanzo cha pato endelevu kinachosaidia kuchochea jamii timamu bila kutegemea akili za wendawazimu??

Siku wakipona wote, wakaacha kufanya makosa tutatoa wapi mapato?! Na nadhani ni sisi tuu utasikia tunajisifia ulevi wa ndani na uvunjifu wa sheria za barabarani umesaidia kuongeza mapato serikali... Ni kama tunawashukuru kwa kuvunja sheria na kuwa walevi wameokoa uchumi

Fikra zetu inabidi zibadilike...huenda ndio maana tunajikuta tunaendelea kuzalisha wapuuzi wengi ..kwa kutokuzingatia loshe Matokeo yake watoto wanazaliwa na not fully developed brains.

Na wakifika hapa Duniani hasa Tanzania kwa sababu wazazi na kila mtu anayewazunguka naye ubongo haukukua sawasawa wanajikula lishe yao inakuwa ya wanga tuu na matokeo wa mtoto ubongo haupati fursa ya kukua sawasawa...

Mtoto anapofikisha miaka miwili na nusu kwenye ukomo wa ukuaji wa ubongo tayari amedumaa ubongo na mwili na kisayansi ndio tusha seal fate yake hapa Duniani. Atabakia kuwa na akili za kuvukia barabara a kujua pini imemchoma.

Mungu Alirehemu Taifa hili Teule na watu Wake. Amina.
 
Back
Top Bottom